Mafunzo ya ujasiriamali na ajira mwanza

bereng

Senior Member
Feb 5, 2013
114
21
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Tuwafikie Tanzania, inapenda kuwakaribisha wakazi wa Mwanza katika mafunzo maalumu ya ujasiriamali yatakayofanyika kuanzia tarehe 16 disemba.
Mafunzo yatakayotolewa ni pamoja na:
-utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo batiki, shampoo, sabuni za maji, mche na unga, dawa za usafi, utengenezaji wa keki, wine, mafuta ya kupaka ya mgando, losheni, manukato, unga wa lishe, mishumaa, nk.
Mafunzo haya yatalenga kuwaandaa wahitimu kuweza kupata ujuzi wa kutengeneza bidhaa zenye ubora. Aidha kutakuwa na nafasi za ajira kwa watakaofanya vizuri ili wawe walimu wa ujasiriamali ktk mradi wetu wa WEZESHA MJASIRIAMALI unaoratibiwa na taasisi kwa kushirikiana na wahisani na mashirika rafiki.
Tumeandaa pia mwalimu maalumu atakayetoa mafunzo haya kwa wasiosikia hivyo tunapokea maombi ya mafunzo kwa wasiosikia, wanaweza kutuma maombi kwa sms au email watajibiwa.

Mafunzo mengine ni uanzishaji na uendelezaji wa taasisi zisizokuwa za kiserikali NGO pamoja na uanzishaji na uendelezaji wa SACCOSS na VICOBA.
Baada ya kuhitimu mafunzo haya kutakuwa na nafasi chache za kazi ya uratibu wa mradi wilayani ktk mkoa wa Mwanza na sehemu zingine mradi utapoanzishwa.

Mafunzo yote yatatolewa kwa gharama nafuu sana. Fomu zinapatikana kwa tsh 5,000. Unaweza kuwasiliana na meneja wa mradi kwa namba 0768 955 185 email:- tuwafikiemwanza@gmail.com.
Tovuti www.tuwafikie.org
 
Watakaopata nafasi ya ajira kushiriki kwenye mradi wetu wa WEZESHA MJASIRIAMALI kama walimu wa ujasiriamali na waratibu, watarudishiwa gharama za mafunzo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom