usiniguse
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 1,724
- 1,188
Nililazimika kutoroka mafunzo ya polisi CCP miaka mitatu iliyopita,kilichonikimbiza ni jinsi mafunzo yalivyokuwa yanatolewa ,kufika tu nilikutana na bango limeandikwa HAKUNA HAKI ZA BINADAMU HAPA nilistuka kidogo na kutaka kujua ni haki zipi hizi .Lilipoanza somo la UVUMILIVU ndilo lililonifanya nikimbie kwani lugha inayotumika ni matusi ambayo kiukweli mengine ni mapya sijawahi kuyasikia, anaitwa mtu(kuruta) na anaitika,mfano tulianza kuitwa ASHAKUM SI MATUSI'WE MKU..DU NILIYEKU ..LA JANA njoo hapa,WE MALAYA MAMAYAKO ALIYETO..BWA UKAPATA NAFASI YA KUJA HAPA NJOO"na matusi mengimengi ya ajabu ambayo huwezi kuamini kuwa yanatoka mdomoni wa wakufunzi ambao ni watu wazima ,na NI LAZIMA UITIKIE NDIYO AFANDE.kiukweli siku ya kwanza nilishudia watoto wa kike wanamwaga chozi na vilio juu.Niliumia sana na kujiuliza hivi jeshi halina njia nyingine ya kufundisha uvumilivu kisaikolojia zaidi ya hii sikupata jibu nikanyoosha mikono juu nikatoroka usiku huohuo.