Michael Chairman
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 922
- 581
Kwa mara nyingine Light and sound meditation Africa ,Inakuletea mafunzo ya kiroho jijini Mwanza yatakayofanyika kwa siku mbili yaani jumamosi na Jumapili 13/14 /4 /2019 kuanzia saa tatu asubuhi ,Maeneo tulivu ya Royal sunset campsite beach Malimbe Luchelele.
Unakaribishwa wewe na familia yako na kwa watu wote njoo tujifunze utamaduni bora na wa kuigwa ambao kila mmoja anapaswa kuwa nao kwa afya ya mwili na akili.
Usuli wake kidogo na faida zake kwako kama utafahamu kufanya na kujifunza Yoga na Meditation....
1. Linapokuja swala la imani na kiroho wengi hufikiri ni kazi ya dini ambazo tunazo , fikra hii yaweza kuwa sawa kama haufahamu unahitaji nini juu ya masuala ya kiroho na uamsho wa kiroho.
2. kukua kiviwango vya kiroho kwenye zama za sasa ni jukumu lako binafsi kujua na kuweka juhudi kulifikia badala ya kusubiri dini zikupatie.
3. kusali na kufanya meditation ndiyo njia kuu ya kujiamsha kiroho wewe binasfi na kutokeza maisha yenye furaha na amani.
4. Kunakusaidia sana kujifahamu na kujijua wewe ulipotoka na hata kujua kwanini upo hapa duniani (kusudi lako nini?)
5. Kujiponya dhidi ya misongo ya mawazo na maumivu ya mwili kama mgongo na misuli na kutuliza akili.
6. Kuondosha hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo na ubongo.
7. Kufanya na kuwa na magunduzi mengi (ubunifu) dhidi ya matatizo ya dunia inayokosa kila siku upendo na amani.
karibuni sana wasiliana na 0759880010 Michael The Great one kwa usaidizi wa kufika Hakuna kiingilio ni bure kabisa mausuala ya kiroho hayana gharama za kuyalipia ni upendo.