Mafunzo ya Lugha ya Kichina katika Afrika yapokelewa kwa dhati kutokana na umuhimu wake duniani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
Na Pili Mwinyi

VCG111157148320.jpg


Kwa muda mrefu sasa China imekuwa ikifungua milango yake na kukaribisha watu kutoka pande mbalimbali duniani kuja China ili kujionea kwa macho yao nchi kubwa iliyopata maendelo ya kasi kwa muda mfupi tu, na pia kuwafanya wachina kwenda nje ili kujionea na kujifunza mengi zaidi. Lakini katika safari yoyote ile ya binadamu mawasiliano ni jambo la muhimu zaidi. Na nyenzo kuu ya mawasiliano ni lugha, ambayo mara nyingi huambatana na utamaduni.

Utamaduni ni muhimu kwasababu upo kama uzi usioonekana kwa macho, ambao unaunganisha watu pamoja ama kuwatenganisha. Ndio maana China, baada ya kufungua milango yake miongoni mwa vitu muhimu ilivyofikiria ni kuwafanya watu wa nje kuifahamu vyema China kupitia lugha na utamaduni wake. Na hapo ndio likaja wazo la kuanzisha taasisi za Confucius duniani.

China ilianza kujenga chuo cha Confucius mwaka 2004 ili kueneza lugha ya Kichina na kuutangaza utamaduni wake duniani, na tangu hapo taasisi hii imeshuhudiwa uwepo wake duniani kote kwa kujengwa vyuo zaidi ya 500, ikiwakilisha nusu ya lengo lake la taasisi 1,000 kufikia mwaka 2020. Katika bara la Afrika, vyuo hivi vya Confucius vimekuwa kama zawadi na pia ni njia ya kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika kwa kuwafanya waafrika waielewe vizuri zaidi China.

Hivi sasa wanafunzi na hata watu wa kawaida katika nchi za Afrika hasa Tanzania wamekuwa na mwamko mkubwa wa kutaka kujifunza lugha ya Kichina, kwani wanaelewa umuhimu na manufaa yake. Kwa upande wa wanafunzi inawaletea fursa ya kupata udhamini wa masomo, na kwa watu wa kawaida hasa wafanya biashara inawapatia fursa ya kuwasiliana kwa urahisi zaidi wakati wanapofanya biashara na wenzao wa China.

Katika kuendeleza juhudi hizo, hivi majuzi wanafunzi na walimu 123 wa Tanzania walitunukiwa tuzo ya “balozi wa China ya mwaka 2021” kwa lengo la kuwahamasisha na kuwazawadia wanafunzi wanaosoma Kichina na kufanya vizuri kwenye mitihani yao. Kwenye hafla ya kutunuku tuzo hizo za nne iliyofanyika kwenye ubalozi wa China jijini Dar es Salaam, Tanzania, Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian alisema katika miaka ya karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la idadi ya wanafunzi wa Tanzania wanaojifunza lugha ya Kichina, na idadi ya shule zinazofundisha kozi ya lugha ya Kichina pia zimeongezeka.

Serikali ya Tanzania ilitangaza kuanza masomo ya mkondo mpya “combinations” kwenye baadhi ya shule kwa wanafunzi wanaoingia kidato cha tano katika mwaka 2021, yaani mkondo wa KFC (Kiswahili, Kifaransa na Kichina) na KEC (Kiswahili, Kingereza na Kichina). Hii inamaanisha kuwa licha ya vyuo vya Confucius kuwepo nchini humo, kozi ya lugha ya Kichina pia imejumuishwa katika mfumo wa elimu ya sekondari wa Tanzania.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, naye pia alishuhudia utoaji wa tuzo hizo, na wakati alipotoa hotuba aliushukuru ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kuendelea kuhimiza ushirikiano wa elimu kati ya pande mbili, na kusema kuwa idadi ya wanafunzi wa Tanzania wanaopewa udhamini wa masomo na serikali ya China imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Tuzo hizo sio tu zinatambua juhudi za wanafunzi wa Tanzania, bali hata juhudi za walimu wanaofundisha Kichina ambao ni Wachina waliopo nchini Tanzania. Kwani kuanzia mwaka jana, nao pia wamekuwa wanufaika wa tuzo hizo.

Watu wa kawaida nao pia wamepokea kwa moyo wa matumaini masomo haya ya lugha ya Kichina, wakiwa na hoja kwamba hivi sasa kuna idadi kubwa sana ya watu duniani wanaongea Kichina, kuna bidhaa nyingi za China ambazo wao wanataka kuzifahamu, China inaongoza katika akili bandia na teknolojia katika karne hii ya 21, pia wanahitaji kujifunza kutoka kwa Wachina, hivyo kwa maoni yao ni vyema wanafunzi na watu wa kawaida wakajifunza Kichina.

Mwaka 1965, China na Tanzania zilisaini "Mkataba wa Urafiki kati ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Vilevile makubaliano mengine mengi ya ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali ikiwemo nyanja ya elimu pia yamesainiwa.
 
Kiingereza kinatosha, wachina wajifunze kiingereza nao watawasiliana na nchi nyingi tu, kuliko kuwapa kazi watu kujifunza lugha yao ngumu...
Labda Waafrika tusiwe kama malaya wanaomeza mb*o ya kila mtu
 
Back
Top Bottom