Mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria ni msalaba kwa wananchi wanyonge. Yafutwe au utaratibu wa zamani urudishwe

Mdaiwa-Sugu

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
284
910
Tangu serikali isitishe kugharamia mafunzo ya JKT - mujibu wa sheria kwa 100% kama awali, hali imekuwa ngumu zaidi kwa upande wa wananchi na kupelekea wanafunzi wengi kushindwa kuhudhuria mafunzo hayo.

Zamani kuanzia mwaka 2015 kurudi nyuma ilikuwa mwanafunzi akichaguliwa kwenda JKT kwa mujibu wa sheria alikuwa akigharamiwa mahitaji yote. Vitu kama bukta, raba, t-shirt, mashuka, vyandarua na mablanketi walikuwa wakipatiwa bure kwenye makambi ya jeshi.

Vile vile, serikali ilikuwa ikigharamia nauli za kwenda na kurudi pamoja na posho kila mwezi kwa wanafunzi.

ingawa posho bado wanapewa, shida kubwa ipo kwenye mahitaji mengine hasa nauli ya kwenda na kurudi. Hapa ndipo kuna tatizo kubwa kiasi kwamba wazazi wanashindwa kumudu gharama za kuwapeleka watoto wao kuhudhuria mafunzo hayo ya jeshi.

Chukulia mfano, mwanafunzi wa Ngara-Kagera achaguliwe kwenda Nachingwea JKT mkoani Lindi. Nauli ya kutoka ngara kwenda nachingwea haiwezi kuwa chini ya elfu tisini jumla na kurudi inakuwa Laki na themanini. Hiyo ni nauli tu anayopaswa kuiandaa mzazi achilia mbali pesa ya chakula njiani.

Kama hiyo haitoshi, mzazi anatakiwa kununua pit short, green vest, raba, mashuka na mahitaji mengine yanayotakiwa.

Ni katika kipindi hicho hicho kifupi mzazi anatakiwa kuandaa pesa, elfu thelathini kwaajili ya mwanae kuomba mkopo wa elimu ya juu. Ndani ya kipindi hicho hicho mzazi anatakiwa kuandaa pesa, elfu hamsini kwa ajili ya kuombea vyuo achilia mbali gharama za hapa na pale kama kulipia RITA nakadhalika.

Ukijumlisha gharama zote kwa hesabu ya haraka haraka mzazi anatakiwa kuandaa si chini ya laki tatu kukamilisha mambo yote hayo.

Laki tatu kwa Mtanzania wa kipato cha chini ni hela kubwa kuipata kwa muda mfupi kwahiyo inafikia hatua mzazi anahairisha kumpeleka mwanae JKT ili kupunguza gharama na kubakisha jukumu moja tu la kumhudumia mwanae kwenda chuo.

Wito wangu kwa serikali yangu ya awamu ya tano.

Naiomba serikali yangu irudishe utaratibu wa kuwalipia nauli na mahitaji mengine wanafunzi wote wanaochaguliwa kwenda JKT na kama hilo haliwezekaniki basi mafunzo ya JKT mujibu wa sheria yafutwe kwa sababu yanawanyima fursa wanafunzi wanaotoka familia maskini kuhudhuria na kulitumikia taifa kupitia mafunzo hayo awali ya kijeshi.

Nawasilisha.
 
Zamani ni tofauti na sasa,kipindi kile vijana waliandaliwa katika kujenga nchi kijamaa.
Hivyo mahitaji yote yaliandaliwa na Serikali kuu iliyokuwa inamiliki njia zote za uchumi.
Leo hii vijana wanajiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ili kukuza uzalendo katika kujitegemea ili kuijenga nchi.
Hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuandaa mazingira rafiki ya kusaidia juhudi za nchi kujitegemea.
Matokeo ya kuchangia ni mengi kuliko kutokuchangia, kwani baadhi ya mahitaji muhimu yanayohitajika yanawanufaisha wananchi moja kwa moja.
 
Tangu serikali isitishe kugharamia mafunzo ya JKT - mujibu wa sheria kwa 100% kama awali, hali imekuwa ngumu zaidi kwa upande wa wananchi na kupelekea wanafunzi wengi kushindwa kuhudhuria mafunzo hayo.

Zamani kuanzia mwaka 2015 kurudi nyuma ilikuwa mwanafunzi akichaguliwa kwenda JKT kwa mujibu wa sheria alikuwa akigharamiwa mahitaji yote. Vitu kama bukta, raba, t-shirt, mashuka, vyandarua na mablanketi walikuwa wakipatiwa bure kwenye makambi ya jeshi.

Vile vile, serikali ilikuwa ikigharamia nauli za kwenda na kurudi pamoja na posho kila mwezi kwa wanafunzi.

ingawa posho bado wanapewa, shida kubwa ipo kwenye mahitaji mengine hasa nauli ya kwenda na kurudi. Hapa ndipo kuna tatizo kubwa kiasi kwamba wazazi wanashindwa kumudu gharama za kuwapeleka watoto wao kuhudhuria mafunzo hayo ya jeshi.

Chukulia mfano, mwanafunzi wa Ngara-Kagera achaguliwe kwenda Nachingwea JKT mkoani Lindi. Nauli ya kutoka ngara kwenda nachingwea haiwezi kuwa chini ya elfu tisini jumla na kurudi inakuwa Laki na themanini. Hiyo ni nauli tu anayopaswa kuiandaa mzazi achilia mbali pesa ya chakula njiani.

Kama hiyo haitoshi, mzazi anatakiwa kununua pit short, green vest, raba, mashuka na mahitaji mengine yanayotakiwa.

Ni katika kipindi hicho hicho kifupi mzazi anatakiwa kuandaa pesa, elfu thelathini kwaajili ya mwanae kuomba mkopo wa elimu ya juu. Ndani ya kipindi hicho hicho mzazi anatakiwa kuandaa pesa, elfu hamsini kwa ajili ya kuombea vyuo achilia mbali gharama za hapa na pale kama kulipia RITA nakadhalika.

Ukijumlisha gharama zote kwa hesabu ya haraka haraka mzazi anatakiwa kuandaa si chini ya laki tatu kukamilisha mambo yote hayo.

Laki tatu kwa Mtanzania wa kipato cha chini ni hela kubwa kuipata kwa muda mfupi kwahiyo inafikia hatua mzazi anahairisha kumpeleka mwanae JKT ili kupunguza gharama na kubakisha jukumu moja tu la kumhudumia mwanae kwenda chuo.

Wito wangu kwa serikali yangu ya awamu ya tano.

Naiomba serikali yangu irudishe utaratibu wa kuwalipia nauli na mahitaji mengine wanafunzi wote wanaochaguliwa kwenda JKT na kama hilo haliwezekaniki basi mafunzo ya JKT mujibu wa sheria yafutwe kwa sababu yanawanyima fursa wanafunzi wanaotoka familia maskini kuhudhuria na kulitumikia taifa kupitia mafunzo hayo awali ya kijeshi.

Nawasilisha.
Mwisho wa siku mafunzo yenyewe ni basi tu, yawe ya hiari.
 
Yana Tija kubwa haya mafunzo, yana andaa wazalendo. Taifa linajengwa kwa gharama yeyote iwe ya mwananchi mmoja mmoja au serikal yenyewe. Mtoto wako akienda kule anaenda kuchota maarifa yasiyo fundishwa darasan na pengine wazazi wengine hawawafundishi watoto wao hayo mafunzo. Kwa hiyo kwa mwananchi kuchangia kidogo ni ile dhana ya maendwlwo shirikishi.

Asante Mkuu!
 
Serikali inatakaiwa kugharamia kila kitu, nauli, uniform, buti, kula, matibabu nk. ndo namna hilo jeshi lilivokuwa linaendeshwa, sasa kuanza kubana wazazi watoe pesa zao ni uzwazwa.
 
Mtoa mada amewambia anakubali mafunzo Ni muhimu, ila uwezo ndio Shida. Lipi bpra kumpeleka mtoto jkt Na baadae ushimdwe kulipia gharama za kuomba vyuo? Tena mtoa mada amesahau humo katikati wanapaswa kurudi nyumani kuomba vyuo! Nami napendekeza kwa kuwa mafunzo haya ni muhimu, sasa hivi makusanyo ya serikali yamepanda, hivyo serikali igarimie gharama za mafunzo
 
Tangu serikali isitishe kugharamia mafunzo ya JKT - mujibu wa sheria kwa 100% kama awali, hali imekuwa ngumu zaidi kwa upande wa wananchi na kupelekea wanafunzi wengi kushindwa kuhudhuria mafunzo hayo.

Zamani kuanzia mwaka 2015 kurudi nyuma ilikuwa mwanafunzi akichaguliwa kwenda JKT kwa mujibu wa sheria alikuwa akigharamiwa mahitaji yote. Vitu kama bukta, raba, t-shirt, mashuka, vyandarua na mablanketi walikuwa wakipatiwa bure kwenye makambi ya jeshi.

Vile vile, serikali ilikuwa ikigharamia nauli za kwenda na kurudi pamoja na posho kila mwezi kwa wanafunzi.

ingawa posho bado wanapewa, shida kubwa ipo kwenye mahitaji mengine hasa nauli ya kwenda na kurudi. Hapa ndipo kuna tatizo kubwa kiasi kwamba wazazi wanashindwa kumudu gharama za kuwapeleka watoto wao kuhudhuria mafunzo hayo ya jeshi.

Chukulia mfano, mwanafunzi wa Ngara-Kagera achaguliwe kwenda Nachingwea JKT mkoani Lindi. Nauli ya kutoka ngara kwenda nachingwea haiwezi kuwa chini ya elfu tisini jumla na kurudi inakuwa Laki na themanini. Hiyo ni nauli tu anayopaswa kuiandaa mzazi achilia mbali pesa ya chakula njiani.

Kama hiyo haitoshi, mzazi anatakiwa kununua pit short, green vest, raba, mashuka na mahitaji mengine yanayotakiwa.

Ni katika kipindi hicho hicho kifupi mzazi anatakiwa kuandaa pesa, elfu thelathini kwaajili ya mwanae kuomba mkopo wa elimu ya juu. Ndani ya kipindi hicho hicho mzazi anatakiwa kuandaa pesa, elfu hamsini kwa ajili ya kuombea vyuo achilia mbali gharama za hapa na pale kama kulipia RITA nakadhalika.

Ukijumlisha gharama zote kwa hesabu ya haraka haraka mzazi anatakiwa kuandaa si chini ya laki tatu kukamilisha mambo yote hayo.

Laki tatu kwa Mtanzania wa kipato cha chini ni hela kubwa kuipata kwa muda mfupi kwahiyo inafikia hatua mzazi anahairisha kumpeleka mwanae JKT ili kupunguza gharama na kubakisha jukumu moja tu la kumhudumia mwanae kwenda chuo.

Wito wangu kwa serikali yangu ya awamu ya tano.

Naiomba serikali yangu irudishe utaratibu wa kuwalipia nauli na mahitaji mengine wanafunzi wote wanaochaguliwa kwenda JKT na kama hilo haliwezekaniki basi mafunzo ya JKT mujibu wa sheria yafutwe kwa sababu yanawanyima fursa wanafunzi wanaotoka familia maskini kuhudhuria na kulitumikia taifa kupitia mafunzo hayo awali ya kijeshi.

Nawasilisha.
Usemavyo ni kweli; kuna kijana wa marehemu kama yangu wa ukoo yeye alimaliza Form IV shule moja ya mission (alisomeshwa bure kama mtoto toka familia duni) Form V kapelekwa Tabora ikabidi niwe mfadhili wake, Jeshini kapangiwa Songea hapo hapo anahitaji kufanya mchakato wa kuomba mkopo na baadaye chuo; huo uwezo atatoa wapi?
 
Tangu serikali isitishe kugharamia mafunzo ya JKT - mujibu wa sheria kwa 100% kama awali, hali imekuwa ngumu zaidi kwa upande wa wananchi na kupelekea wanafunzi wengi kushindwa kuhudhuria mafunzo hayo.

Zamani kuanzia mwaka 2015 kurudi nyuma ilikuwa mwanafunzi akichaguliwa kwenda JKT kwa mujibu wa sheria alikuwa akigharamiwa mahitaji yote. Vitu kama bukta, raba, t-shirt, mashuka, vyandarua na mablanketi walikuwa wakipatiwa bure kwenye makambi ya jeshi.

Vile vile, serikali ilikuwa ikigharamia nauli za kwenda na kurudi pamoja na posho kila mwezi kwa wanafunzi.

ingawa posho bado wanapewa, shida kubwa ipo kwenye mahitaji mengine hasa nauli ya kwenda na kurudi. Hapa ndipo kuna tatizo kubwa kiasi kwamba wazazi wanashindwa kumudu gharama za kuwapeleka watoto wao kuhudhuria mafunzo hayo ya jeshi.

Chukulia mfano, mwanafunzi wa Ngara-Kagera achaguliwe kwenda Nachingwea JKT mkoani Lindi. Nauli ya kutoka ngara kwenda nachingwea haiwezi kuwa chini ya elfu tisini jumla na kurudi inakuwa Laki na themanini. Hiyo ni nauli tu anayopaswa kuiandaa mzazi achilia mbali pesa ya chakula njiani.

Kama hiyo haitoshi, mzazi anatakiwa kununua pit short, green vest, raba, mashuka na mahitaji mengine yanayotakiwa.

Ni katika kipindi hicho hicho kifupi mzazi anatakiwa kuandaa pesa, elfu thelathini kwaajili ya mwanae kuomba mkopo wa elimu ya juu. Ndani ya kipindi hicho hicho mzazi anatakiwa kuandaa pesa, elfu hamsini kwa ajili ya kuombea vyuo achilia mbali gharama za hapa na pale kama kulipia RITA nakadhalika.

Ukijumlisha gharama zote kwa hesabu ya haraka haraka mzazi anatakiwa kuandaa si chini ya laki tatu kukamilisha mambo yote hayo.

Laki tatu kwa Mtanzania wa kipato cha chini ni hela kubwa kuipata kwa muda mfupi kwahiyo inafikia hatua mzazi anahairisha kumpeleka mwanae JKT ili kupunguza gharama na kubakisha jukumu moja tu la kumhudumia mwanae kwenda chuo.

Wito wangu kwa serikali yangu ya awamu ya tano.

Naiomba serikali yangu irudishe utaratibu wa kuwalipia nauli na mahitaji mengine wanafunzi wote wanaochaguliwa kwenda JKT na kama hilo haliwezekaniki basi mafunzo ya JKT mujibu wa sheria yafutwe kwa sababu yanawanyima fursa wanafunzi wanaotoka familia maskini kuhudhuria na kulitumikia taifa kupitia mafunzo hayo awali ya kijeshi.

Nawasilisha.
Sasa mtoto anamaliza form six unajua mbele yake kuna chuo na mafunzo ya hiari unasemaje tena ni muda mfupi?
 
Mafunzo haya ni muhimubkwa kujenga uzalendo uliotukuka sema tu hujui.Ukitaka kujua jiulize kwa nini JWTZ ni moja ya taasisi iliyobaki na heshima kubwa nchini
 
Tangu serikali isitishe kugharamia mafunzo ya JKT - mujibu wa sheria kwa 100% kama awali, hali imekuwa ngumu zaidi kwa upande wa wananchi na kupelekea wanafunzi wengi kushindwa kuhudhuria mafunzo hayo.

Zamani kuanzia mwaka 2015 kurudi nyuma ilikuwa mwanafunzi akichaguliwa kwenda JKT kwa mujibu wa sheria alikuwa akigharamiwa mahitaji yote. Vitu kama bukta, raba, t-shirt, mashuka, vyandarua na mablanketi walikuwa wakipatiwa bure kwenye makambi ya jeshi.

Vile vile, serikali ilikuwa ikigharamia nauli za kwenda na kurudi pamoja na posho kila mwezi kwa wanafunzi.

ingawa posho bado wanapewa, shida kubwa ipo kwenye mahitaji mengine hasa nauli ya kwenda na kurudi. Hapa ndipo kuna tatizo kubwa kiasi kwamba wazazi wanashindwa kumudu gharama za kuwapeleka watoto wao kuhudhuria mafunzo hayo ya jeshi.

Chukulia mfano, mwanafunzi wa Ngara-Kagera achaguliwe kwenda Nachingwea JKT mkoani Lindi. Nauli ya kutoka ngara kwenda nachingwea haiwezi kuwa chini ya elfu tisini jumla na kurudi inakuwa Laki na themanini. Hiyo ni nauli tu anayopaswa kuiandaa mzazi achilia mbali pesa ya chakula njiani.

Kama hiyo haitoshi, mzazi anatakiwa kununua pit short, green vest, raba, mashuka na mahitaji mengine yanayotakiwa.

Ni katika kipindi hicho hicho kifupi mzazi anatakiwa kuandaa pesa, elfu thelathini kwaajili ya mwanae kuomba mkopo wa elimu ya juu. Ndani ya kipindi hicho hicho mzazi anatakiwa kuandaa pesa, elfu hamsini kwa ajili ya kuombea vyuo achilia mbali gharama za hapa na pale kama kulipia RITA nakadhalika.

Ukijumlisha gharama zote kwa hesabu ya haraka haraka mzazi anatakiwa kuandaa si chini ya laki tatu kukamilisha mambo yote hayo.

Laki tatu kwa Mtanzania wa kipato cha chini ni hela kubwa kuipata kwa muda mfupi kwahiyo inafikia hatua mzazi anahairisha kumpeleka mwanae JKT ili kupunguza gharama na kubakisha jukumu moja tu la kumhudumia mwanae kwenda chuo.

Wito wangu kwa serikali yangu ya awamu ya tano.

Naiomba serikali yangu irudishe utaratibu wa kuwalipia nauli na mahitaji mengine wanafunzi wote wanaochaguliwa kwenda JKT na kama hilo haliwezekaniki basi mafunzo ya JKT mujibu wa sheria yafutwe kwa sababu yanawanyima fursa wanafunzi wanaotoka familia maskini kuhudhuria na kulitumikia taifa kupitia mafunzo hayo awali ya kijeshi.

Nawasilisha.
Kwani nauli ya kwenda na kurudi unalipa mala ngapi?!!
 
Watanzania wanapoitwa wanyonge huku wakitupiwa kila mzigo waubebe wenyewe kuna tofauti gani na kutukanwa ?
 
Kwa sasa hivi, wengi hawaendi. Na hilo, linatokana na kukosa fedha za hayo mahitaji, pamoja na nauli.
Wanaomshangaa huyu aliyeleta hoja hii, sina shaka ni wale ambao hawajakutana na shughuri hii. Binafsi, nilivyopata taabu kugharamia issue hiyo, sina hamu tena. Mtoto kutoka Mwanza, kwenda Kigoma. Baada ya muda mfupi, ilibidi arudi kuomba vyuo, kisha arudi tena huko. Kakaribia kumaliza, naambiwa nimtumie nauli. Na bado, kulikuwa na matumizi mengine niliyokuwa nahitajika kugharamia, ikiwa ni pamoja na maji ya kunywa.
Kwa wenye kipato kidogo, huo ni mzigo mkubwa sana!
 
Back
Top Bottom