Mafunzo nyuma ya mrejesho wa kinachoendelea mahakamani kesi ya CCM dhidi ya wananchi

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,798
11,881
Uzi huu, ni maalumu kwa kuandika mafunzo unayoyapata kutokana na kesi namba 16/2020 inayoendeshwa katika mahakama kuu kitengo cha ufisadi na uhujumu uchumi. Ninaomba tukutane hapa kufanya majumuisho ya mafunzo yakini. Kwa upande wangu:-

1. Ninaona kana kwamba polisi wanafanya kazi nzuri wakiwa upande wako, wowote bila kujali misingi ya haki na sheria.

2. Serikali ipeleke mswada wa vyombo vya habari, angalau watangazaji wawe na uwezo wa kusoma hata kwa kiswahili. Hii imetokana na wale makundi wanaotoa mrejesho kwa kuonyesha kabisa hawawezi kusoma achilia mbali maneno machache ya kiingereza, lakini hata kiswahili. Hii idara ni muhimu sana kwa mawasilianao Ikiachwa kuwa na viwango ninavyoviona, mwisho wa siku taifa litalia. Kinachoiogopesha ni kutokujua kama hawa ndio wanaotaka wapewe uhuru usiosimamiwa, wafany awatakalo. Kwa kweli kwa viwango hivi hapana. Kama idara ya habari inataka autonomy kubwa, wabadilishe vigezo vya waajiriwa wao.

3. Kutoka kwa hao hao watangazaji, hata lugha ya kishwahili hawajui. Unasikia wanajiumauma, kuahidiwa, wana sema kuhaidiwa. Kuahirishwa wanasema kuhairishwa, hatari wanasema atari, hayawi wanasema ayawi. Hivi hawa watu huko wanakosomea elimu ya awali na taaluma wanatumia lugha gani? I m not attacking anyone lakini ninaomba maboresho makubwa sana. Hii inashusha hadhi ya sekta na ndiyo sababu hawawezi kupewa uhuru wanaoutaka kwa sababu ya viwango vyilivyo. Kikubwa maboresho.

4. Tuendelee na orodha ya masomo.
 
5.Nimegundua kuwa ni muhimu sana kila mtu kujifunza na kujua jinsi ya kujibu maswali ya cross examination kwani muda wowote mtu unaweza kuwa mahakamani kwa kuwa mahakamani ni sawa na hospitali tu.

Mambo yanayoendelea kwenye hii kesi jinsi ambavyo mashahidi wanajibu maswali wakati wa cross examination ni aibu na yamenifedhehesha sana.

Imagine shahidi alidai kuwa aliiona detention register kisha wakili wa serikali anakuja kumuuliza kuwa kati yako wewe na Polisi ni nani anaijua detention register zaidi kisha shahidi anaingia chaka na kujibu kuwa ni Polisi!

Au shahidi anatoa ushahidi kuwa yupo kwenye ndoa bila ya kutoa cheti cha ndoa mahakamani kisha wakili wa serikali anakuja kumuuliza kuwa;hukuleta cheti chako cha ndoa hapa mahakamani,jibu kweli au siyo kweli?Kisha shahidi anaingia chaka na kujibu kuwa ni kweli bila ya kujua kuwa kuna mbinu za kujibu maswali kama hayo!

Imebidi niingie google fasta sana na kuanza kujifunza jinsi ya kujibu maswali ya cross examination pamoja na jinsi ya kuuliza maswali hayo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom