Mafunzo muhimu kwa watoto wa shule ya msingi na sekondari

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,897
3,338
KUWA NA MAONO YA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA MAZINGIRA YA UTANDAWAZI

(8 – 12TH & 15 – 20TH DECEMBER 2014 – KILIMANJARO, ARUSHA, MWANZA & DAR ES SALAAM)

"Mafanikio yako Mikononi mwa Waaminio Katika Uzuri wa Ndoto zao” ~Eleanor Roosevelt.

Visionary Students’ Network ni mtandao unaounganisha wanafunzi kuanzia ngazi ya elimu ya msingi hadi vyuo vikuu. Tunatarajia kutoa mafunzo yanayohusu maisha halisi katika ulimwengu tuishio sasa kwa watoto wa kuanzia darasa la tano na vijana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Mafunzo hayo yatahusisha maswala mbalimbali ambayo watoto na vijana hawapati fursa ya kuyafahamu kwani hayafundishwi mashuleni na pia kwa bahati mbaya zaidi hata kwenye ngazi ya familia hawayapati pia.

Kwa vijana wa sekondari mafunzo hayo yatahusu “kuwa na maono ya mafanikio makubwa katika mazingira ya kiutandawazi” na washiriki wataweza kupata ufahamu juu ya mambo msingi yahusuyo maisha kama vile:- maisha, urafiki na fedha, pamoja na kujiwekea na kuishi kwa malengo/kufuata maono. Washiriki watafundishwa mbinu mbalimbali za kupanga na kufuatilia mwelekeo wao katika kufanikisha malengo/ndoto zao katika maisha.

Ili kumwezesha kila mshiriki anufaike ipasavyo na mafunzo yetu, mbinu shirikishi zitatumika ili kuwafanya washiriki kikamilifu. Washiriki watashirikishana uzoefu wao kwa kufanya majadiliano na midahalo. Vilevile watafanya maigozi, michezo mbalimbali pamoja na simulizi za hadithi ili kuongeza uchangamfu na hivyo basi kufanya mafunzo hayo yawe na ufanisi mkubwa kwa kuwafanya washiriki waelewe maudhui ya mafunzo kikamilifu.
Yaliyomo kwenye Mafunzo

SEHEMU YA KWANZA: MAISHA, URAFIKI, NA PESA

i. Maisha

Kipengele hiki kinalenga katika kuwafanya washiriki wajue ukweli kuhusu maisha, na watajifunza yafuatayo:

Maana ya maisha

Umuhimu na thamani ya maisha

Maisha na mazingira/viumbe hai

Kukabiliana na changamoto za utandawazi

ii. Urafiki

Maana ya Urafiki

Umuhimu wa kuwa na marafiki

Aina za Marafiki (wazuri/wabaya) faida na hasara zake

Madhara ya kufuata mkumbo na jinsi ya kukabiliana na mkumbo

Jinsi ya kutengeneza marafiki wazuri

Utandawazi na madhara yake (faida na hasara)

Athari za mitandao ya kijamii

Jinsi ya kujinufaisha na utandawazi/Matumizi sahihi ya teknolojia

iii. Pesa

Maana ya pesa

Umuhimu wa pesa

Jinsi ya kutafuta pesa safi (madhara ya pesa haramu)

Matumizi sahihi ya pesa

Umuhimu wa kuheshimu na kutunza pesa na namna za kuzitunza

Uwekezaji sahihi wa pesa ili kuzalisha zaidi

Kusaidia jamii/wanaohitaji pale unapokuwa na pesa za ziada

SEHEMU YA PILI: NDOTO/KUWA NA MALENGO YA MAFANIKIO KATIKA MAZINGIRA YA UTANDAWAZI

i. Maana ya maono/ndoto/njozi/malengo

ii. Kuna umuhimu gani wa kuwa na maono/malengo/ndoto?

iii. Kujiwekea mipango ili uweze kufanikiwa

iv. Mchakato wa kujiwekea malengo

v. Kuwa na malengo makubwa

vi. Kuzingatia dira na kuhakikisha kuwa unakuwa na alama nzuri katika masomo yako

Sisi Visionary Students’ Network tuna dhamira ya dhati ya kuwaendeleza watoto na vijana kwa kuwawezesha waweze kukabiliana na changamoto za utandawazi. Tunalenga katika masuala yafuatayo: kuwa na watoto na vijana wenye malengo/ndoto kubwa; kujiamini kwa kiasi kikubwa; wanaojitambua; wenye mitizamo chanya pamoja na kujijengea ujuzi unaokubalika na soko la ajira kitaifa na kimataifa.

Wasiliana nasi:

Simu: +255 766 063158

Barua Pepe: info@vistunet.com

Kama una mtoto au watoto na ungependa wahudhurie semina hii kwa ajili ya kujifunza mambo haya muhimu tafadhali bonyeza maandishi haya na ujaze fomu.

Karibuni sana.
 
Back
Top Bottom