MAFUNZO:Magonjwa makuu,dalili,tiba na chanjo kwa kuku

soloman

Member
Aug 12, 2015
11
0
Mafunzo haya ni ya wiki moja ambayo yanaendeshwa na kusimamiwa na Tanzania Youth Entrepreneurship and Empowerment Organization yenye usajili namba 00NGO/00006706.

Lengo la mafunzo haya ni kuwasaidia wajasiriamali wapya na wazamani,wadogo na wakubwa ambao wamewekeza katika ufugaji wa ndege.

Mafunzo haya yataanza tarehe 1 February 2016 Katika jengo la TYEEO Gongolamboto Dar es salaam.

Baada ya semina iliyopita kujifunza namna ya uaandaaji mabanda ya kuku na usafishaji wake;semina ya safari hii itajikita zaidi katika kuchambua aina ya magonjwa makuu yanayo athiri ndege aina zote hasa hasa kuku.

Uchambuzi huu utaenda sambamba na kutambua dalili za ugonjwa husika,tiba yake pamoja na chanjo ya ugonjwa huo.

Kwa wale wajasiriamali mnakaribishwa tena katika darasa hili katika tarehe iliyo tajwa hapo juu.

Maada kuu zitakazo jadiliwa ni magonjwa,dalili na tiba.
Vitabu vitaolewa bure.Nyote mnakaribishwa.


A. MAGONJWA
Magonjwa makuu yatakayo tazamwa

1. Magonjwa ya virusi
i. Mafua Makali ya Ndege
ii. Ndui ya Kuku
iii. Mareksi
iv. Mdondo/Kideri
v. Ugonjwa Unaoathiri Mfumo wa Fahamu
vi. Saratani ya Kuku
vii. Gumboro

2. Magonjwa yanayo letwa na bacteria
(i). Magonjwa ya mfumo wa Hewa
(ii). Kuharisha Kinyesi Cheupe
(iii). Homa ya Matumbo
(iv). Kampilobakta
(v). Kolibasilosi
(vi). Kipindupindu cha Kuku

3. Magonjwa mengine
(i) Magonjwa Muhimu ya Protozoa
(ii) Maonjwa ya minyoo
(iii) Magonjwa ya ngozi na wadudu wanaoshambulia ngozi
(iv) Maonjwa ya fangasi
(v) Upungufu wa lishe

A. DALILI
Tutatazama dalili za kila ugonjwa namna ya kutambua dalili kwa kuku ambae yuko hai au kukagua dalili katika mizoga.

B. TIBA NA CHANJO CHANJO
Tutajifunza utaratibu wa utoaji tiba na chanjo sahii kwa kila ugonjwa

Fomu za maombi zinapatikana katika jengo la TYEEO Gongolamboto;yanapo geuzia magari.

Ukishuka stand utakuta ghorofa ndogo nyeupe ina bango la TANZANIA YOUTH ENTREPRENEURSHIP AND EMPOWERMENT ORGANIZATION.Tupo floor ya pili.

Kwa mawasiliano zaidi;-
Block No. 370 – 2BLOCK ESECOND FLOOR
Email: datetz18@yahoo.com
Hotline No: 0657-115587; 0682-202100 or 0654-669431
Mwisho wa kuchukua form ni tarehe 25 january 2016. Nyote mnakaribishwa.
 
Back
Top Bottom