Mafunzo kwa Wajumbe wa UKAWA

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
22,295
49,917
Wanaukumbi.

Pamoja na neno "semina elekezi" kuleta ukakasi masikioni mwa wananchi wengi kutokana na kufanyika mara mbili kwa viongozi wakuu (mawaziri, RCs, na DCs) tena chini ya uenyekiti wa Mh. Rais bila kuleta matokeo yaliyotarajiwa, mtakubaliana nami kwamba semina elekezi ilikuwa na "nia njema" sema "wanafunzi" ndio hawakuelewa kwanini waliandaliwa semina zile tena mwanzoni kabisa; mara tu baada ya uchaguzi au uteuzi.

Kinyume chake taifa likashuhudia mmomonyoko wa maadili wa kutisha, ufisadi wa ajabu, na ulevi wa madaraka miongoni mwa viongozi wa umma hususan walewale waliohudhuria semina husika. Kwamba semina elekezi zilileta tija au la huo ni mjadala mwingine.

Pamoja na mtazamo hasi wa wananchi dhidi ya semina elekezi zilizotangulia, nadhani ingekuwa muhimu kwa viongozi wa nafasi mbalimbali wa UKAWA waliochaguliwa hivi karibuni kufanyiwa mafunzo japo ya wiki moja na ajenda kuu zinaweza kuwa kama hivi:-

(i) Kubadilishana uzoefu - mbinu na changamoto walizokumbana nazo katika kumng'oa "mkoloni mweusi" kwenye maeneo yao.
(ii) Namna ya kukabiliana na changamoto na mbinu chafu za "mkoloni mweusi" katika chaguzi zijazo.
(iii) Kuwa mtumishi wa wananchi - imani na matarajio makubwa ya wananchi kwa UKAWA.
(iv) Propaganda: Namna bora ya kuzitumia na kukabiliana na zile chafu.
(v) Tanzania ilikotoka, ilipo, na iendako kisiasa, kiuchumi, na kijamii.
(vi) n.k. [ongeza]

Mafunzo haya yanaweza kufanyika Mwanza, Mbeya, au Arusha na ni muhimu yarushwe live na vituo vya TV. Baada ya mafuzo kila kiongozi apewe "Job Description" na atoe bianual report ya utekelezaji mojawapo likiwa kueneza elimu ya uraia vijijini na mijini.
 
Mbona kwenye hizo Ajenda sioni yenye manufaa kwa wananchi katika kutatua kero zinazowakabili hasa ikizingatiwa kuwa wagombea wa UKAWA walitumia matatizo ya wananchi kama mtaji wa kisiasa? Sana sana ninachokiona hapo ni kuendeleza siasa za visasi
 
Mbona kwenye hizo Ajenda sioni yenye manufaa kwa wananchi katika kutatua kero zinazowakabili hasa ikizingatiwa kuwa wagombea wa UKAWA walitumia matatizo ya wananchi kama mtaji wa kisiasa? Sana sana ninachokiona hapo ni kuendeleza siasa za visasi

Kero namba moja ya wananchi ni ukosefu elimu ya uraia. Hwajui nani anasema ukweli; Kinana ataongea kana kwamba yuko juu ya serikali, Nape atasema waziri fulani na fulani ni mizigo; Ikulu itasema hakuna waziri mzigo; PM atasema fedha sio za umma, Bunge litasema ni za umma; Mahakama italizuia Bunge kutekeleza majukumu yake, n.k. Yaani wananchi wako confused.
 
Back
Top Bottom