Mafunzo CCP mhhh

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Wadau naomba mchango wenu ..
Je muda wanaoutumia kutoa mafunzo ya askari polisi kwa miezi sita pale CCP unatosha?
-Lini utajifunza uraia na human rights
-Lini utajifunza Law
-Lini utajifunza ukakamavu
-lini utajifunza mbinu na medani za kijeshi za kukabiliana na adui na uhalifu?
-Lini unachunguzwa kama ukikabidhiwa silaha hutaleta nayo madhara?
-Kubwa zaidi ni lini utaenda field kupractise kazi yako before employment? au kujiunga CCP ni already employed
Nakumbuka walioenda National Service kwa mujibu wa Sheria ilikuwa mwaka mzima solid sasa hii ya polisi mhhhh
Hebu tuichambue hii kama ina tija!
 
Kimsingi askari wengi waliopitia mafunzo wa hiyo miezi sita, hawana uelewa wa kutosha juu ya taaluma yao. Muda wa miezi sita ni mfupi sana kitu cha maana pale ni shotokulia vinginevyo ni utata mtupu. Fikiria askari wa mafunzo ya miezi sita kesho ndiyo trafiki, au kitengo cha upelelezi. Nafikiri hawa viongozi wa Jeshi la Polisi waliangalie jambo hili kwa kina maana inawezekana huu ni mzaha katika masuala nyeti na muhimu.
 
Miezi sita inatosha sana wakubwa mengineyo yanapatikana huko huko kazini
haya ndo matokeo kama ya arusha..yaani kufuata oda ya wakubwa hata ukiambiwa unye juu ya meza utatii kwa kuwa mkubwa kasema!! shit
 
Mafunzo ya miezi sita mpaka saba yanatosha. Nadhani hawa mabwana tokea recruit anaingia kuna programe ambayo imeandaliwa kiutalaamu. Miezi ya awali itakuwa ni kuwatoa uraia, yaani ukakamavu baadae kidato kinaanza kama kawa. Mitaala ni lazima itakuwa inabadilika kulingana na wakati mfani sidhani kama maafande wa dep miaka ya 80 -90 kama walikuwa wanajivunza somo la haki za binadamu lakini siku hizi ni tumaini langu mtaala huo utakuwa umejumuishwa katika mafunzo yao ili kuweza kukidhi wakati na mambo mengine.
Mwisho kama utahitajika kwenda mafunzo ya ziada nionavyo ni lazima kuwe na refresh kozi mf. Traffic huwa kuna refresh kozi kwa ajili ya kuwaweka sawa hawa mabwana wasiliaibishe jeshi. Ni kama sisi tu mkuu unaweza kila siku kupewa mahubiri lakini mwisho wa siku ukafanya madudu. Mtazamo wangu muda huo ni muafaka kwani hakuna la ajabu sana katika nchi yetu ambalo litahitaji kuwaweka watu kwa muda huo.
 
kwa ufipi haitoshi hata nusu . washnzi hao wanaoratibu mafunzo. Wenzetu ni 2 years
 
Kimsingi askari wengi waliopitia mafunzo wa hiyo miezi sita, hawana uelewa wa kutosha juu ya taaluma yao. Muda wa miezi sita ni mfupi sana kitu cha maana pale ni shotokulia vinginevyo ni utata mtupu. Fikiria askari wa mafunzo ya miezi sita kesho ndiyo trafiki, au kitengo cha upelelezi. Nafikiri hawa viongozi wa Jeshi la Polisi waliangalie jambo hili kwa kina maana inawezekana huu ni mzaha katika masuala nyeti na muhimu.
pia mfumo ule wa kikoloni wa jeshi la kumkandamiza raia umepitwa na wakati,mbona hii polisi jamii haisongi mbele?
 
Mkuu hebu nisaidie hapo, je unapoingia kule kuna chochote unacholipwa au hadi umalize mafunzo ndio uanze kulipwa?
Ukiwa kama recruit kuna posho wanalipwa kwa sababu wanakuwa bado recruiters hawajaingizwa katika payroll lakini kozi zote zinazofuata wanalipwa kwa sababu wanakuwa ni waajiriwa na wanakuwa waneshakula kiapo cha utii kwa amiri jeshi mkuu au kiapo cha utii wa amri zitolewazo mara kwa mara.
 
pia mfumo ule wa kikoloni wa jeshi la kumkandamiza raia umepitwa na wakati,mbona hii polisi jamii haisongi mbele?
Kuna utofauti lakini huwezi kuuona kirahisi, shida kubwa ya jeshi letu ni kuwa limekaa na linatumika kisiasa lakini lingeacha kutumika kisiasa ni jeshi zuri kabisa miongoni mwa majeshi ndani ya Afrika kwa ujumla.
 
Hapo umenena mkuu...mijamaa inashikishwa SMG haraka sana
Wewe ungekaa JKT miaka miwili ingekuwaje? Chakula kibovu, malazi mabovu n.k lakini wenzetu hata kama ni miaka miwili zile necessities wanazitekeleza. Vile vile hali ya uchumi wa nchi yetu bado ni mdogo ku accommodate kuwaweka watu for two years, na siyo hiyo tu hata ile time interval nayo ni factor kwa sababu unawaweka watu 2000 for 2yrs wakati uhitaji wa ajira ndani ya miaka hiyo miwili ni 8000 soldiers! Inabidi kuwe na muda mfupi halafu baadae hao jamaa unawapa refresh kozi.
 
Wadau naomba mchango wenu ..
Je muda wanaoutumia kutoa mafunzo ya askari polisi kwa miezi sita pale CCP unatosha?
1-Lini utajifunza uraia na human rights
2-Lini utajifunza Law
3-Lini utajifunza ukakamavu
4-lini utajifunza mbinu na medani za kijeshi za kukabiliana na adui na uhalifu?
5-Lini unachunguzwa kama ukikabidhiwa silaha hutaleta nayo madhara?
6-Kubwa zaidi ni lini utaenda field kupractise kazi yako before employment? au kujiunga CCP ni already employed
Nakumbuka walioenda National Service kwa mujibu wa Sheria ilikuwa mwaka mzima solid sasa hii ya polisi mhhhh
Hebu tuichambue hii kama ina tija!

1. Ndo maana hawachukui std 7 tena..unatakiwa uwe umeshavijua kabla hujajiunga! sanasana hapo unaenda kuongezewa zile zihusuzo kazi yako!

2 - 6 Ndani ya miezi sita!!!
it is quite enaf mkuu...you do not make a conclusion on special cases (Arusha, Tarime, etc..)
 
Ukiwa kama recruit kuna posho wanalipwa kwa sababu wanakuwa bado recruiters hawajaingizwa katika payroll lakini kozi zote zinazofuata wanalipwa kwa sababu wanakuwa ni waajiriwa na wanakuwa waneshakula kiapo cha utii kwa amiri jeshi mkuu au kiapo cha utii wa amri zitolewazo mara kwa mara.

Tangu mwaka jana recruits wanalipwa mishahara kama askari aliyemaliza mafunzo
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom