Mafundi umeme wa magari pita hapa

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
24,565
47,012
Habarini wakuu, hapa nimekuja kwa fundi umeme kwajili ya matengenezo ya switch za mlangoni za vioo ila simuelewi nikaona niwashirikishe, naombeni msaada wa kimawazo , nimekutana na changamoto ya power window, sahivi hiyo power window haipandishi kioo cha upande wa dereva ila vingine vyote vinapanda, ni baada ya kutoka car wash, vijana sijui walitia maji, naona kitu kama hicho, maana ni upande huo wa dereva vingine vinapanda kama kawaida sasa nashindwa kuelewa, nipo kwa fundi hapa ananiambia maswala ya kununua switch mpya yani kagusagusa tu kaja na jibu rahisi hivyo.... Naombeni msaada gari ni IST, kuna mtu ame experience hilo tatizo
 
Huenda motor ya kioo chako imekufa, au contact ndani ya switch ya dereva ina kutu.
Shukrani kwa kutoa anagalau mwanga... Nilienda kwa fundi mwingine tena alikuta maji yalikuwepo ndani ya power window na carbonate kiasi chake baada ya kuchukua nakusafisha bado tatizo likawa pale pale
 
Ngoja nijipange kununua power window mpya tu, kwa makisio zinaweza kuwa bei gani wakuu
 
Ngoja nijipange kununua power window mpya tu, kwa makisio zinaweza kuwa bei gani wakuu
Nin uhakika kuwa motor ya dirisha imekufa, huna haja ya kununua dirisha lote bali ukipata fundi mzuri atakubadilishia brushes kwenye motor hiyo, nadhani zillikuwa zimeshaanza kuchoka hivyo baada ya kuingiliwa na maji ikawa ndiyo basi kabisa. Bei ya brush haizidi dola 4 tu.
 
Nashukuru kiongizi umefafanua vizuri sana,nilikutana na fundi mwingine akasema abadilishe wire yani zile wire zilizokua zinapeleka mawasiliano kwenye button ya kufungua kio cha dereva mbele azingainshe na njia nyingine ila kitachotojea nikitaka kushusha/kupandisha kio changu upande wa dereva basi vitashuka viwili vya mbele,hapo ndipo nikawaza sijui ni nunue tu kimashine kipya na nimekuta wanaviuza 90elfu,naomba uhauri juu ya hilo hizo brush zikoje mkuu,
 
Back
Top Bottom