Mafundi Ujenzi, Carpenters, Plumbers wenye uzoefu wanahitajika haraka

Abdul Ghafur

JF-Expert Member
Sep 18, 2017
610
733
Mafundi ujenzi, plumbers, carpenters wenye uzoefu wanahitajika.

Wawe wenye kuijua kazi zao na kuweza kusimamia wengine wasio na uzoefu. Wakiweza kufundisha itakuwa ni plus.

Location yetu ni Misugusugu, Kibaha, Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Kazi zinaweza kuwa za kusafiri na kuhamahama.

Kwa maelezo zaidi, WhatsApp au Telegram au piga 0625249605 Abdul Ghafur.
 
Vipi mafundi umeme hawaitajiki
Fundi umeme kwa sasa hahitajiki, lakini, ikiwa una uwezo wa kufundisha masomo ya awali ya umeme ambayo yanakubalika na VETA basi unaweza kuja tuongee kufungua darasa la ufundi umeme.

Itakubidi uende VETA ukachukue vigezo na mwongozo wa kufungua darasa la umeme, sisi tutawekeza hapa kwetu Madrassatul Abraar kufungua darasa hilo linalokubalika kitaaluma na kisheria.

Fursa hiyo/hizo ni kwako na kwa yeyote mwenye taaluma ya ufundi wowote ule na anaona anaweza na anakidhi matakwa ya VETA kwa fani yoyote ya ufundi kwa kuufundisha kwa vitendo, sisi hapa Abraar tupo tayari kuwekeza kwenye gharama za kuanzisha darasa hilo / madarasa hayo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Abdul Ghafur 0625249605.
 
Nipo tayari kwa upende wa plumber
Karibu sana uje kujionea na tuongee tunavyofanya shughuli zetu.

Tupo mtaa wa Vitendo, Kata ya Misugusugu, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani. Ukija kwa kutumia usafiri wa mabasi unashuka kituo cha Miyomboni shule au kwa jina lingine Misugusugu shule (usishuke Misugusugu check point), hapo utachukua bodaboda, takriban wote wanafahamu tulipo, unamwambia bodaboda nipeleke Abraar kwa Mzee Ghafur. Unafikishwa.

Kwa maelezo zaidi tupigie 0625249605.
 
Hizi ajira ni za kudumu, zipo wakati wote, kama una fani kati ya hizo au kama unataka kujifunza fani hizo, wasiliana nasi.

Abraar Education Centre; 0656399856.
 
Abraar Education Centre

Fursa za ajira na biashara za sekta ya ujenzi.

1) Mchoraji ramani za ujenzi (full-time au part time).

2) Fundi ujenzi msimamizi (masonry foreman) mzoefu.

3) fundi ujenzi wa tofari (bricklayers ) na plaster.

4) Vibarua (wanafunzi wa ujenzi).

5) mhasibu msaidizi na storekeeper (ujenzi)

6) kampuni au vikundi vya ujenzi kuwa subcontractors.

7) wauzaji wa hardware nabraw materials za ujenzi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Abdul Ghafur whatsapp 0625249605 au mobile 9656399856

Tafadhali wasambazie na wengine.
 
Kuja kujifunza ni kiasi gani?
Kujifunza masomo kwenye sekta ya ujenzi ni bure hulipii kitu, masomo mengine kama Computer course, English course na Arabic course unalipia ada ya Shillingi 1,000 kwa siku.

Sisi tunaitwa Abraar Education Centre

Tuna madarasa ya Computer, English,Arabic, kuunda vifaa vya ujenzi na ujenzi wenyewe masonry). Abraar maana yake ni waja wema. Mobile No. 0656399856 au Whatsapp 0625249605 pia tuna madarasa mengine kadhaa ya fani mbali mbali na mengine yanayotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni.

Tupo mtaa wa Vitendo, kata ya Misugusugu, wilaya ya Kibaha, mkoa wa pwani.

Stendi inaitwa Miyomboni Shule au Misugusugu Shule ya msingi. Ukitokea Dar mjini ipo baada kidogo ya kupita Kongowe.
 
Jamani Mimi nifundi wa kutengeneza madirisha ya aluminum milango kabati na shelfu kwa yeyote mwenye kazi tujulishane tushilikiane kwa Bei lahisi
 
Jamani Mimi nifundi wa kutengeneza madirisha ya aluminum milango kabati na shelfu kwa yeyote mwenye kazi tujulishane tushilikiane kwa Bei lahisi
Kama upo tayari kuja kufanyia kazi zako hapa Abraar Education Centre, Misugusugu, Kibaha tuwasiliane kwa whatsapp 0625249605.

Tunachozingatia hapa ni ufundi bora, nidhamu za ufundi na miiko ya ufundi.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom