'Mafundi Tanesco fanyeni kazi saa 24'

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,878
2,000
'Mafundi Tanesco fanyeni kazi saa 24'


Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 7th December 2010 @ 06:26

WAKATI makali ya mgawo wa umeme yakiendelea kuwaumiza wananchi , Serikali imewaagiza mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kufanya kazi kwa saa 24 ili kuharakisha ufungaji wa transfoma ya megawati 36 iliyopo katika Kituo Kidogo cha Kipawa Dar es Salaam ili kupunguza makali ya mgawo huo.

Aidha, wenyewe wamesema wakifanya kazi kwa saa 24 kwa kupeana zamu, watamaliza kwa siku nane.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo alitoa maagizo hayo jana Dar es Salaam wakati alipofanya ziara katika kituo hicho.

“Natoa wito kwenu muongeze kasi ili kupunguza makali ya mgawo wa umeme…mgawo huu unaathiri uchumi wetu kwa kiasi kikubwa,” alisema Jairo.

Kituo hicho cha Kipawa kina uwezo wa kuzalisha megawati 72, kikihudumia wilaya za Ilala na Temeke na mara nyingine kwa Wilaya ya Kinondoni pale panapotokea dharura; hivyo kuharibika kwa transfoma moja yenye uwezo wa megawati 36 iliyoharibika wiki moja iliyopita, ilisababisha kuongeza makali zaidi ya mgawo.

Katika hali hiyo, Jairo aliwaagiza mafundi hao kuongeza kasi ya kuweka mitambo hiyo ili kupunguza hasara zitokanazo na mgawo wa umeme katika uchumi ambapo Kampuni ya National Contracting Company Limited ya Saudi Arabia ndiyo iliyopewa kandarasi ya kusimika mtambo huo, lakini kutokana na kasi yao kutoridhisha, ndipo mafundi wa Tanesco walipolazimika kuingia kazini ili kuokoa jahazi.

Mapema katika maelezo yake kwa Katibu Mkuu, Meneja wa Mifumo na Usambazaji wa Tanesco, Abdullah Fereshi alisema, kuweka mitambo hiyo kutachukua takribani siku 12 kwani mafundi hao wa Tanesco watakua wakifanya kazi kwa saa 18.

Katika hatua hii, Jairo alihoji iwapo itawezekana kupunguza muda huo ikizingatiwa athari zinazoikumba nchi kutokana na mgawo. “Kama tukifanya kazi kwa saa 24 kwa kupeana zamu tutaweza kumaliza kazi ndani ya siku nane,” alisema Fereshi.

Kuharibika kwa transfoma hiyo kumeongeza makali ya mgawo wa umeme Dar es Salaam, kwani licha ya uharibifu huo, mikoa mingine imekumbwa na mgawo kutokana na uhaba wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme huku mitambo miwili ya kuzalisha umeme katika kituo cha gesi cha Songas cha Ubungo pia ikiharibika.

Umeme unaozalishwa kutokana na maji ni takribani asilimia 51 ilihali umeme unaozalishwa kutokana na vyanzo vingine kama gesi asilia na mafuta ni asilimia 49.

Wakati makali ya mgawo huo yakiendelea, Jairo alisema serikali inachukua hatua kadhaa kushughulikia tatizo hilo, akisema “tumeshatoa pesa kwa IPTL kununua mafuta na mpaka sasa wamezalisha megawati 70…lengo letu ni kuzalisha megawati 100.”

Alitoa changamoto kwa Tanesco kujijengea uwezo kwa kununua vifaa na kuacha kutegemea makandarasi.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,878
2,000
SAKATA LA UMEME


*Mafundi TANESCO waamriwa kukesha
*Kazi hiyo kukamilika ndani ya siku nane
*Transifoma ya Chalinze kuziba pengo Dar


Na Grace Michael
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. David Jairo amemtaka mkandarasi na wataalamu wa TANESCO wanaoshughulikia uwekaji wa transfoma jipya katika Kituo cha Kupooza Umeme cha Kipawa, Dar es Salaam kufanya kazi hiyo usiku na mchana ili
imalizike haraka na kupunguza mgawo wa umeme.

Kutokana na amri hiyo ya kufanya kazi usiku na mchana, siku nane zitatumika katika kumaliza kazi hiyo ili transfoma hiyo ambayo imeazimwa kwenye mradi mwingine wa umeme iweze kuwashwa na kupunguza makali ya mgawo uliopo kwa sasa.

Transifoma hiyo iliyochukuliwa Chalinze, mkoani Pwani ilikuwa mojawapo kati ya nne zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya mradi wa kuboresha umeme katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwamo Pwani, Tanga, Shinyanga na Mwanza.

Tayari suala la mgawo wa umeme limeibua taharuki katika jamii, huku mbunge wa Kigoma Kusini, Bw. David Kafulila akipanga kuwasilisha hoja binafsi ya kutokuwa na imani na Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja kwa kushindwa kwake kumaliza tatizo la umeme ndani ya uongozi wake.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, tangu mwaka 2006 serikali imeshindwa kupunguza tatizo hilo na viongozi wakuu wa serikali na hasa Waziri wa Nishati na Madini mara kadhaa wamekuwa akipotosha Watanzania kuwa serikali inalishughulikia lakini siku hadi siku sekta ya umeme imevuka upeo wa viongozi kiasi cha kauli zao kupoteza imani kwa Watanzania.

Hali hiyo ambayo imeikumba karibu mikoa yote nchini, imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Waziri Ngeleja kuingia madarakani kwa mbwembwe huku akiapa kumaliza kabisa tatizo la mgawo huo nchini.

Akizungumza na mafundi hao jana, Bw. Jairo aliwataka kufanya kazi hiyo kwa umakini na haraka kwa kuwa tatizo la umeme lina athari kubwa za kiuchumi lakini pia linasababisha kero kubwa kwa wananchi.Hili ni janga la kiuchumi hivyo kinachotakiwa ni kufanya kazi usiku na mchana ili kuondokana na hili tatizo,� alisema Bw. Jairo.

Alisema kuwa kuharibika kwa transfoma hiyo ambayo ilikuwa inazalisha megawati 36 za umeme imesababisha kuongeza makali ya mgawo, na ikifungwa mpya itazalisha megawati 44 kutasaidia kupunguza makali hayo.

“Mgawo huu mbali ya kuharibika kwa baadhi ya mitambo lakini umechangiwa na hali ya hewa kama kutokuwepo kwa maji ya kutosha na katika kukabiliana na hili, serikali inachukua hatua mbalimbali za kumaliza tatizo hilo,� alisema Bw. Jairo.

Akielezea walivyojipanga katika kufanya hiyo kazi, Meneja Mwandamizi Udhibiti Mifumo na Njia Kuu za Umeme Bw. Abudullah Fereshi alisema kwa kufanya kazi kwa saa 24 kila siku itawezekana kumaliza kwa huo muda wa siku nane.

Akizungumzia transfoma hiyo, alisema kuwa imechukuliwa kutoka kwenye mradi mwingine wa kuboresha umeme ili kukabiliana na tatizo hili la mgawo wa umeme. Kutokana na hali hiyo, aliwataka wananchi kuwa na matarajio ya kupungua kwa mgawo wa umeme mara baada ya kuwashwa kwa transfoma hilo.
 

Questt

JF-Expert Member
Oct 8, 2009
3,010
1,195
Ila wawe Makini..koz umeme ni Technical Thing and DANGEROUS so inaweza kuwa Haraka watu wapate umeme ila baadae ikawa Vifo au uharibifu wa Vifaa vya Wateja....Upo utaratibu wa kufanya technical Jobs...TANESCO wana yao.....its good kama wataifuata na kuachana na Siasa............
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom