Mafundi simu kubadili IMEI namba za simu: Je, TCRA wamezidiwa ujanja?

Tyupa

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
798
1,000
Kwanza kabisa walitangaza kuzima simu zote ambazo ni bandia lakini cha ajabu ni kwamba TCRA hawana uwezo wa kuzima simu bandia.

Mafundi simu wana akili kuliko TCRA kwa sababu wana uwezo wa kubadli IMEI namba ya simu yeyote. Simu mbovu original imei namba yake inawekwa kwenye simu fake na inafanya kazi kama kawaida.

Simu zilizoibwa na wenyewe wakaamua kuzifunga ili alieiba ashindwe kutumia zoezi hilo haliwezekani kwa sababu mafundi simu wanabadili IMEI namba na simu inaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Kwa hiyo wizi wa simu ni kama kawaida tu. Baadhi ya mafundi simu wameandika tangazo kabisa kuwa pamoja na kutengeneza simu pia anabadili IMEI namba. Sasa je TCRA wanajua hili na kama wanajua ina maana wamezidiwa ujanja na mafundi?

Tunawaomba TCRA watujulishe kuwa haya mambo mawili niliyoyataja yako nje ya uwezo wao na hivyo masimu fake yaendelee kuzagaa kuliko ilivyo kuwa mwanzo. Na wezi nao waendelee tu kuiba simu za watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,771
2,000
Kule Korea ya Kaskazini udhibiti wa mawasiliano ni chombo cha kulia cha wanasiasa wenye madaraka ili wasikosolewe wakaonekana kuwa wao pia wanakosea kama binadamu wengine.

Sidhani kama waliingia gharama kubwa kuundo chombo kama hicho kwa ajili ya kuzuia wanyonge wasiibiwe simu .Sent using Jamii Forums mobile app
 
sungwa.j

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
473
500
Tunaomba wahusika TCRA watuelimishe imekaaje hadi mafundi mitaani waizidi serkali akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi nipo Mwanza na ni fundi simu hili suala la kubadili Imei no.mi naona halipo kwa sasa na TCRA Mwanza wametudhibiti sana na tumeshaelewa ni kosa la jinai na siamini kama kuna fundi anayeweza kubadili imei no.Mwanza wewe kama unabisha ukija Mwanza kama haupo hapa jaribu kizungu na simu yako ukitaka ku change imei no.hakuna atayepokea simu yako,nani asiyeogopa Tcra? Nani anayependa kufungwa au kulipa mamilioni kwa ajiri ya kuchange imei no.? Huku Mwanza Tcra wapo Moto,kiasi kwamba ukileta simu yako mafundi wanajua umetumwa na TCRA
.

Ukifika Mwanza zunguka na simu yako ukitaka ibadirishwe hutafanikiwa baba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaby'z

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
3,815
2,000
Mi nipo Mwanza na ni fundi simu hili suala la kubadili Imei no.mi naona halipo kwa sasa na TCRA Mwanza wametudhibiti sana na tumeshaelewa ni kosa la jinai na siamini kama kuna fundi anayeweza kubadili imei no.Mwanza wewe kama unabisha ukija Mwanza kama haupo hapa jaribu kizungu na simu yako ukitaka ku change imei no.hakuna atayepokea simu yako,nani asiyeogopa Tcra? Nani anayependa kufungwa au kulipa mamilioni kwa ajiri ya kuchange imei no.? Huku Mwanza Tcra wapo Moto,kiasi kwamba ukileta simu yako mafundi wanajua umetumwa na TCRA
.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hilo biti mlilopigwa si mchezo
 
BuletAngle

JF-Expert Member
Apr 15, 2017
690
1,000
Akili ndogo Kudhibiti akili kubwa ni zoezi tosha fikirishi sana , Na hakuna wa kuweza kushirikiana nao kama vijana walio hitimu masomo ya Information Technology (IT) Eti kuna mtu anaweza kutamka kwa mdomo wake kumwambia mwanafunzi aliehitimu masomo ya Information Technology (IT) Eti " IT ni ujanja ujanja tu mwisho wa siku wanakutana kwenye PRACTISE...
Matokeo yake ndiyo haya mnaanza kuwaomba TCRA wajaribu kuona wanazuiya vipi hili Tatizo...

Mimi maoni yangu wakae na vijana wanaofanya izo shuhuli za kubadili Imei Number wajuwe wanafanya je ili waweze kushirikiana na kuziba au kushauriana njia gani itumike kuzuiya huo mziki mnene......
Na vilevile waheshimiwa tunaomba watoe Support kwa vijana wenye ujuzi huo ili waweze kujua na kufanyia kazi katika kipindi hiki cha TECHNOLOGY ENDELEVU...

Ila Tutorial zipo nyingi sana kwa ajili ya kuonyesha jinsi ya kubadili au kuweka imei number kwenye simu Na zikiwa zimewekwa na makampuni husika kwa kuwa waligunduwa kuwa baadhi ya vifaa vyao wenyewe vinatatizo hilo la kupoteza Imei number sana sana kwenye simu zinazotumia Software ya Adroid...kwa Upande wa Apple Internetwork Operating System (IOS) hauwezi kubadili emei number....

NB:- MSITOE AU KUBADILI imei Number kisheria ni kosa ,,,,,,,,,Asanten!
 
sungwa.j

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
473
500
Akili ndogo Kudhibiti akili kubwa ni zoezi tosha fikirishi sana , Na hakuna wa kuweza kushirikiana nao kama vijana walio hitimu masomo ya Information Technology (IT) Eti kuna mtu anaweza kutamka kwa mdomo wake kumwambia mwanafunzi aliehitimu masomo ya Information Technology (IT) Eti " IT ni ujanja ujanja tu mwisho wa siku wanakutana kwenye PRACTISE...
Matokeo yake ndiyo haya mnaanza kuwaomba TCRA wajaribu kuona wanazuiya vipi hili Tatizo...

Mimi maoni yangu wakae na vijana wanaofanya izo shuhuli za kubadili Imei Number wajuwe wanafanya je ili waweze kushirikiana na kuziba au kushauriana njia gani itumike kuzuiya huo mziki mnene......
Na vilevile waheshimiwa tunaomba watoe Support kwa vijana wenye ujuzi huo ili waweze kujua na kufanyia kazi katika kipindi hiki cha TECHNOLOGY ENDELEVU...

Ila Tutorial zipo nyingi sana kwa ajili ya kuonyesha jinsi ya kubadili au koweka imei number kwenye simu Na zikiwa zimewekwa na makampuni husika kwa kuwa waligunduwa kuwa baadhi ya vifaa vyao wenyewe vinatatizo hilo la kupoteza Imei number sana sana kwenye simu zinazotumia Software ya Adroid...kwa Upande Apple Internetwork Operating System (IOS) hauwezi kubadili emei number....

NB:- MSITOE AU KUBADILI imei Number kisheria ni kosa ,,,,,,,,,Asanten!
Asante mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tyupa

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
798
1,000
Kama Mwanza hakuna fundi anaeweza kushiriki kubadili imei namba hiyo haimaanishi kuwa hata sehemu zingine kazi hiyo hafanyi ki. Sehemu nyingi hasa Dar.mafundi wengi wanauwezo wa kubadili imei namba na baadhi ya mafundi wameandika hadi matangazo kuwa wana flashi simu na kubadili imei.Simu nyingi zilizofungwa zisitumike mafundi wamefaulu kuzirudisha kwenye matumizi.Hakika kama alivyochangia mada mdau mmoja huu ni mziki mnene TCRA wanatakiwa wakae pamoja na hao wenye ujuzi wa kubadili imei ili waone wanafanyaje ili waweze kutafuta njia nzuri ya kukomesha hii tabia.Lakini kwa jinsi TCRA walivyo wavivu sidhani hata haya yanayoandikwa humu wanayaona.Halafu wanaamini kwa asilimia mia moja kuwa hakuna mtu anaeweza kubadili imei namba.Kwa mintarafu ya habari hii TCRA wanapaswa kutoa tamko lolote.Jirani yangu ana Samsung tablet lakini tulivyoingiza namba za TCRA kuhakiki kama ni original message toka kwao ilisema simu hiyo Tecno na kama namba hazioani basi muda wowote itafungiwa.Ajabu huu ni mwaka wa tatu inachapa kazi na wala haijafungwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kongobelo

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
380
500
Kwanza kabisa walitangaza kuzima simu zote ambazo ni bandia lakini cha ajabu ni kwamba TCRA hawana uwezo wa kuzima simu bandia.

Mafundi simu wana akili kuliko TCRA kwa sababu wana uwezo wa kubadli IMEI namba ya simu yeyote. Simu mbovu original imei namba yake inawekwa kwenye simu fake na inafanya kazi kama kawaida.

Simu zilizoibwa na wenyewe wakaamua kuzifunga ili alieiba ashindwe kutumia zoezi hilo haliwezekani kwa sababu mafundi simu wanabadili IMEI namba na simu inaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Kwa hiyo wizi wa simu ni kama kawaida tu. Baadhi ya mafundi simu wameandika tangazo kabisa kuwa pamoja na kutengeneza simu pia anabadili IMEI namba. Sasa je TCRA wanajua hili na kama wanajua ina maana wamezidiwa ujanja na mafundi?

Tunawaomba TCRA watujulishe kuwa haya mambo mawili niliyoyataja yako nje ya uwezo wao na hivyo masimu fake yaendelee kuzagaa kuliko ilivyo kuwa mwanzo. Na wezi nao waendelee tu kuiba simu za watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kiuhakika TCRA hawawezi kuzima isipokua wanachofanya ni kupitia sheria zake zinawalazimisha makampuni ya simu kutoruhusu simu fake au zenye imei fake kuweza kufanya mawasiliano.
Tatizo ni utekelezaji kwa mfano kuna ule mtandao wenye rangi ya mawingu hawatekelezi hili. Mteja anaweka laini moja hapati huduma (yuko blacklisted) lakini akiweka ya mtandao mwingine inapiga kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom