Mafundi ni wasumbufu, ila hawa wa cherehani wamezidi!!

Ni mwezi wa tano sasa suti yangu haijakamilika, njoo kesho au wiki ijayo ndio jibu nililokuwa napewa kila nikimuona. Ilibidi niazime suti ya kaka wakati wa sherehe iliyokusudiwa niivae hiyo suti. Leo nimeenda kudai kitambaa changu na pesa yangu, nimepigwa na mshangao baada ya kuambiwa na msaidizi wa fundi kuwa suti ilikamilika muda mrefu, lakini ikauzwa..

....mkuu sina nia mbaya ila suti za kushona tatizo koti na has kwenye mabega,kama ulishawahi kuona mtu aliyebobea kwenye pombe kali tena ile haramu basi ndo mara nyingi inakuwa hivyo..........labda kwa ushauri tuu kuna suti toka china bei rahisi sana pita mitaa ya kkoo ujionee.Unanunua asubuhi na kutinga nayo kwenye sherehe jioni.unachofanya ni kupinda chini tuu,hata pasi haziitaji
 
Ni mwezi wa tano sasa suti yangu haijakamilika, njoo kesho au wiki ijayo ndio jibu nililokuwa napewa kila nikimuona. Ilibidi niazime suti ya kaka wakati wa sherehe iliyokusudiwa niivae hiyo suti. Leo nimeenda kudai kitambaa changu na pesa yangu, nimepigwa na mshangao baada ya kuambiwa na msaidizi wa fundi kuwa suti ilikamilika muda mrefu, lakini ikauzwa..
Katavi, fundi mwaminifu ni kinyozi tu. Wengine wote mapepe!
 
Usimpe fundi kitambaa kama haumjui tabia zake
Mimi nilishawai chukua kitambaa kimeshakatwa toka siku iyo tukikubaliana tarehe kama bado anapiga mwenyewe simu lini itakamilika na inakuwa kweli
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom