Mafriji ya Boss!!!

myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,612
6,153
Wadau salam!

Katika pita pita yangu Jumia, nimeona mafriji ya bei nafuu ambayo sio ya kifamilia nimekuta mengi yake ni brand ya Boss! Hata muonekane wake, hususani yale ya double doors naona ni wa kuvutia!

Swali langu ni kwa watumiaji au wenye uelewa wa haya mafriji! Je, ni mazuri interms of matumizi ya umeme, uwezo wa kutengeneza baridi, kugandisha (upande wa juu) na hata possibility ya kutiririsha maji nje pale inapokuwa hakuna umeme!!

Au kwa kifupi, nini uzuri na mapungufu ya haya mafriji.
 
Japo sijawahi kutumia hayo mafriji lkn wengi watumiaji wa hayo mafriji wanasema ni mazuri sana
NImeona kwenye uzi mmoja kuna mdau amesema ni mazuri kwahiyo nimemuomba anijuze zaidi manake maisha haya sio ya kulipa kitu halafu baada ya mwaka mmoja, kinabaki kuwa mzigo na hata kwa kuutupia hakuna!
 
Ni mafriji mazuri ila bati lake linashika kutu kirahisi sana
I see! Yaani unamanisha hili bati la nje>>>
Boss.png
 
Ok, sio hili lenye rangi ya silver, ukikuta lile rangi nyeupe ndio linapata kutu kirahisi
Nahisi kuna utofauti kwenye material, maana kama ilivyokuwa tofauti ya mabati ya zamani baina ya Galco na mabati mengine, tumeelewana myplusbee sorry sana kwa kutokuelewa unamaanisha Boss zipi. Hayo rangi ya silver yako vizuri.
 
Nahisi kuna utofauti kwenye material, maana kama ilivyokuwa tofauti ya mabati ya zamani baina ya Galco na mabati mengine, tumeelewana myplusbee sorry sana kwa kutokuelewa unamaanisha Boss zipi. Hayo rangi ya silver yako vizuri.
Nothing to say sorry man! Kwanza umenisaidia sana kwa sababu ndo umenikumbusha kwamba kuna yale meupe ambayo nilishayasahau! Hii itanisaidia hata siku nikitaka kununua, naweka wazi kwamba sihitaji yale meupe!
 
Back
Top Bottom