Mafisadi yatatafutwa popote yalipo, kauli ya Rais mmeielewa?

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,741
6,432
Mh Rais wetu mpendwa wa Tanzania jana kaelezea nchi hii ilivyokuwa shamba la bibi na akatolea mfano wa kampuni za simu kukwepa kulipa kodi.

Akatolea mfano nchini Ethiopia mapato yatokanayo na simu ndo yanajenga reli ya SGR wakati sisi TCRA ipo na imelala.

Ameeleza ufisadi kupitia watumishi hewa, ufisadi kupitia jeshi la polisi ambapo askari wanaambiwa wakuchukue uniform kwa mhindi fulani.

Ameeleza ufisadi makao makuu ya polisi ambapo serikali inatuma mabilioni lakini hayafiki kwa Ma RPC na hakuna mkubwa ndani ya polisi ambaye amewajibika kwa dhambi hii?Nadhani hapa anamaanisha LUGUMI etc.

Lakini zaidi ya yote amesisitiza kuwa mafisadi yatatafutwa popote yalipo na hayatekwepa mkono wa sheria. Je mmeelewa aliposema yeyote aliyejihusisha na ufisadi atatafutwa popote alipo??

Haya tujadili kwa kutoa mfano.

Asante
 
ya lugumi bado haijaguswa itaguswa hakuna pa kupitia subirini document zote zipatikane watakamatwa wote na kulipa pesa za umma hakuna kulindana kipindi hiki mlichagua wenyewe na kubeba wenywewe sasa subirini muda ufike
 
Ni Move tu hamna ukweli niambieni tangu mazingaombwe ya majipu yaanze kuna mtu kafungwa?
Binafsi siamini kama nitakuja kuona au kusikia mafisadi wanafungwa au kufirisiwa Mali zao ndani ya utawala wa ccm kamwe haiji kutokea.
 
siyo muvu..subiri mahakama ya mafisaidi na wala rushwa
 
HV bado mnadanganya watanzania? hebu mpk sasa mtuambie fisadi gani keshashughulikiwa? tajeni majina hapa kwa maana hasa ya wale mafisadi wanaojulikana na watanzania,naona chorus tu zinabadilishwa
 
HV bado mnadanganya watanzania? hebu mpk sasa mtuambie fisadi gani keshashughulikiwa? tajeni majina hapa kwa maana hasa ya wale mafisadi wanaojulikana na watanzania,naona chorus tu zinabadilishwa
Thubutu hawawezi yani hao wote wanaoipigia debe ccm ni njaa tu ndo zinawasumbua jaribu kufanya sensa majumbani kwao uone walivyochoka chama chao cha maigizo naona kinaanza taratibu kufifia mana move zinawakati wake hata ukipima wananchi wenyewe wameshanza kuwaona ni wasanii na taratibu wanachama wao wanaanza kung
61cbf60651882b8b15c3e2f51a40cd99.jpg
`atuka.
 
Haya maigizo yataisha ndani ya muda mfupi ujao...Kilo ya sukari sasaivi ni 2800 alafu kuna watu wanatupigia stori zisizo na faida kwetu....

Nafurahi sana kwa sababu this guy ni Mpango wa Mungu kwa ajili ya Kuondoka daima kwa CCM

Kila siku anatafuta kiki na kupiga porojo...analalamika kuliko hata raia wa kawaida......

Ame raise expectation kubwa sana kwa wananchi...kitu ambacho katu hawezi kifikia

Maisha yanazidi kuwa magumu...Hizi ngonjera muda si mrefu zitakuwa irrelevant
 
Sasa wewe Mmwera hilo swali unamuuliza nani? Ulishauliza swali kama hilo kupitia ile ID yako nyingine ambayo huwa unatumia kuchangia mambo ya kipuuzi. Nakushangaa hukuridhika kule swali hilo hilo unauliza kwa ID nyingine. Pole sana. Kuumbuka kubaya sana
Hahahahah mbona Mimi sina ID nyingine?
Umeshikwa pabaya

Shindu na mwaka tu ndiyo id yangu hiyo nyingine itakua copy and paste
 
Hahahahah mbona Mimi sina ID nyingine?
Umeshikwa pabaya

Shindu na mwaka tu ndiyo id yangu hiyo nyingine itakua copy and paste
Usijifanye hujui. Hoja unazoandika kwa ID hii ndizo unaandika kwa ile ID nyingine hasa unapotaka kueleza kuwa mimi ni kibaraka wa kiongozi fulani. YUmejificha weee mwisho umeumbuka mwenyewe. Pole sana
 
Hahahahah umechemka.!
 
Haya maigizo yataisha ndani ya muda mfupi ujao...Kilo ya sukari sasaivi ni 2800 alafu kuna watu wanatupigia stori zisizo na faida kwetu....

Nafurahi sana kwa sababu this guy ni Mpango wa Mungu kwa ajili ya Kuondoka daima kwa CCM

Kila siku anatafuta kiki na kupiga porojo...analalamika kuliko hata raia wa kawaida......

Ame raise expectation kubwa sana kwa wananchi...kitu ambacho katu hawezi kifikia

Maisha yanazidi kuwa magumu...Hizi ngonjera muda si mrefu zitakuwa irrelevant
Baada ya kuigiza kule Mbagala, Juzi nimemuona Lowassa akiigiza kule Dumila.
 
Back
Top Bottom