Mafisadi Wenye Uchu Wa Mamlaka, Hiki ni Chumba Chenu -The Hague | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi Wenye Uchu Wa Mamlaka, Hiki ni Chumba Chenu -The Hague

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by bagamoyo, Oct 17, 2010.

 1. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,522
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Hii ndiyo selo ambayo mafisadi wakibadili matokeo halali ya uchaguzi wa Tanzania hapo 31 Oktoba 2010 watakapokuwa wakisubiri mashitaka ya kusababisha maafa. Mafisadi ni pamoja na wale wote watakaoshiriki kwa namna moja au nyingine kutumia nafasi zao kuvuruga matokeo ya uchaguzi.

  Nafasi zao mafisadi zaweza kuwa za kiutendaji kama vile Maofisa wa NEC, wasimamizi wa vituo vya kura, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa mikoa, Mawaziri, wafanyabiashara, maofisa usalama, Polisi, JWTZ , wataalamu wa IT, vituo vya redio n.k kwa ufupi orodha ni ndefu ya wanaoweza kushiriki kuvuruga matokeo ya uchaguzi kwa njia za kifisadi.

  Mkumbuke kuwa mwaweza kuwa mmejifungia ktk ofisi za ghorofa Upanga au upo ktk ofisi 'nyeti' ya kiserikali ama upo wilaya ya ndanindani mkipanga kuchakachua matokeo, lakini lazima mkono wa sheria wa Ocampo utawafikia. Hivyo ni bora mkakubali mbaki na mahekalu yenu mkiwa huru kuliko kuishia kufunguliwa mashitaka na Ocampo kwa kuchakachua matokeo halali ya uchaguzi.

  Wenzenu huko Kenya (mafisadi) hawalali kwani Ocampo ambaye ni mwendesha mashitaka wa kimataifa, anataka wale wote walioshiriki ktk machafuko baada ya uchaguzi huko Kenya wafikishwe mbele ya chombo hili cha sheria, yaani Mahakama ya The Hague.

  Kwa maelezo zaidi ya mazingira finyu ambayo watuhudumiwa watakuwamo baada ya tamaa yao ya madaraka tembelea hii linki : Daily Nation:*- Politics*|Five-star treatment awaits Kenyan suspects at The Hague
   
Loading...