Mafisadi wataka Kikwete ang’oke; Wadai naye ni gamba, chama kitamfia mikononi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi wataka Kikwete ang’oke; Wadai naye ni gamba, chama kitamfia mikononi

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by nngu007, Apr 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  na Salehe Mohamed  HOFU kubwa imezuka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya hatua ya uongozi wa chama hicho kuwapa muda wa siku 90 wanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

  Sasa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wanataka na mwenyekiti wao aondoke nao kwenye uongozi wa chama.
  Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumapili umebaini kuwa makada wa chama hicho, ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi, na ambao wamepewa siku 90 wajiondoe, wanasema ufisadi wa CCM unamgusa hata mwenyekiti wao.

  Wanadai naye ametuhumiwa mara kadhaa, kama wao, na kwamba amechangia kukipa chama sifa mbaya.
  Wanamshangaa Rais Jakaya Kikwete, kwamba amekuwa kigeugeu, kwani alishaweka wazi kuwa kamwe hawezi kumfukuza, kumuwajibisha kiongozi wa serikali au wa chama bila ya kuthibitika kwa tuhuma zinazomkabili, ili kuepusha serikali kulipa mabilioni ya fedha iwapo mhusika atakwenda mahakamani na kushinda.

  Wanadai kwamba kama ni kuwajibika au chama kujivua gamba, hata Rais Kikwete alipaswa kuwa ni miongoni mwa wale wanaotakiwa kuwajibika, kwa sababu alishatajwa mara kadhaa kuhusika na ufisadi mbalimbali, ukiwemo ule wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

  Na wanadai kutajwa kwake huko ndiko kumeshusha heshima yake kwa umma, na hata kumfanya apite kwa shida katika uchaguzi mkuu uliopita, huku akiwa rais aliye madarakani.

  Wanasema kuwa kama kutajwa mara nyingi katika kashfa za ufisadi ni kukichafua chama na ndicho kigezo kilichotumiwa na CC, NEC, Rais Kikwete hapaswi kupona kwa kuwa alishawahi kutajwa katika orodha ya mafisadi 11 na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alipokuwa akihutubia wananchi katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

  Septemba 15, 2005, Dk. Slaa aliwataja baadhi ya makada wa CCM na watendaji wa serikali akiwamo Rais Kikwete kuwa ni mafisadi wanaochangia umaskini wa taifa kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa manufaa yao.

  Wachambuzi hao wanasema kuwa hicho kilikuwa kipimo tosha kwa wana CCM kuwaadhibu makada wao lakini haikufanya hivyo na badala yake kikajikita katika kukanusha kuhusika na kuhusishwa kwa makada wao hasa Rais Jakaya Kikwete.

  Miongoni mwa watuhumiwa wa ufisadi wameliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa tatizo lilipo ndani ya CCM si wao kama inavyoelezwa na kushabikiwa, kwani kama wangekuwa tatizo wasingeweza kushinda uchaguzi katika majimbo yao kwa asilimia kubwa kuliko hata zile alizopata Rais Jakaya Kikwete kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba 30, mwaka jana.

  Alisema ana uhakika watuhumiwa wa ufisadi wakitoka ndani ya CCM na kuwania ubunge kupitia vyama vya upinzani watarejea bungeni wakiwa mashujaa kama ilivyo kwa wenzao walioshinda ubunge baada ya kufanyiwa zengwe kwenye chama hicho tawala.
  "Sisi si tatizo ndani ya CCM… kuna matatizo lakini NEC, CC hawakuyaangalia hayo, kimsingi naona maamuzi yaliyofanyika yaliwalenga watu zaidi kuliko hoja, tusipokuwa makini chama kitaendelea kupoteza umaarufu," alisema.

  Kada huyo alibainisha kuwa tatizo lililopo hivi sasa ni la kimfumo zaidi na wala si la mtu mmoja mmoja.

  Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaweka bayana kuwa uamuzi wa kujiondoa chamani kwa watuhumiwa wa ufisadi unaweza pia kuyumbisha shughuli za utendaji wa serikali pamoja na kuimarisha upinzani ambao umepata umaarufu zaidi baada ya kuonekana ndiyo unaosimamia masilahi ya wananchi.

  Wanasema kuwa uamuzi wa CCM unaweza kuwa na madhara zaidi kwa kuwa chama hicho hakijapata kuwaadhibu wanachama wengi kwa wakati mmoja kama ilivyo hivi sasa kwa sababu huko nyuma kilikuwa kikitoa adhabu kwa mtu mmoja moja.
  Kwa sababu hiyo, hivi sasa wanachama wamegawanyika juu ya uamuzi huo, huku kundi moja likiona umefanywa kwa fitna, majungu na chuki, hasa kwa lengo la kuwavunja nguvu vigogo wanaodaiwa kuanza mbio za kuwania urais.

  Gazeti hili limedokezwa kuwa uamuzi huo wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) umeanza kukimega chama katika mapande makubwa mawili kuelekea 2015.

  Iwapo moja litajiondoa na kujiunga na upinzani utakuwa mwanzo wa utabiri wa hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere ambaye aliweka bayana kuwa upinzani wa kweli na utakaokiangusha chama tawala utatoka ndani ya chama hicho.

  Nyerere alisema iwapo CCM haitabadilika kwa viongozi kuacha kuendekeza majungu, fitna, kujilimbikizia mali na kuwanyenyekea watu wachache (matajiri) huku ikiwatupa wananchi walio wengi, kingekumbwa na hatari ya kumegeka.

  Lakini yeye alisisitiza pia kwamba mmeguko utakaokisaidia chama hicho ni ule wa kiitikadi. Wachambuzi wa kisiasa wanasema CCM ya sasa inaelekea kumeguka kwa majungu na fitna.

  Baadhi ya makada wenye hofu ya kumeguka kwa chama hicho wanahoji ushahidi uliotumika kuwataka watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi waachie nyadhifa zao ilhali hawajawahi kuhojiwa na taasisi yoyote ya dola na kufikishwa mahakamani kama ilivyo kwa wengine ambao mpaka sasa kesi zao zinaendelea kusikilizwa.

  Tanzania Daima Jumapili, imedokezwa kuwa makada wa CCM wana hofu kuwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi wakiamua kukihama chama hicho na kujiunga na upinzani wana uwezo wa kuondoka na wafuasi wengi wanaowaunga mkono, hivyo kuinyong'onyeza CCM.

  Sababu kubwa inayotolewa na wanaodai hivyo ni kwamba kwa kuwa viongozi wanaoendekeza majungu si waadilifu, lakini wana madaraka, wale wanaodhani wameonewa ni rahisi kupata wafuasi wanaowaonea huruma, hasa wanaoamini kwamba uongozi wa sasa wa CCM hauna uadilifu wala uwezo wa kukivusha kwenye mapambano na upinzani unaokua, hasa CHADEMA.

  Wasiwasi huo unachagizwa zaidi na kuwapo kwa tetesi kuwa watuhumiwa hao, Edward Lowassa (Monduli), Andrew Chenge (Bariadi Mashariki), na Rostam Aziz (Igunga) hawakuridhishwa na uamuzi wa CC, NEC ambao unadaiwa kuamuliwa kifitna zaidi kuliko kuangalia uhalisia wa tuhuma za wahusika.

  Wachambuzi wa masuala ya siasa wameweka wazi kuwa wameshangazwa na uamuzi wa CCM kutaka kuwatosa watuhumiwa wa ufisadi kwa kusikiliza maneno ya watu, huku naye (mwenyekiti) akituhumiwa kwa ufisadi kama wao, bila ya kupata ushahidi wa namna walivyoshiriki kwenye ufisadi unaotajwa.

  Wakati huo huo, Mwenyekiti Mwenza wa Taasisi ya Utafiti na Elimu ya Demokrasia (REDET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, anasema bila ya mabadiliko ya kisela, kifalsafa na kiitikadi, CCM haiwezi kusalimika katika hatari ya kung'oka madarakani.

  Dk. Bana alisema katika mfumo wa vyama vingi ambapo wananchi wanapata fursa kubwa ya kusikia na kuona ushindani wa sera, itikadi, falsafa za vyama mbalimbali ni lazima CCM iviangalie vitu hivyo ili kutimiza matakwa ya wananchi na wanachama wao, kinyume na hapo mabadiliko yoyote yatakayofanyika hayatoweza kukiepusha na hatari ya kung'oka madarakani.

  Na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema matatizo waliyonayo CCM ni sawa na saratani (kansa) iliyopo damuni ambayo kamwe hayawezi kupona, hivyo jitihada zinazofanywa na chama hicho kujinusuru na kifo haziwezi kuzaa matunda.
  Naye Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Mjini Kati, Askofu Thomas Laizer, wakati akiwa katika mazishi ya mama yake, alimtaka Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, atulie kwani walichokifanya wenzake wa CCM ni kutoa boriti kwenye jicho la mwenzao wakati macho yao yana magogo.

  Kauli hiyo inaonyesha wazi kuwa kiongozi huyo wa dini hakubaliani na kilichofanywa na CCM, kwa kuwa wapo viongozi wengi ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakinyooshewa kidole kwa kuhusika na ufisadi lakini NEC na CC hawajawachukulia hatua zozote. Wachambuzi wa mabo wamebainisha kuwa hivi sasa wanatarajia CCM itawaandikia barua kujiondoa kwenye chama hicho makada wengi zaidi, kwa kuwa Dk. Slaa ametaja orodha nyingine ya watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi. Wanabainisha kuwa mabadiliko yaliyofanywa na chama hicho hayawezi kutoa matunda mazuri, kwa kuwa kwa kiasi kikubwa yametokana na hoja ya ufisadi waliyoiteka kutoka kwa wapinzani, hasa baada ya kutangaza orodha ya mafisadi mwaka 2007 katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jamani, mbona hatuelewani vema hapa???

  Watanzania GAMBA letu linalonyima nafasi ngozi za miili yetu kupumua na kung'ara ni CCM. Hivyo, maadam Jakaya Mrisho Kikwete aonekana kulitambua hilo na hata kujichukulia hatua ya kuficha baadhi ya magamba yasijitokezesaana machoni mwetu, Vijana sisi sasa kazi yetu ni kumalizia kabisa kukwangua na kulitupilia mbali kabisa hili gamba nyonyezi liitwalo CCM.

  Maadam janja zao za kutugawa kidini, kikanda na kikabila ndio hivyo tayari tumeshayajua, ni jukumu letu kuungana pamoja ili tuwe na nguvu zaidi kujipangia aina ya maisha ambayo tungependa kuishi sasa na baadaye BILA CCM.

  Ndugu zangu Watanzania, Maisha bila Gamba na ukurutu CCM yawezekana kabisa. Tuchukue hatua zaidi kuhakikisha kunapatikana KATIBA ya Walalahoi bila udalali.
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Asee, gamba nouma asee! Gamba linamutate
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Sasa cinema ndio imekwishaanza kwa Jakaya kumwaga Ugali na inaelekea kundi la Ngoyai nalo limeamua kumwaga Mboga; wanasema Jakaya nae alihusika pamoja na mambo mengine mengi ya ufisadi lakini pia na ule wa mkataba wa IPTL!! Inaelekea wameamua kama alivyoamua Makamba kuwa kama wakiondoka kwenye chama lazima waondoke na KILONGOLA wao kwani hawakubali kutolewa kafara!
   
 5. CHIMPANZEE

  CHIMPANZEE Member

  #5
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Nimekukubali mkuu
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu hapa,maana hata magazeti ya RA yamekuwa makali kwelikweli kushambulia upande wa pili.Ngoja tuone vita hii.
   
Loading...