Mafisadi walitumbukiza fedha Chadema - Mtei | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi walitumbukiza fedha Chadema - Mtei

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Oxlade-Chamberlain, Sep 1, 2009.

 1. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Muasisis wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei, amesema mafisadi wamepenyeza fedha chafu katika chama hicho ili kuvuruga mpango wa kujiimarisha na 'kuchukua' dola.
  Mtei, alisema hatua hiyo inapaswa kutambuliwa na kudhibitiwa na vijana wa Chadema, vinginevyo itakiathiri chama hicho na kusababisha kishindwe kufikia malengo yake.
  Muasisi huyo ambaye pia ni Mwenyekiti Mstaafu wa Chadema, alisema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) jijini Dar es Salaam jana.
  Mtei ambaye hakuwataja mafisadi hao kwa majina, alisema kuna fedha chafu zilizoingizwa na zitakazoingizwa Chadema kupitia kwa wanachama ama vyama vingine vya siasa hususani vya upinzani, ili kufanikisha ushawishi wenye lengo la kukisambaratisha chama hicho.
  “Vijana mjihadhari na mbinu za wale wanaoihujumu nchi ili kujinufaisha, wanatumia fedha chafu ili kuwasambaratisha, watawapaka matope viongozi wenu kwa njia mbalimbali,” alisema na kuongeza kuwa: “Watapenyeza fedha hizo hata kupitia vyama vya upinzani bila hata wenyewe kutambua, ni lazima tutambue kuna vyama vya upinzani vilianzishwa na mafisadi hao ili utawala wao udumu.”
  Mtei, alisema ni jukumu la vijana wa Chadema kuvijua vyama hivyo na kubuni mbinu za kuvikabili.
  Kwa upande mwingine, Mtei alilalamikia kile alichokiita kuwepo baadhi ya vyombo vya habari, vinavyoshindwa kutekeleza wajibu wenye maslahi kwa nchi badala yake vinatumika kulinda na kutetea maslahi ya mafisadi.
  Vilevile, Mtei alisisitiza kuwa kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwepo madarakani kwa takribani miaka 48 bila kufanikisha maisha bora kwa kila Mtanzania, hakuna haja ya kuendelea kujadili uwezo wake, na kwamba njia inayofaa ni kukiondoa madarakani.
  Mtei aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu (BoT) wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Kwanza iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Julius Kambarahe Nyerere, alisema Tanzania ingefanikiwa kufikia ustawi wa jamii na kukuza uchumi wake ikiwa rasilimali za umma kama madini zingetumika ipasavyo.
  Alitoa mfano kuwa mikataba ya madini ingesainiwa kwa sharti la Serikali kumiliki asilimia 51 katika kila mgodi nchini, umasikini unaozungumzwa na kushuhudia kwa miongo kadhaa sasa ungekuwa historia.
  Naye Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, alisema azma ya kuchukua dola kutoka CCM ni jukumu zito linalohitaji nyenzo mbalimbali ikiwemo rasilimali watu hasa vijana wenye nguvu, ubunifu na uwezo.
  Hata hivyo, Dk Slaa, alisema mazingira yaliyopo Chadema yanaufariji umma kutokana na watu wenye taaluma na viwango tofauti vya elimu na vipaji kujitokeza kwa hiari yao kuwania uongozi wa chama hicho.
  “Zamani tulikuwa tunawabembeleza watu, wasomi na vijana walikuwa wanajiunga nasi kwa kificho, wasionekane, waliiogopa CCM na usalama wa taifa, lakini leo watu wanashindana, hakuna woga,” alisema. Alidai hivi sasa Chadema ina maadui wengi wanaoongozwa na CCM, kisha akavishambulia vyombo vya habari (si vyote) kwa kuandika kinyume cha ukweli unaohisiana na chama hicho.
  “ Tumendikwa kwamba chama chetu ni cha kidikteta, hata hivyo sikutegemea gazeti ambalo Septemba 15 mwaka 2007 nilimtaja mmiliki wake kuwa ni fisadi, lingeniandika mimi na Chadema kwa uzuri,” alisema bila kulitaja gazeti hilo ama mmiliki wake.
  Dk Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Kataru, alipuuza taarifa zinazohusu kuchapishwa kwa kitabu kinachomhusu Makamu Mwenyekiti wa zamani wa chama hicho, Marehemu Chacha Zakayo Wangwe, huku kifo hicho kikihusishwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.
  “Chadema haturudi nyuma hata wakiandika vitabu ili kutekeleza mpango wa kutuvuruga...na vijana mnatakiwa kuilinda na kuitetea, isiishie humu ndani, bali jitokezeni hadi kuwania nafasi za uongozi kwenye serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani,” alisema.
  Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto, alisema hivi sasa Taifa limeelekeza fikra zake katika chaguzi zinazofanyika ndani ya chama hicho, hivyo kuwataka vijana hao kufanya maamuzi muhimu yatakayokiimarisha (Chadema).
  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Zitto, wamejitokeza wakiwa pamoja kwa mara ya kwanza, tangu kuanza kwa mchakato wa kuwania Uenyekiti wa chama hicho.
  Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alitangaza kuwania nafasi hiyo, lakini alijitoa baadaye kufuatia ushauri wa wazee wa chama hicho, walioongozwa Mtei.
  Zitto na Mbowe aliyebaki kuwa mgombea pekee katika nafasi hiyo, walikutanishwa hadharani jana mbele ya waandishi wa habari na Dk Wilbroad Slaa na Mtei.
  Mbowe aliyevaa vazi lake maarufu kama `magwanda ya ukamanda', alikaa kushoto kwa Dk Slaa na Mtei, huku Zitto aliyekuwa amevaa suruali ya jeans na shati za bluu na raba zenye rangi nyeupe na nyeusi kulia kwa viongozi hao.
  Akizungumza kwenye mkutano huo, Slaa alisema kujitoa kwa Zitto kuwania nafasi hiyo, kulitokana na ushauri wa kamati ya wazee wa Chadema, kupitia kanuni zinazotambulika kwenye katiba ya chama hicho.
  Slaa, alisema katiba hiyo inatoa haki ya kufikia maamuzi kwa njia ya muafaka, huku kila hatua ya mazungumzo na uamuzi vikiwekwa wazi kwa wanachama wake. Kwa mujibu wa Slaa, uwazi na mwafaka ni miongoni mwa misingi ya demokrasia inayotekelezwa pia na taasisi kama Umoja wa Afrika (AU) na Bunge la Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SADC).
  “ Sasa kama kuna watu wanadai hatua hiyo imekandamiza demokrasia na ni udikteta, wanatuambia nini kuhusu AU (Umoja wa Afrika) na Bunge la SADC (Jumiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika) ambalo mimi ni mmoja wa wabunge wake? ” Alihoji.
  Kwa upande mwingine, alithibitisha kuwapo kwa mgawanyiko uliotokana na Zitto na Mbowe kuwania nafasi hiyo na kusema ni jambo la kawaida katika chaguzi za taasisi yoyote ikiwemo Chadema.
  Alisema kufuatia kujitoa kwa Zitto, chama hicho kimezidi kuimarika na kufifisha matumaini ya watu 'waliotabiri' kwamba kitaporomoka.
  Naye Mtei, alisema wazee wa Chadema wanatambua uwezo na vipaji vya Zitto na kwamba bado ana mchango mkubwa kwa chama hicho na Taifa.
  “ Tunaamini kwamba Zitto ambaye ni mchanga kisiasa bado ana nafasi kwa mwaka 2015 na kuendelea...ataichukua nchi, hivyo tulimuomba aondoe jina akakubali, alionyesha azma yake ya kutaka umoja ndani ya chama,” alisema.
  Kwa upande wake, Zitto alisema kujitoa kwake kuwania nafasi hiyo, kulitokana na mazungumzo ya muda mrefu na wazee wa Chadema.
  “Lengo letu sote ni kuona chama kinakuwa kimoja, kwa vyovyote vile wazee walioanzisha chama walikuwa na maono yao, nisingependa kukaidi maono yao hivyo nikajitoa bila masharti yoyote,” alisema.
  Zitto, alisema kwa kuwa Chadema bado kipo katika mapambano ya kutafuta dola, wanachama wake wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwenye nafasi yoyote na si kugombania vyeo.
  Naye Mbowe aliyekuwa anazungumza kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mzozo huo, alisema ukimya wake ulikusudia kuondoa hatari ya kuwepo kauli ambazo zingechochea mgawanyiko katika chama hicho.
  “Mambo mengi yaliandikwa, ikiwemo mimi kutoelewana na kamanda wangu Zitto, kitu ambacho si cha kweli,” alisema.
  Hata hivyo, Mbowe aliunga mkono hoja ya Zitto kuhusu nafasi za uongozi kutokuwa lengo la mwanachama kujiunga Chadema.
  Alisema nafasi ya uongozi kama Uenyekiti ni jukumu zito lisilokuwa na maslahi yoyote zaidi ya utumishi wa umma katika kufikia malengo waliyojiwekea.
  “ Uenyekiti wa Chadema si ulaji, msije mkaandika viongozi watakaochaguliwa watakuwa wameula, hakuna ulaji huku ni kazi kwa kwenda mbele,” alisema.
  Mbowe alipinga hoja kadhaa zinazoenezwa dhidi yake, ikiwemo ya kukifanya chama hicho kukosa mtandao hasa mikoani.
  Alisema ushiriki wa wanachama katika vikao vya mabaraza ya wazee, wanawake, vijana, Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu kutoka Tanzania Bara na Visiwani ni uthibitisho wa kuenea kwa Chadema nchi nzima.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hongera sana kwa kazi nzuri
   
 3. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Pole mzee Mtei. Sasa upo Nao sebuleni.
   
 4. misasa

  misasa JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2017
  Joined: Feb 5, 2014
  Messages: 5,453
  Likes Received: 2,522
  Trophy Points: 280
  Alichotabiri kimetimia kazi kwake kama muasisi anakisaidiaje chama chake?
   
 5. darcity

  darcity JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2017
  Joined: Jul 20, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 4,823
  Trophy Points: 280
  Watu wanajua kupekuwa. Hili kaburi la 2009 linafukuliwa leo.
   
 6. V

  VIVIANET JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2017
  Joined: Aug 30, 2015
  Messages: 1,806
  Likes Received: 2,207
  Trophy Points: 280  CCM wanatafuta kwa bidii kupata doa chama chochote cha upinzani, ila kwa madoa walionayo mengi wameshindwa, maana yao yanaonekana wazi
   
 7. imhotep

  imhotep JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2017
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 6,001
  Likes Received: 4,428
  Trophy Points: 280
  Chadema inakata roho,maradhi yameizidi.
   
 8. Mathias Raymond Nyakapala

  Mathias Raymond Nyakapala JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2017
  Joined: Mar 1, 2017
  Messages: 1,340
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  Mh
   
 9. S

  Siyabonga101 JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2017
  Joined: Mar 8, 2016
  Messages: 2,437
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Sio sebuleni tena mkuu. Yupo nao master bedroom kwa sasa.
   
 10. S

  Siyabonga101 JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2017
  Joined: Mar 8, 2016
  Messages: 2,437
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Jamii Forum katika ubora wake.
  WALIBERALI pitieni huu Uzi ili mzibue fikra zenu.
   
 11. gp1rooney

  gp1rooney JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2017
  Joined: Jan 16, 2015
  Messages: 1,249
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280
   
 12. S

  Siyabonga101 JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2017
  Joined: Mar 8, 2016
  Messages: 2,437
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Acha tu mkuu....yaani wanamtumbulia macho Mzee Mtei akiwa na boxer na vesti tu. Tehe tehe...siasa hizi!
   
 13. m

  mwingereza2 JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2017
  Joined: Sep 26, 2017
  Messages: 213
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Kwa bini ulete hapa mambo ya 2009 hapa. Unamfuatilia fisadi moja ambapo umewaacha maelfu fisiem. Shame on you.
   
 14. k

  kambale mweusi Member

  #14
  Sep 30, 2017
  Joined: Sep 30, 2017
  Messages: 35
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 15
  Da we acha tu!
   
 15. gp1rooney

  gp1rooney JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2017
  Joined: Jan 16, 2015
  Messages: 1,249
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280
  sjui mzee wa watu anajiskiaje hko alpo
   
 16. m

  mwingereza2 JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2017
  Joined: Sep 26, 2017
  Messages: 213
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Hivyo hamuoni fisiem inavyokata roho bila polisi. Kwaauaji haya unadhani kuna mwananchi anayependa kuitwa c...????
   
 17. Mudawote

  Mudawote JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2017
  Joined: Jul 10, 2013
  Messages: 5,266
  Likes Received: 3,660
  Trophy Points: 280
  Mzee aliona mbali na kweli edo alimwaga 10 bilion na mbowe bila ajizi akasambaratisha na kuua chadema mpaka sasa chadema ilishakufa, hahahaha, CCM oyeee
   
Loading...