Mafisadi wakikamatwa nchi itatikisika. Nani katuloga akili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi wakikamatwa nchi itatikisika. Nani katuloga akili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Welu, May 21, 2012.

 1. W

  Welu JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 815
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Hivi mipora nchi na mijizi ya mali za watanzania mifisi-adi ndo ilishatetewa kwamba ikikamatwa nchi itayumba? Hivi hizi fikra za kulindana tulizipata wapi? Kama Tz iliweza pigana na nchi ya nini leo kumwogopa mtu binafsi? Je mafisi-adi wana jeshi kushinda nchi? Au kauli hii haikuwahi semwa na kiongozi yeyote? Au ni ninyi wenyewe mnaogopa kujishika? Hakika nchi yangu nakupenda kwa moyo wote! Nilalapo nakuota wewe!
   
 2. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  Mchawi mkubwa aletuloga wa tz ni CCM . Hakika siku yako inafika uking'oka ndipo tanzania na watanzania watafaidi na kuneemeka.
   
 3. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kila chenye mwanzo kina mwisho ccm ilikuwa na mwanza pia hata mafisadi wanaowafuga walikuwa na mwanzo pia na mwisho wake unakuja na wataumbua na kuaibika na hili halibishiki ni siku tu inasubirika sasa
   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,792
  Likes Received: 3,879
  Trophy Points: 280
  wewe unataka mafisadi washike nchi mara ngapi ndugu yangu?? sasa hivi si ndio wanaongoza nchi? unasikia kila siku hawalipi kodi? wanauza wanyama hai nje? wanachukua madini yetu? wamejimilikisha maelfu ya hekta za ardhi?wanauza madawa ya kulevya? wamejenga mahekalu nje na ndani ya nchi? watoto, hawara na wake zao wanafanya kazi sehemu nyeti kama BOT TRA? wanarithishana madaraka?watoto wao wanasoma ulaya na marekani? wamejigawia mashirika ya umma kwa kisingizio cha ubinafsishaji?wamegawana nyumba za serikali? wanajichotea pesa toka hazina EPA?? wakishikwa na mafua kidogo tu wameshakimbizwa ulaya au india! huo ndio mfumo wa mafisadi unaoongoza nchi! rais hawezi kuteua yoyote au kufanya lolote bila ku compromise na mafisadi ambao ndio walimuweka madarakani ili awatumikie wao na sio sisi wenye nchi walala hoi! Ole wetu!! kazi ipo tena sii ndogo!!
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Mimi naona bila kuikamata ndio nchi inayumba kama MV Bukoba au Titanic! Wananchi tuchukue wajibu wa kuwakamata kama Arab spring!!!!!!
   
 6. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Hii ni kauli mbaya kuliko zote iliyowahi kutolewa na kiongozi wa wananchi katika dunia hii.
  Adhabu ya kiongozi anayetoa kauli kama hii hadhrani ni kumchapa viboko hadharani ili iwe fundisho kwa wenye mawazo kama yake kwa kizazi hiki na iwe historia kwa vizazi vijavyo.
   
 7. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Jana nimepata taarifa kuwa pale Kilimanjaro Kempsiky. Viongozi wetu wanalipia parking hata mwezi mzima, yaani aje asije hiyo sehemu inalindwa. Mtu wa kawaida ukija unaambiwa parking imejaa ukiuliza pale. Unaambiwa pale pamelipiwa. Sasa nikajiuliza hivi hao viongozi wanatoa wapi pesa za kutumia hovyo hivyo. Huu ndo ufujaji hovyo wa mali za uma
   
Loading...