Mafisadi wajibu

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
3
VITA dhidi ya ufisadi iliyoanza kupamba moto katika miezi ya hivi karibuni sasa inaonekana kubadili mwelekeo na kuanza kuwarudi baadhi ya wanasiasa na wananaharakati waliojitokeza kwa nyakati tofauti kupambana dhidi ya vitendo vya ubadhirifu, wizi na uporaji wa rasilimali za taifa.
Dodoso lililofanywa na Tanzania Daima Jumapili, limethibitisha pasipo shaka kwamba, kundi maalumu la watu ambalo linajumuisha watu wanaotuhumiwa kuwa mafisadi, limeanzisha mapambano makali ya hoja dhidi ya wale wote wanaowanyoshea kidole wao.

Uchunguzi huo aidha unaonyesha kuwa kundi hilo likitumia nguvu ya ushawishi ya vyombo vya habari, limeanzisha operesheni maalumu ya kujibu mapigo, likiwalenga wanasiasa, wanaharakati, wamiliki wa vyombo vya habari na wanahabari ambao kwa namna moja au nyingine walihusika kwa namna moja au nyingine katika kuendesha au kushabikia vita dhidi ya ufisadi.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, operesheni hiyo maalumu ambayo kimsingi ajenda yake ni kuwasafisha baadhi ya mafisadi na kubadili mwelekeo wa upepo kihoja, imewasaidia mafisadi hao kupumua na wakati mwingine wakijikuta katika mazingira magumu.

Katika tukio moja la wiki hii, mfanyabiashara mmoja maarufu na mmiliki wa vyombo vya habari ambaye baadhi ya magazeti yake yalikuwa mstari wa mbele kuendesha vita dhidi ya mafisadi, alilazimika kutumia ‘mbinu za kijasusi’ kuzima mkakati maalumu wa kundi hilo la mafisadi kutumia chombo kimoja cha habari kumchafua.

Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili linazo zinaeleza kuwa, mfanyabiashara huyo alilazimika kunasa mawasiliano ya wanaharakati wa kundi hilo waliokuwa wakijadili mikakati waliyokuwa wamejiwekea ili kufanikisha lengo la kumchafua wakitumia gazeti moja la Kiswahili linalochapishwa kila wiki.

Mara baada ya kunasa mawasiliano hayo, mfanyabiashara huyo aliitisha mkutano maalumu ukiwajumuisha watu waliokuwa wakitajwa kuhusika katika njama hizo za kumchafua huku akitumia sauti alizonasa katika mkanda wa kaseti zilizokuwa zikiainisha hoja na mbinu ambazo zingetumika kumpaka matope.

Chanzo cha kuaminika cha habari hizi, kimelieleza Tanzania Daima Jumapili, mbinu za mfanyabiashara huyo kunasa mawasiliano hayo ndiyo ambazo kwa kiwango kikubwa zilifanikisha kukwama kwa mpango wa kumchafua, ambao ulikuwa utekelezwe kupitia katika chombo hicho cha habari.

Wakati mfanyabiashara huyo akifanikiwa kuzima operesheni hiyo, habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata zinaeleza kwamba, kundi hilo la mafisadi limeanza kukusanya vielelezo kwa ajili ya kuelekeza tuhuma zenye mwelekeo huo huo dhidi ya mwanasiasa mwingine mwenye ushawishi na Mbunge wa Viti Maalumu, Anne Kilango Malecela.

Kada mmoja wa CCM aliyezungumza na gazeti hili wiki hii, alilieleza kuanza kwa kazi ya kufuatilia historia ya kikazi ya mama huyo tangu akifanya kazi katika taasisi moja ya kimataifa miaka kadhaa iliyopita.

“Subirini. Bomu la Anne Kilango linakuja, watu wameshaanza kumpekua. Si unajua namna alivyowashikia bango mafisadi wa Richmond bungeni? Hawa jamaa wameshaanza kujibu,” alisema mwanasiasa huyo aliyepata kuwa mbunge.

Wakati Kilango akiandaliwa kombora hilo, hali inaonekana kuwa tofauti kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta, ambaye yeye tayari ameshaanza ‘kushughulikiwa’.

Sitta ambaye msimamo wake wa kushikia bango suala la Richmond, ambalo hatimaye lilisababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wengine wawili hata kusababisha kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri, anaingia kwa mara ya kwanza katika orodha ndefu ya wanasiasa wanaopakwa matope kwa njia ya mtandao wa intaneti, akihusishwa na ufisadi.

Katika sakata hili la aina yake, Sitta anahusishwa katika kashfa ya ufisadi akidaiwa kuwa amekuwa akitumia vibaya fedha za umma na hususan kasma yake ya uspika kwa ajili ya masuala yake binafsi.

Katika tuhuma hizo zilizoanza kusambazwa katika mtandao wa intaneti katikati ya wiki hii, Spika Sitta anatuhumiwa kumtumia msaidizi wake mmoja kuchota mamilioni ya fedha kwa kisingizio kuwa ni masurufu ya safari za ndani na nje ya nchi.

Tuhuma hizo dhidi ya spika zinaainisha kulipwa kiasi kikubwa kwa ajili ya safari anazofanya ndani na nje ya nchi, huku akidaiwa kujilimbikizia deni kubwa linalotajwa kufikia shilingi milioni 60.

Mbali ya hilo, Sitta anatuhumiwa pia kuyatumia magari mawili ya Bunge kwa ajili ya matumizi yake binafsi na yasiyotambulika kisheria na kikanuni kwa madaraka yake ya uspika.

Aidha, Sitta katika tuhuma hizo alizoeleza kuwa zinatolewa na wahuni, anadaiwa kutumia vibaya fedha za Bunge hata kusababisha kamati moja ya kudumu ya Bunge kugundua mapungufu hayo.

Tuhuma hizo dhidi ya Sitta zinarudi nyuma na kujaribu kuipekua historia ya utendaji kazi wake wakati akiwa Mwenyekiti wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC).

Katika hili la TIC, Sitta anatuhumiwa alitumia wadhifa wake huo kuingia ubia na wafanyabiashara wengi wa kigeni hata kumwezesha kununua hisa katika kampuni moja ya Kichina inayosafirisha magogo ambayo hata hivyo haitajwi kwa jina.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu kuvumishwa kwa taarifa hizo jana, Spika Sitta alikiri kupokea taarifa hizo zinazomuhusisha na ufisadi tangu juzi.

“Ni kweli nimezipata taarifa hizi kupitia kwenye mtandao mmoja hivi, lakini mimi sina cha kusema zaidi ya kusema hizi tuhuma zinalenga kunichafulia jina,” alisema Sitta kwa masikitiko.

Alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kina na kwamba akifanya hivyo itakuwa ni sawa na kujibizana na wahuni, jambo ambalo litamshushia heshima yake.

“Nasema kwamba siwezi kujibizana na wahuni. Naomba mtafuteni mtu wa utawala awaeleze kama suala hili lipo au halipo,” alisema Sitta akionyesha dhahiri kuzikana tuhuma hizo.

Sitta anaingia katika orodha hiyo ya watuhumiwa siku chache tu baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe, naye kujikuta akiandamwa na tuhuma dhidi yake zenye mwelekeo huo huo wa kuchafuliwa.

Katika hali ambayo hakutarajia, Jumatatu ya wiki hii, Mbowe alijikuta akilazimika kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake kutokana na taarifa zilizokuwa zikimhusisha na deni ambalo moja ya kampuni zake inadaiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Taarifa za Kampuni ya Mbowe Hotels Ltd, kukopa NSSF kiasi cha shilingi milioni 15 ziliandikwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la Rai, kabla suala hilo halijadakwa na wanasiasa wawili, Paul Kyara, ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) na Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), mwenye siasa za kitatanishi, Christopher Mtikila.

Akijibu tuhuma hizo dhidi yake, mwanzoni mwa wiki hii, Mbowe alizielezea taarifa hizo kuwa ni mkakati maalumu wa kundi la mafisadi wenye lengo maalumu la kuzima moto wa kisiasa uliowashwa na kambi ya upinzani na hususan CHADEMA dhidi yao.

Mbowe alieleza kushangazwa na hatua ya watu hao ambao hata hivyo hakuwataja, kugeuza deni alilokopa kisheria NPF (sasa NSSF) mwaka 1990 na ambalo tayari amelipa kiasi cha shilingi milioni 75.5 lionekane kuwa ni ufisadi na kuwekwa katika chungu kimoja na tuhuma za wazi za kibadhirifu za Buzwagi, EPA na sasa Richmond.

Wakati Mbowe na Sitta wakikabiliana na tuhuma hizo, mtu mwingine ambaye naye mashambulizi yanaonekana kuelekezwa kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, ambaye tuhuma zake zilifikishwa ndani ya chumba hiki cha habari wiki hii.

Butiku, mmoja wa watu wa mwanzo kuionyoshea kidole CCM kwa kupoteza dira yake huku akiwatuhumu baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho kwa ubadhirifu, yeye mwenyewe anatuhumiwa kutafuna zaidi ya sh milioni 400 zilizochangwa mwaka 2003 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la taasisi hiyo.

Butiku anadaiwa kuwa alipokea sh milioni 100 kutoka kwa Rais msataafu Benjamin Mkapa kama mchango wake katika ujenzi wa jengo na mamilioni mengine ya fedha yaliyochangwa na watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara maarufu kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo.

Lakini inadaiwa kuwa tangu wakati huo mpaka sasa, jengo halijaanza kujengwa hata kwa hatua ya msingi na kwamba taasisi hiyo haina fedha, jambo linaloashiria kuwa ziliishia mfukoni mwake.

Butiku, ambaye alizungumza na gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam, mapema wiki hii kuhusu suala hilo, alisema anazo taarifa za kuhusishwa kwake na ubadhirifu wa fedha hizo, lakini alikanusha kuwa kamwe hajatafuna hata senti tano ya mfuko anaouongoza.

Alifafanua kuwa, taasisi hiyo iliamua kuitisha harambee baada ya kuona umuhimu wa kuwa na jengo lake, lakini fedha zilizopatikana hazikutosha hivyo taasisi ikaanza mchakato wa kuwachangisha Watanzania wote.

“Kweli harambee ilikuwepo, zilipatikana kama sh mil. 400, tulikuwa tukihitaji zaidi ya bilioni 10 kujenga jengo hilo. Takaanza kuomba mchango kutoka kwa Watanzania wote, lakini aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Frederick Sumaye, aliuzuia kwa madai kuwa, taasisi ilikuwa ikichangisha fedha kwa ajili ya kumsadia Dk. Ahmed Salim kwenye kampeni za urais.

“Tukawa hatuna njia, fedha iliyokuwapo tuliitumia kwa ajili ya michoro ya jengo hilo na safari zangu zinazohusu taasisi ikiwemo ya Marekani. Kama kuna mtu anasema mimi nimechota fedha za taasisi huyo ana lengo baya na mimi. Sitakubali jina langu kuchafuliwa,” alisema Butiku.


Source:Tanzania Daima
 

Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 14 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
hawa mafisadi ambao wengi wao ndio wana mtandao akii zao ni ndogo sana na ndio mana mnaona hata huyo rais waliyempa nchi anakwama kila kukicha sababu kazungukwa na watu ambao uwezo wao wa kupembua mambo na kusoma alama za nyakati ni mdogo sana,inasikitisha kuona akili zao ndio mwisho wake hapo yani wamekaa chini na kufikiria ila suati zao zimenaswa na wamekwama kwa mzee mengi,kisa alisema warudishe pesa sasa watuchafue watz wote mana ndio tunaopiga kelele kuhusu hela zetu na km wanafikiri kuwazima hao ndio mwisho wa vita ya ufisadi basi wanajidanganya ktk vita yoyote kuna watu hujitolea kufa kwa ajili ya wengi,sasa hao wanaotaka kuchafuliwa walliamua kujitoa kwa ajili yetu,na mi nasema hatutawaangusha,wakati ule kabla hatuna fulsa ya kutuma comments nilimwambia jamaa 1 ya kua hawa wanamtandao ambao leo wanaonekana watu safi,wakiachiwa huko mbele watakua watu hatari sana,na hyo ilikua km 2yrs ago sasa naona yanaanza kuonekana tuwang'oe hawa wote kuanzia rais wao alieanzisha siasa chafu mpk wao,na hizo kusema ya kua mzee butiku aliambiwa kala hyo hela tungejua tu na huyo sumaye aliesema ya kua hilo hela ni kwa ajili ya kumsaidia salim hana akili hata kidogo alitegemea yeye angepata urais,kikubwa ni kwamba hawa mafisadi si watu wa kucheka nao kabisa na wala kuwaacha kupita majukwaani kusema walionewa km karamagi juzi huko kwao,wakumbuke dr.mwakembe ni daktari wa sheria sasa maswala ya defamation aliyajua tokea akiwa mwaka wa kwanza wa masomo yake ya sheria,sasa leo hii atasemaje vitu ambavyo anajua vitawachafua watu na vitamgharimu yeye wasitufanye watanzania wajinga 2meamka

na mstari wa mbele, calif/usa, - 23.03.08 @ 10:32 | #3317

HAHAHAHAHAHA!Mnataka kumsafisha mbowe kwa style hiyo!!!Mmeanza kwa mbali kumbe malengo yenu kumsafisha boss wenu!!!hahahah!!!

na kk - 23.03.08 @ 10:39 | #3318

Sitta atuhumiwa kwenye mtandao unaom fadhiliwa na chadema na wana chadema

na peter - 23.03.08 @ 10:44 | #3320

WEWE kk wa 3318, mbona hueleweki?? hayo majungu na hayafai kwa mtu kama wewe ambaye na suspect umeelimika, eleza au chambua habari hiyo hapo juu, kwa manufaa ya sisi wengine, wengine wakp nje ya nchi ni vizuri ukaeleweka, unasema Mbowe no bosi wa Tanzania daima??? mimi namjua mbowe kama mtu wa CCM amwekwa mahususi kuua upinzani??

na lwero, japan, - 23.03.08 @ 09:17 | #3328

kweli mafisadi mmejipanga vyema. Sina shaka KK na peter ni wanamtandao au wale madokta hewa wa CCM. Like or dislike it tutawashughulikia. Hata huyo baba yenu wa Ikulu mwisho wake kama atakaa sana 2015. Siyo mbali kama zilivyo ndoto zenu na hapo mtalipa mpaka senti ya mwisho. Kweli mafisadi wa TZ mko kwenye kiwango cha umafia. Unaposema anatetewa mbowe, basi pinga hoja kwamba hakukuwepo mpango wa kumchafua mfanyabiashara na kwamba hakuna mkanda juu ya tukio. Sisi tunaamni pesa inayokopwa kisheria haiwezi kuwa ufisadi. Mnaandaa bomu jingine enyi mafia mliomwagia Kubenea tindikali.

na Quara, Tanzania, - 23.03.08 @ 09:25 | #3330

Watu wanaotaka kuwachafua Sitta, Kilango Malecela na Butiku ni kundi lille lile la Lowassa na Rostam.Ndoto zao za Urais wanaona zimeyayuka sasa wanaona wasife peke yao bali waondoke na wengi.CCM ili ijinusuru watakapokwenda huko Butiama waamue kuwafukuza uanachama wale wote waliokiabisha chama kwa kushiriki katika vitendo vya ufisadi, bila hivyo watapata laana ya mwalimu na hawatajua kitu kitakachowasibu hapo baadae.Jakaya afanye usanii wake mahala popote pengine lakini asijaribu kufanyia usanii kwenye kaburi la "MUSSA".

na bulesi, Tanzania, - 23.03.08 @ 09:35 | #3332

UFISADI UFISADI HAKUNA LOLOTE MNAPIGWA CHANGA LA MACHO TU.WATU WANAENDELEA KUKAMUA.SHIDA YENU MANENO TU HAMHOJI MWISHO WAKE.NANI AMEONJA CHUNGU YA UFISADI?MBONA WOTE WANAENDELEA KUTESA TU...Halafu mhariri haka kaparagraph ka mwisho kana vutia...mwandishi vipi unatuingizia na viungo vya uzazi kwenye habari?

na kibose, BOT, - 23.03.08 @ 10:26 | #3335

Masikini kk, mwaka huu kazi mnayo. Sijui nani atawasikiliza, labda mwende vijijini kama kawaida yenu, maana mkuu wenu aliungwa mkono na 'wajinga' Tunajua mnachofanya, mkuu wenu mwingine si alisema wakipakana matope hakuna atakayebaki?? Si ndicho anafanya sasa kupitia wewe?!!! Lakini its too late, Tutakomaa mpaka tuone mapendekezo ya tume dhidi ya mafisadi yametekelezwa. Kama vipi undeni tume ya kumchunguza mbowe na warioba, maana nyinyi kwa tume hamjambo.

na kukuz, singapore, - 23.03.08 @ 11:01 | #3340

kweli mfa maji haishi kutapatapa ninachojua mimi na watanzania wengine Mh Lowasa wakati wa kampeni umlitumia sana vyombo vya habari kuwanadi wewe na rafiki yako na kuwapaka sana matope wenzenu lakini nasema hivi kila jambo huwa lina mwisho na ngomma ikilia sana hupasuka mimi nilidhani km kweli unabusara baada ya haya yote kutokea ungekaa kimya wewe na mtandao wako ukamwomba mungu akakusamehe kwa yote. sasa tena huo mtandao wenu mnaendeleza mapambano kwenye vyombo vya habari kutaka kufitini wenzenu nasema hivi kwa sababu haya yanayotokea sasa sioni ni wapi mpendwa wetu utakwepea kwa tabia yako yakupenda vyombo vya habari vikunadi kumbuka ndivyo hivyio vilivyokuanika kwa sababu siku zote ukweli hubaki ukweli hataukijitahidi kuutoroka

na MWAINUNU, DSM, - 23.03.08 @ 11:42 | #3347

Jamani huyu ni Rostam azizi na Lowasa, wameamua kuanzisha vyombo vya habari (Magazeti) na kuwanunu waandishi wa habari wenye njaa kwa ajili ya kuwachafua Wazalendo. Hapa mmeshitukiwa kwani mlianza kwa kumchafua Mzee Mengi na Dkt Slaa mkachemsha sasa Mbowe, Butiku na Sitta (pia mmechemsha) hata kwa Anne Malecela, Dkt Mwakyembe mtashindwa tu. Acheni ufisadi.
Kikwete ebu, washughulikie hawa mapema, wanakoelekea ni kukuchafua wewe.

na Mr. Clean, China, - 23.03.08 @ 11:47 | #3349

Lowassa aliwaomya wanaccm wenzie pale bungeni kuwa wakianza kuchafuana hakuna atakayebaki na sasa naona ameanza kuthibitisha usemi wake!! Mheshimiwa Sitta,Anne Malecela Butiku na wengine wenye uchungu na nchi hii msiende mmbali kumtafuta mchawi; watu walioanza mchezo wa kuwachafua wenzao ni hao hao Lowassa na Rostam wakitumia magazeti ya Rostam aliyoyannunua kutumia fedha zetu za EPA.Ni vyema kama ccm itawatosa watu hawa mapema[kwani wanatoboa mtumwi ] ama sivyo watamfikisha Jakaya pabaya na nchi yetu itachafuka; hili msilifanyie mashallah.CCM iwashuhurikie hawa mapema kabla hakujacha.

na siriha, Tanzania, - 23.03.08 @ 12:13 | #3355

....tatizo ni huyu rais wetu,alijua kwamba kazungukwa na mafisi but he failed to drop them earlier!! angewapiga chini mapema tungemuelewa na asingepata dhambi ingawa alitumia pesa zao kwenye kampeni..wakizidi, na sisi tutachukua jukumu, Tanzanias nchi yetu, sio ya ******** wachache!!!

na mike, dsm, - 23.03.08 @ 12:22 | #3356

Ili tuweze kumuamini Kikwete ni bora avunje hiyo kamati inayoongozwa na mwanyika halafu afuate ushauri uliotolewa na kampuni iliyochunguza bank kuu,maana kila kitu kiko wazi sas miezi 6 ya nini? matokeo yake ndo hayo kundi la mafisadi limeshajipanga na limeaanza kuchafua hata wasio husika.Rostam ndiyo kiongozi mkuu wa kundi anawanyonya hata wafanyakazi wake,kampuni yake inafanya kazi mgodini yeye anasema ni kampuni ya ujenzi,Rostam mgodini unajenga nini mbona hata jengo moja au barabara hatujaziona ulizojenga? kama si kuwafisadia wafanyaj=kazi wako?

na Mabwiga, nzega, - 23.03.08 @ 13:19 | #3360

Mafisadi ni mafisadi tu. Hata ipite miaka 20 ao 40 bado watabaki mafisadi. Jina likichafuka hakuna siku litasafika.Kama ni mchafu ni mchafu tu siku zote.
Sasa naona mambo yameiva. Wakati wa ukweli ndiyo umefika. Mafisadi kujificha au kufichwa walizani itawasaidia kumbe imetupa sasa mwanya wa kuyajuwa mambo yote ya kale na ya sasa. Tusikumbatie watu kwa kuwakingia kifua. Akitajwa mtu, asiwepo wa kumtetea. Kama yalifichwa miaka yote hiyo na sasa yamebainika hili ni fundisho kwetu. Kweli HAKUNA SIRI HAPA CHINI YA JUA.
Yasingekua mambo haya ya Ufisadi tungejua wapi kwamba Mil.400. Watu wamechanga kwa kujituma kwa ajili ya kumkumbuka mtu muhimu kwa taifa hili anajitokeza mtu mmoja anakomba hela yote alafu akitajwa kwa ubadhirifu anatetewa...... Aibu. Ebu huyo baba atueleze hivi kweli michoro ya ujenzi wa nyumba na safari zake binafsi zinawezaje kumaliza mil.400 za shilingi. Nae achunguzwe maadamu ametajwa, amekiri kuzitafuna.Shilingi 400,000,000 si mchezo. Kama si ufisadi, tuelezwe badi ni kufikia kiwango gani mtu akitafuna aitwe fisadi?
Ndugu zangu wakati wa ukweli ndio huu acheni hii operesheni ya kutajana iliyokwisha anza iendelee ili mwananchi ajue ukweli.Ikumbukwe kuwa kila kitu kina mwisho wake. Ipo siku tu CCM haitakuwa madarakani. Itakapo pokonywa uongozi wa dola, vigogo wote fisadi watakao kua hai watakiona. Wao wacheze leo na IPTL,SONGAS,RICHMOND, TANGOLD, EPA, BoT, BUZWAGI n.k. ila ipo siku wala haiko mbali. Isitoshe hata ikia ulikuwa CCM na ukakimbilia Upinzani bado utakuwa huna kinga utafuatwa tu.

na Sifurukuti, Singida, - 23.03.08 @ 13:54 | #3362
 
MAFISADI WAANZA KUJITAKASA KWA WENGINE FALSELY KUJIBU BAADHI YA TUHUMA,NSSF UMEJIBU......VOGUE LA WATU JE.....AU UMERUDISHA KIMYA KIMYA.....!
 
MAFISADI WAANZA KUJITAKASA KWA WENGINE FALSELY KUJIBU BAADHI YA TUHUMA,NSSF UMEJIBU......VOGUE LA WATU JE.....AU UMERUDISHA KIMYA KIMYA.....!

too bad kwamba hii habari imetoka katika gazeti la mbowe, na kuna sehemu wanadai deni la mbowe kwanza lilitoka gazeti la rai ( la rostam aziz ) na wamesema hivyo, sasa mbona habari hizi zikitoka tanzania daima mbona hawasemi la mbowe ? jamaa pumbavu, na nimewachoka, sisomi tena gazeti ushuzi lao !

Na magazeti siku hizi naona yameshapoteza mwelekeo mzima kum***na zao, wanaendekeza siasa bali ya kutupa hali halisi, screw them all ! excuse my french !ila wameniuzi !
 
too bad kwamba hii habari imetoka katika gazeti la mbowe, na kuna sehemu wanadai deni la mbowe kwanza lilitoka gazeti la rai ( la rostam aziz ) na wamesema hivyo, sasa mbona habari hizi zikitoka tanzania daima mbona hawasemi la mbowe ? jamaa pumbavu, na nimewachoka, sisomi tena gazeti ushuzi lao !

Na magazeti siku hizi naona yameshapoteza mwelekeo mzima kum***na zao, wanaendekeza siasa bali ya kutupa hali halisi, screw them all ! excuse my french !ila wameniuzi !
KADA HILI LIMEONEKANA....! KUNA KAMPENI ZA KUSAFISHA MAFISADI KUPITIA BAADHI YA MEDIA INCLUDING.....TANZANIA DAIMA&RAI.........NIMEELEWEKA HAPO....?
 
Hachafuki mtu kila mmoja atabeba mzigo wake mwenyewe siku ikifika.
 
Hachafuki mtu kila mmoja atabeba mzigo wake mwenyewe siku ikifika.
MWIBA.....NA ITAKUWA MWIBA KWAO WAKIONA HASAFISHIKI.......UFISADI NI KAMA KIVULI CHAO....KITAWAANDAMA DAIMA WAENDAKO....!
 
Back
Top Bottom