Zee la shamba
Member
- Oct 17, 2007
- 55
- 4
VITA dhidi ya ufisadi iliyoanza kupamba moto katika miezi ya hivi karibuni sasa inaonekana kubadili mwelekeo na kuanza kuwarudi baadhi ya wanasiasa na wananaharakati waliojitokeza kwa nyakati tofauti kupambana dhidi ya vitendo vya ubadhirifu, wizi na uporaji wa rasilimali za taifa.
Dodoso lililofanywa na Tanzania Daima Jumapili, limethibitisha pasipo shaka kwamba, kundi maalumu la watu ambalo linajumuisha watu wanaotuhumiwa kuwa mafisadi, limeanzisha mapambano makali ya hoja dhidi ya wale wote wanaowanyoshea kidole wao.
Uchunguzi huo aidha unaonyesha kuwa kundi hilo likitumia nguvu ya ushawishi ya vyombo vya habari, limeanzisha operesheni maalumu ya kujibu mapigo, likiwalenga wanasiasa, wanaharakati, wamiliki wa vyombo vya habari na wanahabari ambao kwa namna moja au nyingine walihusika kwa namna moja au nyingine katika kuendesha au kushabikia vita dhidi ya ufisadi.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, operesheni hiyo maalumu ambayo kimsingi ajenda yake ni kuwasafisha baadhi ya mafisadi na kubadili mwelekeo wa upepo kihoja, imewasaidia mafisadi hao kupumua na wakati mwingine wakijikuta katika mazingira magumu.
Katika tukio moja la wiki hii, mfanyabiashara mmoja maarufu na mmiliki wa vyombo vya habari ambaye baadhi ya magazeti yake yalikuwa mstari wa mbele kuendesha vita dhidi ya mafisadi, alilazimika kutumia mbinu za kijasusi kuzima mkakati maalumu wa kundi hilo la mafisadi kutumia chombo kimoja cha habari kumchafua.
Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili linazo zinaeleza kuwa, mfanyabiashara huyo alilazimika kunasa mawasiliano ya wanaharakati wa kundi hilo waliokuwa wakijadili mikakati waliyokuwa wamejiwekea ili kufanikisha lengo la kumchafua wakitumia gazeti moja la Kiswahili linalochapishwa kila wiki.
Mara baada ya kunasa mawasiliano hayo, mfanyabiashara huyo aliitisha mkutano maalumu ukiwajumuisha watu waliokuwa wakitajwa kuhusika katika njama hizo za kumchafua huku akitumia sauti alizonasa katika mkanda wa kaseti zilizokuwa zikiainisha hoja na mbinu ambazo zingetumika kumpaka matope.
Chanzo cha kuaminika cha habari hizi, kimelieleza Tanzania Daima Jumapili, mbinu za mfanyabiashara huyo kunasa mawasiliano hayo ndiyo ambazo kwa kiwango kikubwa zilifanikisha kukwama kwa mpango wa kumchafua, ambao ulikuwa utekelezwe kupitia katika chombo hicho cha habari.
Wakati mfanyabiashara huyo akifanikiwa kuzima operesheni hiyo, habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata zinaeleza kwamba, kundi hilo la mafisadi limeanza kukusanya vielelezo kwa ajili ya kuelekeza tuhuma zenye mwelekeo huo huo dhidi ya mwanasiasa mwingine mwenye ushawishi na Mbunge wa Viti Maalumu, Anne Kilango Malecela.
Kada mmoja wa CCM aliyezungumza na gazeti hili wiki hii, alilieleza kuanza kwa kazi ya kufuatilia historia ya kikazi ya mama huyo tangu akifanya kazi katika taasisi moja ya kimataifa miaka kadhaa iliyopita.
Subirini. Bomu la Anne Kilango linakuja, watu wameshaanza kumpekua. Si unajua namna alivyowashikia bango mafisadi wa Richmond bungeni? Hawa jamaa wameshaanza kujibu, alisema mwanasiasa huyo aliyepata kuwa mbunge.
Wakati Kilango akiandaliwa kombora hilo, hali inaonekana kuwa tofauti kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta, ambaye yeye tayari ameshaanza kushughulikiwa.
Sitta ambaye msimamo wake wa kushikia bango suala la Richmond, ambalo hatimaye lilisababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wengine wawili hata kusababisha kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri, anaingia kwa mara ya kwanza katika orodha ndefu ya wanasiasa wanaopakwa matope kwa njia ya mtandao wa intaneti, akihusishwa na ufisadi.
Katika sakata hili la aina yake, Sitta anahusishwa katika kashfa ya ufisadi akidaiwa kuwa amekuwa akitumia vibaya fedha za umma na hususan kasma yake ya uspika kwa ajili ya masuala yake binafsi.
Katika tuhuma hizo zilizoanza kusambazwa katika mtandao wa intaneti katikati ya wiki hii, Spika Sitta anatuhumiwa kumtumia msaidizi wake mmoja kuchota mamilioni ya fedha kwa kisingizio kuwa ni masurufu ya safari za ndani na nje ya nchi.
Tuhuma hizo dhidi ya spika zinaainisha kulipwa kiasi kikubwa kwa ajili ya safari anazofanya ndani na nje ya nchi, huku akidaiwa kujilimbikizia deni kubwa linalotajwa kufikia shilingi milioni 60.
Mbali ya hilo, Sitta anatuhumiwa pia kuyatumia magari mawili ya Bunge kwa ajili ya matumizi yake binafsi na yasiyotambulika kisheria na kikanuni kwa madaraka yake ya uspika.
Aidha, Sitta katika tuhuma hizo alizoeleza kuwa zinatolewa na wahuni, anadaiwa kutumia vibaya fedha za Bunge hata kusababisha kamati moja ya kudumu ya Bunge kugundua mapungufu hayo.
Tuhuma hizo dhidi ya Sitta zinarudi nyuma na kujaribu kuipekua historia ya utendaji kazi wake wakati akiwa Mwenyekiti wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC).
Katika hili la TIC, Sitta anatuhumiwa alitumia wadhifa wake huo kuingia ubia na wafanyabiashara wengi wa kigeni hata kumwezesha kununua hisa katika kampuni moja ya Kichina inayosafirisha magogo ambayo hata hivyo haitajwi kwa jina.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu kuvumishwa kwa taarifa hizo jana, Spika Sitta alikiri kupokea taarifa hizo zinazomuhusisha na ufisadi tangu juzi.
Ni kweli nimezipata taarifa hizi kupitia kwenye mtandao mmoja hivi, lakini mimi sina cha kusema zaidi ya kusema hizi tuhuma zinalenga kunichafulia jina, alisema Sitta kwa masikitiko.
Alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kina na kwamba akifanya hivyo itakuwa ni sawa na kujibizana na wahuni, jambo ambalo litamshushia heshima yake.
Nasema kwamba siwezi kujibizana na wahuni. Naomba mtafuteni mtu wa utawala awaeleze kama suala hili lipo au halipo, alisema Sitta akionyesha dhahiri kuzikana tuhuma hizo.
Sitta anaingia katika orodha hiyo ya watuhumiwa siku chache tu baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe, naye kujikuta akiandamwa na tuhuma dhidi yake zenye mwelekeo huo huo wa kuchafuliwa.
Katika hali ambayo hakutarajia, Jumatatu ya wiki hii, Mbowe alijikuta akilazimika kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake kutokana na taarifa zilizokuwa zikimhusisha na deni ambalo moja ya kampuni zake inadaiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Taarifa za Kampuni ya Mbowe Hotels Ltd, kukopa NSSF kiasi cha shilingi milioni 15 ziliandikwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la Rai, kabla suala hilo halijadakwa na wanasiasa wawili, Paul Kyara, ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) na Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), mwenye siasa za kitatanishi, Christopher Mtikila.
Akijibu tuhuma hizo dhidi yake, mwanzoni mwa wiki hii, Mbowe alizielezea taarifa hizo kuwa ni mkakati maalumu wa kundi la mafisadi wenye lengo maalumu la kuzima moto wa kisiasa uliowashwa na kambi ya upinzani na hususan CHADEMA dhidi yao.
Mbowe alieleza kushangazwa na hatua ya watu hao ambao hata hivyo hakuwataja, kugeuza deni alilokopa kisheria NPF (sasa NSSF) mwaka 1990 na ambalo tayari amelipa kiasi cha shilingi milioni 75.5 lionekane kuwa ni ufisadi na kuwekwa katika chungu kimoja na tuhuma za wazi za kibadhirifu za Buzwagi, EPA na sasa Richmond.
Wakati Mbowe na Sitta wakikabiliana na tuhuma hizo, mtu mwingine ambaye naye mashambulizi yanaonekana kuelekezwa kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, ambaye tuhuma zake zilifikishwa ndani ya chumba hiki cha habari wiki hii.
Butiku, mmoja wa watu wa mwanzo kuionyoshea kidole CCM kwa kupoteza dira yake huku akiwatuhumu baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho kwa ubadhirifu, yeye mwenyewe anatuhumiwa kutafuna zaidi ya sh milioni 400 zilizochangwa mwaka 2003 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la taasisi hiyo.
Butiku anadaiwa kuwa alipokea sh milioni 100 kutoka kwa Rais msataafu Benjamin Mkapa kama mchango wake katika ujenzi wa jengo na mamilioni mengine ya fedha yaliyochangwa na watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara maarufu kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo.
Lakini inadaiwa kuwa tangu wakati huo mpaka sasa, jengo halijaanza kujengwa hata kwa hatua ya msingi na kwamba taasisi hiyo haina fedha, jambo linaloashiria kuwa ziliishia mfukoni mwake.
Butiku, ambaye alizungumza na gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam, mapema wiki hii kuhusu suala hilo, alisema anazo taarifa za kuhusishwa kwake na ubadhirifu wa fedha hizo, lakini alikanusha kuwa kamwe hajatafuna hata senti tano ya mfuko anaouongoza.
Alifafanua kuwa, taasisi hiyo iliamua kuitisha harambee baada ya kuona umuhimu wa kuwa na jengo lake, lakini fedha zilizopatikana hazikutosha hivyo taasisi ikaanza mchakato wa kuwachangisha Watanzania wote.
Kweli harambee ilikuwepo, zilipatikana kama sh mil. 400, tulikuwa tukihitaji zaidi ya bilioni 10 kujenga jengo hilo. Takaanza kuomba mchango kutoka kwa Watanzania wote, lakini aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Frederick Sumaye, aliuzuia kwa madai kuwa, taasisi ilikuwa ikichangisha fedha kwa ajili ya kumsadia Dk. Ahmed Salim kwenye kampeni za urais.
Tukawa hatuna njia, fedha iliyokuwapo tuliitumia kwa ajili ya michoro ya jengo hilo na safari zangu zinazohusu taasisi ikiwemo ya Marekani. Kama kuna mtu anasema mimi nimechota fedha za taasisi huyo ana lengo baya na mimi. Sitakubali jina langu kuchafuliwa, alisema Butiku.
Source:Tanzania Daima