Mafisadi wa Elimu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
KITABU cha ‘Mafisadi wa Elimu’ kimezidi kuwa lulu jijini Mwanza baada ya

nakala zake 25,000 ambazo zilitarajiwa kusambazwa kwa mauzo,

kununuliwa na mmoja wa wabunge na kuchomwa moto.

Habari zilizopatikana jijini Mwanza na kuthibitishwa na mmoja wa

mawakala waliopewa jukumu la kusambaza ili kuuza vitabu hivyo,

zilieleza kuwa mwanasiasa huyo kupitia kwa watu wake wa karibu aliomba

kununua nakala zote hizo za vitabu kwa nyakati tofauti kwa madai ya

kuvisambaza bure kwa watu.

Kitabu hicho ambacho kimeanza kusambazwa katika mikoa mbalimbali kwa

mauzo kimekuwa kikitafutwa na wananchi kwa ajili ya kusoma ili

kutambua kilichoandikwa hivyo kuwa gumzo kwa wananchi.

Imeelezwa kuwa mbunge huyo wa kanda ya ziwa kwa mara ya kwanza

alipata taarifa za kuingia kitabu hicho na kutuma watu kukusanya

nakala hizo katika meza za wauzaji na kwenda kuchoma moto.

“Baada ya nakala za kwanza ambazo zilikuwa kama 5,000 kununuliwa

kwa siku moja na kuisha, wakala aliwasiliana na mwenye kitabu ambaye

aliamua kutuma nakala nyingine kwa ajili ya kuuzwa, lakini pia

aliambiwa zimeisha baada ya siku mbili” alieleza mmoja wa wauza

magazeti wa mkoani Mwanza.

Kutokana na kukosekana kwa kitabu hicho baadhi ya wafanyabiashara kwa

kutumia moja ya nakala ambazo wamebahatika kuwa nazo wameanza kudurufu

kitabu hicho kwa kutoa nakala ambazo wanaziuza mitaani

kwa bei ya Sh3000.

“Mimi binafsi kila ninapokwenda kuuza magazeti watu wamekuwa

wakiniulizia kitabu hicho na wengine wameniomba kikifika tu

niwapelekee wakanunue, sasa nilipowaambia bado hakipatikani ila kuna

nakala walisema niwapelekee na waliweza kununua kwa bei

ile ya kitabu” alieleza muuza magazeti huyo.

Katika kitabu hicho wabunge ambao walidaiwa kuwa na shahada feki ni

Anthony Diallo, Deodarus Kamala pamoja na Raphael Chegeni ambao

walitajwa kuwa na shahada ya uzamili(masters) na uzamivu(PhD) feki.
 
Huyu muheshimiwa kichwani amejaza matope au ubongo!
Nakala 25,000 x 2,000 (chukulia kitab ki1 sh elfu 2) = 50, 000, 000.

Achome moto si chini ya milion 50?! Huyu si fisadi tu wa elimu, bali pia ni fisadi wa EPA. He can't even think!
Shame on him.
 
Huyu muheshimiwa kichwani amejaza matope au ubongo!
Nakala 25,000 x 2,000 (chukulia kitab ki1 sh elfu 2) = 50, 000, 000.

Achome moto si chini ya milion 50?! Huyu si fisadi tu wa elimu, bali pia ni fisadi wa EPA. He can't even think!
Shame on him.
hv hakuna uwezekano wa kukiweka hicho kitabu mtandaoni?na tuliombali tunataka kukiona nn kilichomo ndani!
 
Ni kweli kabisa watuwekee kwa net tuone kama watakuwa na ubavu wa kukidestroy tena, ukweli unauma!!
 
ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu kwani ujumbe lazima utafika kwa jamii jamaa wamezoea kuwa vihiyo na sasa tumechoka hizo fedha si bora angepeka kilosa kwani zingesaidia ujenzi kwa waathirika wa mafuriko, nahisi kichwa chake kitakuwa kimejaa tope
 
jamani me naomba hayo majina yangewekwa katika mtandao kwani hakuna atakayeweza kufuta na itakuwa vizuri kwani wengine hawatapa hivyo vitabu coz wababe wameanza visa vyao
 
Kitabu kipo mtaani kinazwa kwa sh 3,000/= tu. Mnataka kiwekwe kwenye mtandao ili mwandishi wa kitabu hiki hakose mapato? mimi ninacho na sijataka kukiweka kwenye mtandao ili kumuunga mkono huyu mzalendo wa kweli aliye na uchungu na nchi yake.
 
Kitabu kipo mtaani kinazwa kwa sh 3,000/= tu. Mnataka kiwekwe kwenye mtandao ili mwandishi wa kitabu hiki hakose mapato? mimi ninacho na sijataka kukiweka kwenye mtandao ili kumuunga mkono huyu mzalendo wa kweli aliye na uchungu na nchi yake.
ila sasa kama kitabu ni threat kwa hao wabunge waliotajwa,sio hatari kwa maisha ya muandishi wetu huyu?!maana wababe wetu hawa tunawajua!hasa kipindi hiki cha kampeni!
 
Nasikia Dkt Mwakyembe alifeli Form IV, akatumia cheti cha mdogo wake kuendelea na masomo!
 
Maktaba imetema
Mzee wetu wa mwanza naye anahojiwa elimu yake,mzee anayemiliki kampuni ya jangwa la sahara na nyota television,sasa naona mahojiano ya jumatatu yatanoga,maana aliyealikwa naye ni wale wale
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom