Mafisadi wa BOT na RDC ni Wahujumu Uchumi?

Kubwajinga

JF-Expert Member
Jan 23, 2008
2,194
297
Wana JF,
Ikiwa huyu mkurugenzi aliyechota Sh4 bilioni za NBC ameweza kushitakiwa kwa kosa kubwa la kuhujumu uchumi, hivi haitawezekana kwa wale walioiba za BOT na hata wale wa Richmond wakakamatwa na kushitakiwa kwa makosa kama hayo hayo ya kuhujumu uchumi? Kwa anayefahamu hukumu ya mhujumu uchumi ningeomba atupe maelezo kidogo, shukran.
Mkurugenzi wa kampuni kortini kwa kuchota mabilioni benki
Na Pauline Richard


MKURUGENZI wa Kampuni ya Ujenzi ya jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka ya kuiibia Benki ya Biashara (NBC) Tawi la Corporate la jijini Dar es Salaam, zaidi ya Sh4 bilioni.


Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Naima Msangi alimtaja mshtakiwa huyo mbele ya Hakimu Samwel Maweda kuwa ni mkazi wa Mikocheni 'B', David Mapunda (57).


Msangi alidai kuwa, mshtakiwa huyo mbali ya kujipatia kiasi hicho cha fedha kwa njia ya udanganyifu, anakabiliwa na mashtaka mengine mawili ya kuongoza kufanya njama, kuhujumu uchumi na kuiibia benki hiyo.


Alidai kuwa kati ya Februari 4 na 22 mwaka huu, mshtakiwa huyo, akiwa mkurugenzi na mmiliki wa akaunti namba 011103000537 kwa makusudi kusababisha upotevu kwa fedha hizo mali ya benki hiyo.


Awali ilidaiwa katika mahakama hiyo kuwa, Januari 25 na Februari 22, mwaka huu, katika benki hiyo, mshtakiwa huyo aliiba kiasi hicho cha fedha baada ya kuweka hundi hiyo, kwenye akaunti ambayo haikuwa na fedha.


Mshtakiwa huyo, hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi kama hiyo ya uhujumu uchumi, hadi atakapofikishwa Mahakama Kuu.


Kabla ya mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo, wakili anayemtetea mshtakiwa huyo, Peter Swai aliiambia mahakama kuwa, mteja wake ana matatizo ya shinikizo la damu na kuiomba kumruhusu kupelekwa mahabusu na dawa.


Ombi la wakili huyo, lilikubaliwa na upande wa mashtaka na mahakama kuahirisha kesi hiyo, hadi Machi 10, mwaka huu, kesi hiyo, itakapotajwa tena. Mshtakiwa huyo alipelekwa rumande.


Matukio ya wizi katika mabenki nchini, yamekuwa yakitokea mara kwa mara na hivyo kusababisha hasara kubwa katika benki hizo.


Oktoba 23, mwaka jana , wafanyakazi watatu wa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe, nao walifikishwa katika mahakama hiyo, kujibu mashtaka ya wizi wa Sh922milioni mali ya benki hiyo.
 
..... na ukiona hivyo ujue kuna LijiFisadi hapo limetoswa kwenye hiyo dili ndo maana, maana pesa hizo hazitokei hivi hivi

Nakubaliana na wewe mkuu kuwa, kuna fisadi aliyenyimwa kitu kidogo.


Lakini sasa wale wa BOT, hasa hawa wanaojulikana wakirudisha hizo pesa, kwa nini wasidakwe wakapigwa nao mhuri wa UHUJUMU UCHUMI??
 
Back
Top Bottom