Mafisadi;Tutawapa muda mpaka lini?

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,949
4,431
Source Majira 17 May 2008
Tahariri
HABARI kuu katika gazeti la leo ni muendelezo wa kufichuka kwa siri za ndani zaidi katika ufisadi uliofanywa kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu na ambao uchunguzi wake umechukua muda mrefu sasa.

Kwa sadfa tu, wakati wachunguzi wetu wakikamilisha kupata taarifa za habari hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu alikaririwa na vyombo vya habari akieleza katikati mwa wiki hii kuwa Serikali kwa sasa haimtafuti Balali, ikimhitaji itamtafuta na kumpata.

Hatupingani na kauli hiyo kwa sababu Bw. Reyemamu yeye ni mtoa taarifa tu. Hoja yetu ipo kwa Serikali juu ya masuala mbalimbali kwa ujumla yanayogusa matatizo makubwa ya kitaifa hasa ufisadi.

Hii si mara ya kwanza sisi kusisitiza kuwa ipo haja ya kumaliza kero zinazojitokeza ili Serikali ipate wasaa wa kushughulikia masuala mengine ya wananchi. Tukirejea namna masuala kama ya EPA na Richmond yanavyochukua muda sasa.

Hali hiyo sote tumeiona imeisumbua sana Serikali:wahisani walijifikiria mara mbili kutuchangia tena kwenye bajeti, heshima ya hata viongozi wakuu mbele ya jamii imeshuka na nchi imekuwa ya hisia nyingi na tetesi.

Hoja yetu awali na inayobaki hadi sasa ni kwamba kuna haja ya kuyamaliza matatizo hasa ya ufisadi kwa wahusika kufikishwa kwenye vyombo husika vya dola ili sisi wanahabari na hata wanajamii wasiachwe kubaki kutawaliwa na hisia kisha wakalaumiwa kuwa wanajifanya wapelelezi, waendesha mashtaka na mahakimu.

Suala la Balali kwa mfano, nyaraka nzito ambazo sisi tunazo na tunazoamini kuwa Serikali inazo kwa kina zaidi, zinaonesha kuwa kiongozi huyo wa zamani wa Benki Kuu alihusika moja kwa moja kubariki ufisadi kwenye akaunti ya EPA.Leo bado ameachwa tu.

Tuliwahi kusema huko nyuma kwamba ukiangalia makosa waliyoyafanya watuhumiwa wengi wa ufisadi kwa wataalamu wa sayansi za makosa ya jinai hasa kwa kuzingatia ripoti kwa mfano za ukaguzi zilizokwishafaywa na kampuni za kitaalamu, haihitaji hata wiki mbili kuwafikisha kortini wahusika.

Lakini kimya na kiza kinene kimetanda, kiasi kwamba mtazamo wa wananchi wengi mitaani na ambao sasa unazidi kupata nguvu kutokana na kigugumizi cha Serikali ni kuwa kumbe wenye nazo wako juu ya sheria.

Wanasema hivyo kwa hisia kali za uchungu, wanataka kuona nchi ikisafishwa kwa mafisadi nao kuburutwa kortini kwa kutumia sheria zetu zile zile zilizowafanya wezi wa kuku, makahaba na wazururaji wajazane magerezani.

Matokeo ya ukimya na kuahirisha matatizo tunakoendekezwa sasa, ndio kunawapa mwanya watuhumiwa wengi kuanza kuja na mikakati, mara vitisho vya kuanika siri nzito za Serikali iwapo wataburutwa kortini na pia wengi wao wakiwa na mbinu zinazofanana kwa kutumia utetezi ule ule wa jumla; wanapakwa matope na wabaya wao.

Taifa kwa mtazamo wetu haliwezi kuendelea kuwa la tetesi hivi, tuhuma zinaibuliwa, uchunguzi unafanyika, inaonekana dhahiri kuna makosa, hatua zinakawia, mitaani zinajaa mijadala juu ya watu,si maendeleo, watuhumiwa nao wanaibua tetesi zenye maslahi kwao, nchi inakuwa ya tetesi, mijadala na hisia nyingi. Tanzania yenye neema haiwezi kufikiwa kwa staili hii. Tujikosoe. Tubadilike.
 
... mpaka pale chama kinachotawala kitakapoondolewa madarakani!

Sioni sababu ya Salva kusema "tutakapomuhitaji tutampata", hivi kuna kipindi ambacho taifa linamhitaji Balali zaidi ya hiki! Zaidi ya kashfa ya EPA, Zakia Meghji alisema wazi alidanganywa na Balali (kuhusu malipo ya Kagoda)! Je pamoja ya haya yote bado taifa alimhitaji huyu mtu kwa sasa! Hivi ni lini tena tutasema tunamhitaji Balali????

Katika hili nadhani Tanzania kuna wenye madaraka zaidi ya rais wa jamhuri!!!
 
Fide,
please use link, hii itatusaidia sisi tuliowazembe, kusoma na kuelewa kwa haraka mzee, samahani kwa hilo, na kwa mantiki hiyo ujumbe ubebwe na haya fupifupi, use jonourism stlye to send ua msg to us.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom