Mafisadi TFF...waroho wa SAFARI!

Engineer Mohamed

JF-Expert Member
Jul 27, 2007
451
9
duh hawa jamaa sio utani,yaani kila safari timu ya taifa kiongozi anatoka TFF,ukiachilia ile ya burkina faso.
uonhoziw a juu wote unaenda australia hakuna hata kiongozi kutoka ZFA.
mafisadi kweli hawa.

TFF yajibu mapigo ya ZFA

2008-05-28 08:49:50
By Somoe Ng?itu


Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limesema kuwa linashangazwa na barua waliyoandikiwa na Chama cha soka cha Zanzibar (ZFA) ya kuvunja ushirikiano nao kwa madai kuwa inakiuka makubaliano waliyoyafikia jambo ambalo si sahihi na halina ukweli.

Akizungumza na Nipashe jana kwa njia ya simu kutoka Sydney, Australia, Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa waraka huo ambao ZFA umewaandikia ni wa kuipotosha jamii na wao wakati wote wamekuwa wakifanya kazi za shirikisho kwa kufuata kanuni na si siasa.

Mwakalebela alisema kuwa katika malalamiko ambayo ZFA imeyatoa dhidi ya TFF kuwa inawatenga yote utekelezaji wake uko wazi kwa kuanzia Dola za Marekani 250,000 zinazotolewa na Shirikisho la soka la kimataifa (FIFA) ambazo zinaelekea kutumiwa katika maandalizi ya timu ya taifa, Taifa Stars, timu ya wanawake, Twiga Stars, semina za makocha, waamuzi ambazo washiriki kutoka pande zote mbili za nchi hupata nafasi ya kushiriki.

Mwakalebela alisema pia wanashangazwa na kauli ya ZFA kuwa uwiano wa wachezaji walioko katika timu ya taifa haulingani huku wakifahamu wazi kuwa uteuzi wa kikosi hicho hufanywa kiufundi na kocha mkuu, Marcio Maximo kwa kufuata vigezo muhimu.

``Tunawashangaa sana wenzetu wa ZFA kwa malalamiko walioyatoa ambayo si ya kweli na wanataka kufanya mambo yaendeshwe kisiasa na kuacha kiutendaji kama ambavyo inatakiwa,`` alisema Mwakalebela.

Aliongeza pia chama hicho kinalalamika kuwa TFF inawanyima kuwapa sehemu ya mgawo wa fedha zinazotoka katika Shirikisho la soka la Afrika (CAF) ambazo ni Dola za Marekani 100,000 ambapo wao Zanzibar ni wanachama na walitakiwa kuandika maombi katika shirikisho hilo ambayo yanaendelezea mipango wanayotaka kuifanya na hivyo kupatiwa baada ya kukubali.

``Sisi na nchi nyingine 12 za Afrika tulipeleka mapendekezo CAF na kupatiwa fedha hizo na wao Zanzibar ambao ni wanachama wa CAF walipaswa kuandika pia lakini wao wanataka wapewe sehemu ya fedha hizo ambazo kila mwanachama aliambiwa aandike maombi yake,`` aliongeza.

Alisema pia Zanzibar wanadai kuwa wanabaguliwa katika misafara ya nje ya timu ya taifa jambo ambalo si sahihi kwa sababu wakati Stars inakwenda Burkina Faso mwaka jana kucheza na wenyeji wao iliongozwa na Naibu Waziri wa Habari na Michezo wa visiwa hivyo, Mahmoud Thabit Kombo na ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Alisema kuwa TFF imesikitishwa sana na taarifa hizo na kusema kuwa hazichangii kuleta maendeleo huku pia akiongeza kuwa Ligi ya Muungano ambayo ilikuwa inashirikisha timu za Bara na Visiwani inashindwa kufanyika kutokana na ratiba ya ligi za pande hizi mbili inatofautiana na pia zamani ilichezwa ili kupata wawakilishi wa nchi katika mashindano ya kimataifa.

Wakati huo huo, Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kimelalamikia hatua ya kutengwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF), ambapo kwa makusudi wameamua kwenda kwenye Mkutuno Mkuu wa Shirikisho la Dunia (FIFA) juzi bila ya kuwa na mwakilishi yeyote wa ZFA.

Viongozi waliokwenda kwenye mkutano huo nchini Australia ni Rais wa TFF, Leodger Tenga, ambaye ndio kiongozi wa msafara huo, Makamu wake wa kwanza , Crescentius Magori na Katibu Mkuu wake Frederick Mwakalebela.

Mkutano huo ambao unashirikisho viongozi wa Mashirikisha na vyama vya Soka Duniani ulianza juzi, ambapo unatarajiwa kumalizika Ijumaa.

Akizungumza kwa njia ya simu na Nipashe mmoja wa viongozi wa ZFA, ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake kwa madai kuwa si msemaji wa ZFA, alisema kitendo kilichofanywa na viongozi wa TFF ni uroho wa safari.

 
Tatizo Lisiwe Siasa Inachanganywa Na Michezo....hapaa Haya.........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom