Mafisadi: Semeni sasa potelea mbali – anzeni kutajana waziwazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi: Semeni sasa potelea mbali – anzeni kutajana waziwazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Apr 24, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Jamani eeeeh!

  Kama tunavyoshuhudia suala la ufisadi ndani ya CCM na serikali yake linashika moto kwa kasi sana huku vigogo wao kadha wa chama hicho wanajitokeza na kuzidi kulimwagia mafuta.

  Kwa maana nyingine huenda imewadia wakati wa kuonyeshana vidole wenyewe kwa wenyewe. Jee kwa mwenendo huu, si dhahiri kwamba sasa hivi ni bora hicho kifanyike?

  Maana sasa hivi imekuwa kurushiana ngumi kijuu juu – yule dogo Nape anarusha makonde kwa adui zake ambao hataki, hana ubavu wa kuwataja kwa majina. Ni unafiki tu kama alivyosema kada mmoja wa CCM Amb Peter Ndobho.

  Mimi naona ni bora sasa mafisadi wakatajana majina bila kujificha, pengine hii ndiyo njia itakayomaliza mambo yote.

  Kwa mfano imefikia wakati wale wanaoonyeshewa kidole katika ufisadi wa Kagoda nao wataje wahusika wengine – maana Kagoda haikuwa hao tu wanaonyeshewa kidole. Kwa mfano RA ataje wahusika wengine.

  Vivyo hivyo kwa rada. Chenge hakuwa peke yake. Asiogope kuwataja akina Mkapa, JK, Dr Rashid na wengine bila shaka. Tukija Richmond nayo hivyo hivyo.

  Tumeshuhudia kwa mbali jinsi Jeetu Patel alivyojaribu kupeleka ujumbe kwa wananchi kupitia kwa wakili wake Mabere Marando kwamba hakuwa peke yake katika dili ile ya EPA ambayo anashangaa kwa nini arudishe fedha alizochota EPA huku kiasi kikubwa kilichukuliwa na CCM.

  Kama tunavyofahamu Jeetu ana kesi kwa sababu hakurudisha fedha za EPA na hivyo sasa anaona na lolote na liwe. Sidhani iwapo wengi wetu walimuelewa Marando wakati wa ufunguzi wa kampeni pale jangwani mwishoni wa Agosti mwaka jana.

  Sasa basi kabla ya kufika huko, nadhani ni wakati muafaka sasa mafisadi wakaanza kusema ukweli kuhusu walivyofisidi, washirika wao walikuwa akina nani etc etc.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kama hawawezi kutajana -- basi CCM iunde tume ya ukweli na maridhiano -- Truth and Reconciliation Commission --TRC-- ambayo kazi yake itakuwa kumaliza suala hili. Mafisadi wote waende kukiri mbele ya tume, wakubali walifisidsi nchi kwa kukitaja kile walichofisidi na waambiwe warudishe angalau sehemu ya kile walichofisidi ili wasamehewe kwenda mahakamani na lupango.

  Hii itakuwa ni tofauti na msamaha aliotoa JK mwaka 2008 kuhusu wezi wa EPA kwani katika msamaha huo hatukuambiwa ni akina nani hao na ngapi walizodaiwa kurudisha.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nakubalina nawe mkuu Zak. hakika imefika potelea mbali -- mambo yote yawekwe uwazi tuone nani atamshitaki nani. Ni unafiki tu kuwachukuwa wachache kuwafanya scapegoats kwa madhambi ambayo wengine pia walihusika. Hata kwa Mungu hii ni dhambi kubwa.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Penye red:

  Hili suala la Marando na Jeetu wengi hawakuwa wamelielewa. Inakuwaje Marando ambae yuko katika kambi ya upinzani kumtetea fisadi?
  Lakini pia kuna hili la Marando kuwa wakili wa fisadi mwingine -- Manji katika kesi yake aliyomfungulia Mengi kwamba alimdhalilisha kumtaja yeye ni mmojawapo wa mafisadi papa. Nadhani pia kuna kitu hapo.

  Tusisahau Manji alidaiwa kukubali ndiye mwenye kampuni ya Kagoda na kukubali kulipa mchoto ule wa Sh 40bn/--- akatoa baadhi ya cheki kwa aliyekuwa AG Johnson Mwanyika ambazo zilimchachia! Sasa kama Mzee Mengi alitoa mahakamani ushahidi huo wa ufisadi wa Manji (ambao uliktataliwa na mahakama ya Kisutu hadi hakimu kujiuzulu) -- basi Marando atakuwa amefanya kitu pale, katika kutafuta ukweli kuhusu Kagoda -- yaani nani hasa mmiliki wa Kagoda.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kwenye rangi: yaani unataka kusema naye manji anataka kutoa yaliyo moyoni mwake kuhusu Kagoda kupitia Marando? Kwa Jeetu inakaa vizuri, lakini si kwa huyu manji!
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nimekusoma mkuu hii ndio sawasawa, kwa sababu ni unafiki. Watajane tu.:A S shade:
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Watajane tu, halafu ije truth and reconsiliation.:israel:
   
Loading...