Shukurani
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 251
- 11
WATATAJANA TU MSIMU HUU
Mafisadi, sasa waanza kuumbuana
SOURCE: ALASIRI
2008-01-31 15:37:37
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Kama Waswahili wasemavyo kwamba Waarabu wa Pemba hujuana kwa viremba, basi ndivyo inavyotokea hivi sasa kwa wale watafunaji wa pesa za umma, almaarufu kama mafisadi.
Kutokana na kutambuana, imeelezwa kwamba baadhi wameanza kuumbuana wao kwa wao huku wakitishiana kuanikana hadharani.
Taarifa kutoka kwa chanzo chetu katika wizara ya Madini na Nishati zinadai vigogo kadhaa ambao awali walikuwa wakishirikiana, hivi sasa ni maji na mafuta na chanzo cha uhasama huo ni mmoja kudaiwa kumchomea utambi mwenzake.
Imedaiwa kuwa kigogo mmoja alilikisha taarifa za mwenzake kwa mapaparazi ambao bado hawajachapisha kutokanana kuendelea kuzifanyia kazi, kitu kilichomkasirisha aliyetuhumiwa.
``Huyo aliyetuhumiwa inasemekana baada ya kubaini hilo, naye alianza kuwasaka waandishi ili awape data kumhusu mwenzake,`` kikaongeza chanzo hicho.
Imedaiwa kuwa pia baadhi ya watendaji wamekuwa wakituma taarifa kibao kwenye mitandao zinazowatuhumu wenzao kwamba ni mafisadi, ingawa hawaweki majina yao wala kutaja ni wapi waliko na wana ushahidi gani wa kile wanachokisema.
Kadhalika katika Wizara ya Fedha inadaiwa baadhi ya watendaji ambao kwa njia moja ama nyingine ndio wanawachomea utambi wenzao kutokana na kufahamu dili zao.
``Hakuna anayetaka kufa peke yake. Kutokana na kutoaminiana, unakuta kila mmoja anamchimba mwenzake,`` kimedai chanzo hicho.
Imedaiwa kuwa hivi sasa katika wizara kadhaa hakuna anayemwamini mwenzake kutokana na kutofahamu nani atakuchomea utambi.
Sakata la ufisadi lilipamba moto baada aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu kutimuliwa kazi kufuatia kubainika kwa ulaji mkubwa wa pesa za umma.
Soo la kuwepo kwa ufisadi nchini liliibuliwa mwaka jana na Mbunge wa Karatu Dk. Wilbrod Slaa .
SOURCE: Alasiri