Mafisadi sasa kumekucha

mshumbusi

JF-Expert Member
Oct 24, 2011
457
231
AHADI ya Rais John Magufuli kuanza kushughulika na viongozi wa umma wanaofanya ufisadi, sasa inapelekwa mkukumkuku, anaandika Faki Sosi.

Ikiwa tayari Bunge la Jamhuri limepitisha Sheria ya Uanzishwaji wa Mahakama nchini, Jukwaa la Haki na Jinai ambalo hujumuisha vyombo vya dola linakutana mjini Dodoma kuanza mchakato huo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria ambapo amesema kuwa, lengo la kikao hicho ni kufanya maandalizi ili khakikisha mahakama hiyo inafanya kazi zake kwa ufanisi.

Kikao hicho kinahitimishwa leo ambapo amesema, washiriki wake ni wale alio katika taasisi za haki jinai.

Taasisi zilizotajwa ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi.

Na kwamba, Takukuru wanapaswa kufanya uchunguzi kwa haraka, polisi watatakiwa kupeleleza haraka na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) atatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi.

Hatua ya kuelekea uanzishwaji wa mahakama hiyo ni ahadi ya Rais Magufuli kuahidi uanzishwaji wake wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Hivi karibuni, Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu alilieleza Bunge kuwa, tayari serikali ilianzisha Divisheni ya Mahakama ya Rushwa na Ufisadi katika Mahakama Kuu.

“Kuhusu ahadi ya kuanzisha Mahakama Maalum ya Ufisadi napenda kuliarifu Bunge lako kwamba, Serikali imeanzisha Divisheni ya Mahakama ya Rushwa na Ufisadi katika Mahakama Kuu itakayoanza kufanya kazi mwezi Julai 2016,” amesema Majaliwa.

Aliahidi kuwa, serikali itaimarisha Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kwa pamoja ziweze kuharakisha utoaji wa haki kwa kesi zitakazofikishwa kwenye mahakama hiyo.

Kiongozi huyo wa serikali aliongeza: “Serikali itaimarisha ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kwa pamoja ziweze kuharakisha utoaji wa haki.”

Katika siku ya kilele cha Wiki ya Mwaka Mpya wa Mahakama Jijini Dar es Salaam mapema mwaka huu, Rais Magufuli alimtaka Jaji Mkuu, Othman Chande kutosubiri Bunge kupitisha Sheria ya Uanzishwaji wa Mahakama ya Mafasidi, badala yake mahakama hiyo ianze kufanya kazi haraka iwezekanavyo.

Amesema, kuchelewesha kuanza kwa mahakama hiyo kunatoa mwanya kwa mafisadi kuendelea kuangamiza nchi na kuifanya kuwa masikini wakati ina rasilimali za kutosha ambazo zinaweza kuiendesha nchi bila kutegemea fedha za wafadhili.

Chanzo: Mwanahalisi Online

My take;
Wampe Magufuli mapema uenyekiti ili awapeleke haraka makada wenzake walio tufikisha hapa
 
Duh Mafisadi sasahivi ni matumbojoto. Presha inapanda presha inashuka ! ngoja nikae mkao wa kula nione nani atakuwa wa kwanza kupanda kizimbani.
 
Kwani tatizo lilikuwa majengo au ni mgumu huo ? Na hao majaji wanaagizwa kutoka mbinguni au ni wale wale wanufaika wa Escrow? KWA nini swala la immunity linamezewa? Tunao utashi kweli wa jambo hili?
 
  • Thanks
Reactions: cmp
mafisadi? Nafikiri lowassa ndio fisadi tu nchi hii baada ya kuhama CCM, mwingine yoyote hata aibe kiasi gani sio fisadi, wengine wamepigiwa kampeni na hiki chama kinachochukia ufisadi, wengine wamepewa nyadhifa bungeni,

wakati watu hawa walipaswa kunyang'anywa kadi ya chama na kufikishwa mahakamani ila wakawapitisha kwenye kura ya maoni na kuwa wagombea ubunge na wakapigiwa kampeni nzito,

kwani huyu Lowassa anayeandamwa na hawa wanaomtukuza huyu baada ya kukatwa jina angeamua kubaki CCM na kugombea ubunge kwani Magufuli asingempigia kampeni na kumsifu?

halafu leo hii tunaambiwa kuna mahakama ya mafisadi inaanzishwa kisha tunachekelea? Watanzania mbona tunakuwa mazuzu hivi?
 
Acheni uongo. Nani aliwaambia tatizo la kutoshughulikiwa kwa mafisadi ni kukosekana kwa Mahakama? Think BIG.

tatizo ilikuwa ni kiongozi mwenye nia ya dhati au utashi wa kisiasa wa kupambana na ufisadi. sasa raisi anaonesha anania ya dhati, hiyo mahaka ya mafisadi lengo ni kesi za ufisadi zihukumiwe haraka
 
Duh Mafisadi sasahivi ni matumbojoto. Presha inapanda presha inashuka ! ngoja nikae mkao wa kula nione nani atakuwa wa kwanza kupanda kizimbani.
Nyoka mwenye makengeza na 10m pesa ya mboga
 
Hebu tuone,kama waliochukua fedha na sandarusi stanbic hakuwatajwa.

Hisa za UDA pamoja na utata wake bado ziko Simon group.

Ununuzi wa rada,mabehewa.

Ubinafishaji wa NBC,mauzo ya makampuni ya umma.

Uuzwaji wa Kiwira coal mine.

Mikataba ya madini.

Kwa mtazamo wangu kikubwa ni utaishi wa viongozi kushughulikia ufisadi.Hivyo hatua alizochukua Mh.JPM tumpe muda na kuona Mahakama itatoaje Haki.Ila wanyonge wasionewe na wakubwa wakaachwa.
 
AHADI ya Rais John Magufuli kuanza kushughulika na viongozi wa umma wanaofanya ufisadi, sasa inapelekwa mkukumkuku, anaandika Faki Sosi.

Ikiwa tayari Bunge la Jamhuri limepitisha Sheria ya Uanzishwaji wa Mahakama nchini, Jukwaa la Haki na Jinai ambalo hujumuisha vyombo vya dola linakutana mjini Dodoma kuanza mchakato huo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria ambapo amesema kuwa, lengo la kikao hicho ni kufanya maandalizi ili khakikisha mahakama hiyo inafanya kazi zake kwa ufanisi.

Kikao hicho kinahitimishwa leo ambapo amesema, washiriki wake ni wale alio katika taasisi za haki jinai.

Taasisi zilizotajwa ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi.

Na kwamba, Takukuru wanapaswa kufanya uchunguzi kwa haraka, polisi watatakiwa kupeleleza haraka na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) atatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi.

Hatua ya kuelekea uanzishwaji wa mahakama hiyo ni ahadi ya Rais Magufuli kuahidi uanzishwaji wake wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Hivi karibuni, Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu alilieleza Bunge kuwa, tayari serikali ilianzisha Divisheni ya Mahakama ya Rushwa na Ufisadi katika Mahakama Kuu.

“Kuhusu ahadi ya kuanzisha Mahakama Maalum ya Ufisadi napenda kuliarifu Bunge lako kwamba, Serikali imeanzisha Divisheni ya Mahakama ya Rushwa na Ufisadi katika Mahakama Kuu itakayoanza kufanya kazi mwezi Julai 2016,” amesema Majaliwa.

Aliahidi kuwa, serikali itaimarisha Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kwa pamoja ziweze kuharakisha utoaji wa haki kwa kesi zitakazofikishwa kwenye mahakama hiyo.

Kiongozi huyo wa serikali aliongeza: “Serikali itaimarisha ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kwa pamoja ziweze kuharakisha utoaji wa haki.”

Katika siku ya kilele cha Wiki ya Mwaka Mpya wa Mahakama Jijini Dar es Salaam mapema mwaka huu, Rais Magufuli alimtaka Jaji Mkuu, Othman Chande kutosubiri Bunge kupitisha Sheria ya Uanzishwaji wa Mahakama ya Mafasidi, badala yake mahakama hiyo ianze kufanya kazi haraka iwezekanavyo.

Amesema, kuchelewesha kuanza kwa mahakama hiyo kunatoa mwanya kwa mafisadi kuendelea kuangamiza nchi na kuifanya kuwa masikini wakati ina rasilimali za kutosha ambazo zinaweza kuiendesha nchi bila kutegemea fedha za wafadhili.

Chanzo: Mwanahalisi Online

My take;
Wampe Magufuli mapema uenyekiti ili awapeleke haraka makada wenzake walio tufikisha hapa
Aliyenunua mabehewa fake ya tren naye atapanda kizimbani kwenye hiyo mahakama????
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom