Mafisadi papa wote,wahujumu uchumi wote ni kizazi cha waliochapwa viboko.

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,268
1,593
Miaka ya nyuma kila ilipo Shule palikuwa na msitu wa Miti, Miti hiyo kwa sehemu Kubwa ilikuwa ni maalumu kwaajili kukata fimbo za kuwachapia wanafunzi watukutu.Zama hizo viboko ilikuwa ni jambo la kawaida sana sana.Kosa Dogo tu walimu walikuwa radhi kuacha vipindi madarasani kwenda harambee ya kuchapa bakora.Kosa moja mwanafunzi aliweza kuchapwa hadi fimbo miamoja.Wale waliochapwa enzi hizo baadhi yao ndo hao wahujumu uchumi,mafisadi papa,Wanaoingia mikataba mibovu ya kuiba rasilimali za Taifa,wengine ndo hao wanaondesha siasa za kutofuata katiba ya nchi.Sijui viboko viliwasaidia kuwa na hofu ya Mungu? Lakini zama zile za viboko kushamiri mashuleni ndiyo zama ambazo Shule nyingi zilitawaliwa na migomo mingi sanaaa.Ndo kusema kwamba viboko vile viliwafanya wawe sugu hata kuendesha migomo bila woga?

Nafikiri tuangalie namna bora ya kutoa adhabu,hivi viboko si ndo vilivyo sababisha kifo cha mwanafunzi kule kagera na mwalimu aliye sababisha kifo kile kwa viboko amehukumiwa kifo hivi karibuni? Kama adhabu Hii ni halali nashauri yule Mwl aachiwe.
 
Nadhani ni kile cha miezi 18 sio mwaka mmoja chief 😁cha mwaka mmoja ni cha kwenda miaka ya 90 hivi!!
 
Hawa wazee wa zamani wako overrated sana wanajio wao ndio watakatifu wakati ndio kizazi cha ajabu sana..
Zamani migomo vyuoni na mashuleni ilikua kawaida sana lakini sasa hivi vijana wametulia hawana mambo ya kipuuzi ya migomo migomo..

Unakuta wazee wanalalamika vijana wananyia viduku na kuvaa modo.. wakati wao zamani walikua wanafuga minywele kichwani na kuvaa nguo zinazobana mapaja na kuachia chini... wanashindwa kuelewa hizi modo na viduku ni fashion tu ambazo hata zamani zilikuwepo na hazitakuja kuisha... utadhani walanafikiri kwa kutumia spinal cord
 
Back
Top Bottom