Mafisadi kuwekwa vyumba vya VIP,inatufundisha nini hasa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi kuwekwa vyumba vya VIP,inatufundisha nini hasa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Nov 15, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimefutilia kwa ukaribu sana matatizo mbali mbali yanayoikumba nchi yetu,na kutadhmini kwa kina utayari wa serikali yetu kuyatatua.Katika mambo yote ninayo 'conclusion' moja tu,nayo ni kwamba,serikali ama haina watendaji wenye uwezo wa kutekeleza wajibu wao,ama 'it's controlled by outside forces' au watendaji wana uwezo, lakini wanafanya wafanyayo kwa ajili ya maslahi binafsi.Nashawishika kusema kwamba, yote hayo matatu yamo katika uongozi wa nchi yetu and 'hence the magnitude of the problem.'Juzi tu tumeshuhudia mambo ambayo yanachefua.Jamani watu ambao wamechangia katika umaskini wa wananchi wetu wanawekwa 'VIP rooms' Keko?Kama sio matusi kwa wanachi maskini wa Tanzania ni nini.La kujiuliza hapa ni kwamba hawa wafanyakazi wa magereza wanaowaweka watu hawa katika vyumba vya VIP, wanafanya hivyo kwa amri ya nani.Kwanza hili wazo la 'VIP rooms' magereza, linatoka wapi.Kwangu mimi mhalifu ni mhalifu tu,swala la uVIP linatoka wapi.Watanzania maskini wenzangu, tuangalie matukio haya kwa umakini mkubwa sana.Hili na utendaji wa serikali yetu wenye kutiliwa mashaka kwa muda mrefu sasa, unanipa picha moja tu' kwamba serikali haiko 'serious' katika kuwashughulikia mafisadi inavyopaswa na hatimaye kuwaletea wananchi maendeleo yao.Nimesema mara nyingi kwamba serikali imewakosea wanachi wa Tanzania kwa kiwango cha kutisha sana.Ingekuwa vema kama serikali ingewaomba radhi wanachi na ikaadhimia kuanza upya kusaidia wananchi wa Tanzania.Mimi sioni hilo badala yake ninaona kichwa ngumu na 'business as usual.'Hakika hatufiki!
   
 2. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Watanzania wengine ni wafungwa lakini mafisadi ni wafungwa kuliko wafungwa wengine.

  Serikali hapa inalipa fadhila kwa kupotea fedha EPA. Anyway mgeni aje mwenyeji apone. Wakitokea mafisadi mara kwa mara basi labda magereza/jela zitafanywa zote za kisasa. That is according to my free will and comprehension. Vinginevyo ubongo wangu hauna maelezo mengine. Labda kesho nitapokuwa katika mood ya utulivu.
   
Loading...