Mafisadi kupokelewa majimboni kishujaa je ni usaliti? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi kupokelewa majimboni kishujaa je ni usaliti?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tatanyengo, Jul 15, 2011.

 1. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Imejitokeza mara kadhaa katika nchi yetu viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanapojiuzuru nyadhifa zao mara warudipo majimboni kwao hupokelewa kama mashujaa na washindi wa vita.Hali hiyo iliwahi kujitokeza jimboni kwa Adrew Chenge, Edward Lowassa na juzi kwa Rostam Aziz hadi baadhi ya wanachi kuzimia ovyo. Je wananchi wa majimbo hayo hawaoni kwamba wanawasaliti wananchi wengine wanaolipigia kelele suala la ufisadi? Naomba kuwasilisha>
   
 2. T

  Tata JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,734
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  Asante kwa swali lako. Mimi napenda kuliangalia kwa upana zaidi. Je ufisadi unachukiwa kwa kiasi gani kwenye jamii zetu za Tanzania nikianzia ndani ya familia zetu mojamoja, kitongoji, kijiji, kata, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla? Je ndugu yetu anapofanikiwa kujenga jumba kubwa la kifahari na kuendesha magari ya thamani kuliko uwezo wake huwa tunamhoji, kama familia, alipozipata pesa kedekede? Au tunaishia kumpa hongera na kumsifu kuwa ni mtu mwenye akili sana na zaidi ya hapo tunamtunuku uongozi ili aibe zaidi na kutugawia sehemu kidogo ya alichofanikiwa kukwapua..

  Turudi vijijini, kwa nini gari la abiria likipata ajali siku hizi kitu cha kwanza wanachofanya wananchi wanaoishi jirani na eneo la ajali ni kupora pesa na mali za wasafiri waliojeruhiwa? Je huu siyo wizi au ufisadi sawa na anaofanya Rostam Aziz? Wewe hujawahi kusikia kuwa wakati mwingine polisi hawafanikiwi kuwakamata wanaofanya huu unyang'anyi wa mali za abiria kwa sababu hawapati ushirikiano wa wananchi wanaoishi jirani na tukio?

  Hoja ninayojaribu kujenga hapa ni kuwa viongozi tulionao wanatoka kwenye familia zetu na zaidi kwenye jamii zetu na mambo wanayoyafanya yanaakisi mila, desturi, na utamaduni wetu katika kuendesha maisha yetu. Hivyo ufisadi wa Tanzania ni sehemu ya mila, desturi na utamaduni wa sasa wa mtanzania wa kawaida awe wa mjini au vijijini.

  Nikirudi kwenye swali lako la msingi iwapo wananchi hawaoni kuwa kwa kuwashangilia hawa mafisadi wanawasaliti wanaowapinga jibu ni HAPANA. Hawaoni kuwa ni wasaliti kwa sababu wanaamini kuwa watu wote wanaoishi mijini ni mafisadi na wanamshambulia huyo aliyejiuzulu kwa sababu ya husuda tu. Wanaamini kuwa hata ukimtoa huyo anayeitwa fisadi ukamwingiza mwingine naye atafisidi tu kwani ufisadi ndiyo urithi wetu kwa sasa tangu ulipoasisiwa na Azimio la Zanzibar lililopiku lile la Arusha.

  Kwa ufupi ufisadi unachochewa na ubinafsi wa mafisadi. Hivyo sera ya UBINAFSIshaji ambayo kimsingi imsingi wake mkuu ni ubinafsi ilitungwa kwa minajili ya kujenga mazingira ya Ufisadi unaoendelea sasa. Sera hii imehubiriwa kwa takriban miaka ishirini na CCM na imeeleweka vilivyo kwa wananchi. Ndio maana wananchi wa sasa hawatenganishi SIASA, UBINAFSISHAJI na UFISADI. Hivyo watu wote wanaoenda mikoani na vijijini na kuhubiri ubinafsishaji wanaeleweka kwa wananchi wa kawaida, ambao ni waelewa kuliko tunavyodhani, kuwa ni walewale yaani MAFISADI. Watu wa Igunga wanajua kuwa hata huyo watakaye mpigia kura baada ya Rostam ni fisadi mtarajiwa tu. Ndio maana kuna msemo maarufu toka kwa wananchi kwenda kwa wanasiasa, wakati wa kampeni za uchaguzi, wa "SISI UNATUACHAJE HAPA" ukiwa na maana kuwa uwape hongo ili wakufikirie. Hiyo ni Tanzania zaidi ya tuijuavyo.

  Baadhi walizimia kwa sababu hawana uhakika kama huyo fisadi anayekuja atakuwa mkarimu kama huyu aliyeondoka na kama wataweza kuwa na mahusiano ya kuwawezesha kupata mgawo wao wa ufisadi kama ilivyo kwa huyu wa sasa.
   
 3. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,613
  Trophy Points: 280
  1. wengi wao wanajipendekeza ili wapewe ya ugali.
  2.watanzania walio wengi wanajua mtu anayeiba ni masikini kwa sababu wakiona walio magerezani ni watu masikini.
  3.siku zote mtaji wa mafisadi ni;
  UJINGA na UMASKINI.
  so wanatumia ujinga wetu kutudanganya kwa kuwa wanajua hatuna elimu.
  na kwa kuwa sisi ni maskini wanatumia pesa zao kama kufuri ya midomo na akili hata wale walio na uelewa pesa zinawafunga akili na midomo.hii inawafanya waonekane mungu watu.mia.
   
 4. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hii inatokana na ubovu wa viongozi wahusika wenyewe pamoja na ujinga wa wananchi. Watanzania wengi wako 'illiterate' na bado wanaishi katika enzi au zama za nyuma. Hawajui majukumu ya viongozi ni nini na unapolalamika kuwa viongozi hawatekelezi majukumu yao wengi huona kuwa unawaonea viongozi wale wivu. Wananchi wengi hawajui wajibu wao kwa serikali na wajibu wa serikali kwao. Walishazoea kuwa serikali ni kitu kisichokuwa na uhusiano nao, isipokuwa tu katika kukusanya kodi na hawajui kuwa kodi zile zinakusanywa ili hatimaye zisaidie kuboresha maisha yao.

  Viongozi wengi wabovu hupenda kupendwa na kusifiwa na watu. Wanapoharibu mifumo ya serikali kwa ufisadi wao, hutumia sehemu ya mapato yao ya wizi kuwahonga wananchi, hasa wale wanaowatumia kuendelea kubaki madarakani. Kwanza huhakikisha kuwa wananchi hawaoni uhusiano uliopo kati ya utendaji mbovu wa serikali na viongozi wao. Hutumia udhaifu wa ujinga kwa wananchi walio wengi kuhakikisha kuwa wanawanunua kwa kuwapa vizawadi vidogo vidogo na kuhakikisha kuwa utendaji wao serikalini hauhojiwi na angalau hauonekani. Yaani wananchi kwa mfano wa kule Monduli, hawaoni uhusiano uliopo kati ya wao kukosa dawa hospitalini na uongozi wa waziri mkuu.

  Wananchi wengi (hasa walio vijijini) huona uongozi kama personal achievement. Na viongozi hawa, huendelea kuwaaminisha hivyo. Kwa hiyo suala la kuwa shule zao hazina walimu, hospitali zao hazina dawa, wananyang'anywa ardhi, n.k. hawayahusianishi mambo haya na utendaji wa viongozi walio madarakani. Kiongozi wa kutoka eneo lao, anaweza kushiriki kutunga sheria itakayosababisha wananchi wale wanyang'anywe ardhi, lakini kiongozi yule akienda kule kwao, huwaambia kuwa wanaofanya hivyo ni maadui zake wanaomuonea wivu; na wananchi wale wanakubali.

  Kwa kifupi, kiongozi fisadi anayeachishwa madaraka kwa kashfa halafu akapokelewa kama shujaa kwao, inaonesha ni jinsi gani alivyofanikiwa kuwa-brainwash watu wa kwao na jinsi alivyo-tayari kuwatumia kama ngao. Viongozi kama hao hawako tofauti na wale wapiganaji wanaowatumia watoto kama ngao; yaani anakufyatulia risasi, ukitaka kumrudishia, anakimbia katikati ya kundi la watoto ili uogope kumpiga kwa sababu ya kuogopa kuwapiga wale watoto.

  Viongozi wengi wa kiafrika wako hivyo! Ndiyo sababu hizi siasa za ukabila, udini, ujimbo na kadhalika zinajikita sana Afrika. Watu hawa wanapata hasa jeuri hiyo kwa sababu wananchi wengi bado ni mbumbumbu na hawajajua kufanya tathmini ya mambo. Ndo maana unaona viongozi wengi wa hivyo wakiguswa tu, hukimbilia katika yale makundi wanayojinasibu nayo kuwa wao wametokea huko. Wanajua wengi wa walio huko hawawezi kuwauliza maswali magumu.

  Wananchi wengi wa Bariadi hawaoni uhusiano wa kashfa ya rushwa iliyomkabili mbunge wao na matatizo walio nayo. Wakinyanyaswa na polisi sana sana watawlalamikia polisi wale na mkuu wao. Hawaoni picha kubwa, kuwa utendaji wa wale polisi unatokana na mfumo mzima wa serikali ulivyo na ukiwa mbovu polisi hawawezi kuwatendea wao haki.

  Tatizo hili ni kubwa, yaani tatizo la ujinga wa wananchi! Ndo maana viongozi wetu wengi wanafanya hivyo wanavyofanya. Suluhisho halitakuja kirahisi, mpaka wananchi wengi watakapoelimika formally na informally! Kwa hali ilivyo sasa hivi bado mambo ni mabaya na wananchi wengi hawajui hasa wanataka nini! Ndo maana wanamshangilia kiongozi aliyejiuzuru kwa kashfa ya kuwaibia, kwani hawajui kuwa kile kilichoibiwa ni chao. Wananchi wengi hawaoni kwa mfano kuwa kwenye madini tunaibiwa kwani wengi wanasema - "si hatuna uwezo wa kuyachimba? Waache wanaoweza kuchimba wachukue!!" Ni kutokana na kundi kubwa la wananchi kuwa wa hivi ndo maana tunapata viongozi wa aina hiyo tuliyo-nayo; ama kweli tunapata viongozi tunaostahili.
   
 5. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ni uviazi wa wapiga kura wao.njaa Jaman
   
 6. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wanamsaliti mwananchi gani!Wakati wanaempokea ni Mwakilishi wao waliemchagua kwa manufaa yao!Ndg yangu wewe vp, Dunia ya Leo Unasikiliza makelel!Mbona hata baadhi ya wezi huiba afu ndio wa kwanza kupiga Kelele za mwizi
   
 7. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wajinga ndio waliowao.
   
Loading...