Bill
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 8,277
- 8,492
Katika hali inayoonyesha kuwa ni JITIHADA ZA KUFIFISHA MOTO WA VITA YA UFISADI nchini, mafisadi wanajipanga kumng'oa Mbunge wa Kishapu ndugu Fredrick Tungu Mpendazoe. Mpaka sasa Mafisadi wakiongozwa na Kinara wao wao Rostam wameanza jitihada za kumchafua. Jumamosi iliandikwa katika Gazeti la Mtanzania kuwa Mpendazoe anatengeza makundi jimboni, jana Jumatano gazeti la Majira limerudia habari hiyo. Mtu anayeandaliwa na Mafisadi kuchukua nafasi hiyo ni Katibu mkuu wa UVCCM ndugu Shigela ambaye ana baraka zote za Mafisadi ikisemakana na Mkuu mwenyewe Mr Handsome.
Kwa hatua hii bado vita dhidi ya ufisadi ni ngumu na ndugu wana JF tuchangie kuona ni jinsi gani Mpiganaji mwenzetu ndugu FT Mpendazoe atabaki kuendeleza moto wa ufisadi
Kwa hatua hii bado vita dhidi ya ufisadi ni ngumu na ndugu wana JF tuchangie kuona ni jinsi gani Mpiganaji mwenzetu ndugu FT Mpendazoe atabaki kuendeleza moto wa ufisadi