mafisadi kuliko mchwa kwa kuila nchi

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,187
671
Mafisadi sasa wahujumu TRA bandarini, mipakani
2008-05-05 09:06:28
Na Patrick Chambo, PST, Kilimanjaro


Mradi wa kuhakiki bidhaa ziingiazo nchini wa Tiscan unaomilikiwa na Kampuni ya Cotecna Group, unadaiwa kuchezewa na baadhi ya maofisa waandamizi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kushirikiana na wafanyabishara wakubwa na hivyo kuiibia serikali mamilioni ya fedha.

Mradi huo ndio uliopewa dhamana na serikali kuhakiki mizingo ya makontena yote yanayoingia nchini ili kubaini kama kuna ukwepaji wa kodi za serikali na udhibiti wa mali ambazo ni hatari kuingia nchini.

Baadhi ya makampuni yamekamatwa na nyaraka halali za Tiscan zikionyesha kuwa yamekaguliwa bandarini, viwanja vya ndege na mipakani wakati sio kweli, na mbaya zaidi, baadhi ya makontena yamesheheni mali zilizopigwa marufuku na serikali.

Kamshina wa Forodha nchini, Bw. George Lauwo, alikiri kuwapo kwa matukio hayo, alipofanya mahojiano maalumu na PST na kuongeza kuwa zaidi ya makampuni 10 ya kuhakiki bidhaa yamefutwa kutokana na udanganyifu.

Alizidi kusema kwamba baadhi ya makampuni yaliyotumia misamaha ya kodi vibaya nayo yamefutiwa vibali vyao. Hata hivyo, hakutaja idadi ya makampuni hayo.

Bw. Lauwo, alisema mradi wa Tiscan ni ukombozi kwa TRA na serikali katika ukusanyaji wa kodi za serikali na kuwa katika kupambana na makampuni yasiyokuwa na uadilifu wamekuwa wakitoa alama za uaminifu.

Hata hivyo, alisema kuwa hana taarifa za maofisa wa TRA kumiliki kampuni za uhakiki wa mali.

``Tiscan unatuwezesha kujua gari hili ulinunua wapi na kwa shilingi ngapi?... Au umebeba nini katika kontena tunaweza kujua kuna nini ndani,`` alisema kamishna huyo.

Kuhujumiwa kwa mradi huo, kumetokana na baadhi ya maofisa waandamizi wa TRA kutoka mikoani na makao makuu wanaofahamu kasoro za Tiscan na hivyo kufungua makampuni ya uhakiki wa bidhaa kutoka na kuingia nchini na wengine kujiingiza katika biashara za makampuni na kufanikiwa kupata misamaha ya kodi, hali ambayo imeleta mgongano wa maslahi ndani ya TRA.

Baadhi ya makampuni ya wakubwa hao wa TRA yaliyokiri kwa maandishi kwa Kamishna wa TRA Forodha katika Form Na. 71 ya Ushuru wa Afrika ya Mashariki katika sheria ya mwaka 2004, kuwa wameihadaa TRA na serikali kwa kuuza mali walizosamehewa kodi na kukiri makampuni yao kufanya hujuma, wamerejeshewa tena vibali waendelee na misamaha yao au kuwa wakala wa TRA kwa kukingiwa kifua na baadhi ya Makamishna wa TRA, imedaiwa.

Waandishi waliokuwa wakifanya uchunguzi wa upotevu wa kodi za serikali na ufisadi ndani ya TRA katika maeneo ya bandari, mipakani na viwanja vya ndege wameelezwa kuwa kutokana na baadhi ya maofisa hao waandamizi, kwa kushirikiana na baadhi ya makamishna wa TRA kujiingiza katika biashara, kumekuwa na mvurugano katika utendaji wa TRA ambapo ofisa mmoja anapofungia kampuni, mwingine anaipatia kubali cha kuendelea na kazi.

Mradi wa Tiscan unakagua asilimia 80 ya makontena katika Bandari ya Dar es Salaam na asilimia 20 ni kutoka katika mipaka na viwanja vya ndege mikoani ambapo mradi huo huchukua asilimia 1.2 ya kodi zinazolipwa kwa serikali katika kila kontena.

SOURCE: Nipashe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom