Elections 2010 Mafisadi kuamua nani awe rais 2010?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Mafisadi kuamua nani awe rais 2010?

Godfrey Dilunga Machi 18, 2009
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Mbunge wa CCM asema nchi iko rehani

MBUNGE wa Kishapu, Fred Mpendazoe, amesema kutokana na matajiri mafisadi kuachwa wakitamba watakavyo, zipo dalili za wazi sasa kwamba wamejipanga kuamua nani awe rais wa nchi, mbunge, waziri na hata diwani; wakipora jukumu hilo kutoka kwa wananchi.

Akionyesha kukerwa na mwenendo wa mambo na hasa kuimarika kwa matabaka miongoni mwa wananchi, mbunge huyo amesema mafisadi hao wameweka mizizi yao ndani ya serikali, na nchi inaelekea kuwekwa rehani kwao.

"Kinachofanyika sasa kinazidi kutoa harufu ya ufisadi kwenye serikali. Upo msemo wa kisambaa unaosema kama unataka kuepuka nzi tupa kibudu cha mzoga. Kama Serikali inataka kuepuka harufu ya ufisadi, ishughulikie vyanzo vya ufisadi na iviondoe la sivyo itaendelea kuandamwa na kashfa," anasema Mpendazoe katika mahojiano na gazeti hili ambayo yamechapishwa kwa kina.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, tatizo kubwa linaloitafuna serikali ya sasa ni uteuzi kufanyika katika misingi ya urafiki; hali inayowakwaza wenye mamlaka ya kuteua na hatimaye kushindwa kuwawajibisha wateule pale wanaposhindwa kutimiza wajibu wao.

"Upo msemo kwamba A friend in power is a friend lost; yaani rafiki yako akipata madaraka na dhamana kubwa ya kuongoza anakoma kuwa rafiki," anasema na kufafanua kuwa;

"Anakoma kuwa rafiki yako ili aweze kutekeleza majukumu yake bila kuwa na upendeleo wowote. Nchi nyingi zinazoendelea zina tatizo hili. Mtu anapopata madaraka utakuta anaweka rafiki zake kwenye sehemu nyeti akidhani watamsaidia kumbe huwa ni kinyume chake."

Akizungumzia kuhusu nchi kuwekwa rehani, mbunge huyo alisema ni jambo hatari sana, "maana yake serikali itaongozwa na matajiri na hivyo haitawajibika tena kwa wananchi na demokrasia itakoma na udikteta utaanza.

"Serikali haitakuwa ya watu na kwa maana hiyo haitachaguliwa na watu na haitawajibika kwa wananchi. Matajiri wataamua nani awe rais, nani wawe wabunge kwenye majimbo," anasema na kuongeza kuwa;

"Wananchi hawatachagua madiwani wanaowataka. Baadaye matajiri wataamua nani awe waziri, jaji na wakuu wa vyombo vya dola ili kuhakikisha maslahi yao yanalindwa sehemu zote kwa mwavuli wa maslahi ya Taifa.


Na zipo dalili za kuelekea huko. Serikali inapochelewa kuchukua hatua haraka juu ya ufisadi unaotendeka si dalili nzuri."

Katika kushauri nini kifanyike, mbunge huyo alisema; "Mfumo wa utawala tulionao unaotokana na Katiba hautoi fursa kwa watendaji kuwajibishana bali unatoa nafasi kubwa ya kulindana.

Ni mfumo wa viongozi kulindana badala ya kuwajibishana inapobidi."


Akiweka wazi msimamo wake kuhusu sakata la ununuzi wa mitambo ya kufua umeme ya Dowans, na hususan kauli ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, mbunge huyo alimshauri waziri huyo kuwasilisha hoja yenye malalamiko yake kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, ili yajadiliwe.

Katika hatua nyingine, alitonya kuwa kuna uwezakano wa kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu suala la Dowans, na alipoulizwa lini hatua hiyo inaweza kufanyika alijibu kwamba ni katika mkutano ujao wa Bunge.
 
Fred Mpendazoe: Uchumi wa nchi umo mikononi mwa familia tisa za matajiri

Godfrey Dilunga Machi 18, 2009
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

MACHI 12, mwaka huu, Mwandishi Wetu Godfrey Dilunga alifanya mahojiano na Mbunge wa Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa. Mahojiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam na yafuatayo ndiyo yaliyojiri.

Swali: Watalaamu na wananchi wanaonya kwamba matabaka yanazidi kuimarika na pengo kati ya masikini na matajiri linazidi kuimarika. Unakubaliana na mtazamo huo?

Jibu: Ni kweli kumeanza kuibuka matabaka mbalimbali katika jamii yetu na chanzo kikubwa ni uporaji wa uchumi unaofanywa kwa njia mbalimbali za ufisadi.

Swali: Umezungumzia kuibuka matabaka mbalimbali ni yapi hayo?

Jibu: Kwa sasa matabaka manne yanaibuka na kuzidi kuimarika kila kukicha. Tabaka la kwanza linaundwa na matajiri. Tabaka hili linaweza kumiliki sehemu kubwa ya uchumi wa nchi kwa njia ya ufisadi…kwa Lugha ya Kigiriki tabaka hili linaitwa Oligaki.

Inasemekana uchumi wa Tanzania kwa sasa unamilikiwa na familia tisa za matajiri. Hizi familia tisa zinaweza kutoa fedha ya kuendesha nchi. Tabaka hili la oligaki linatengeneza tabaka la pili ambalo ni tabaka la wateule wanaojiona bora kwenye jamii kwa Kigiriki linaitwa Aristokrasi.

Oligaki wataweka watu wao kwenye sehemu muhimu na nyeti kwa ajili ya kulinda maslahi yao kwa mwavuli wa maslahi ya Taifa, mfano benki, wizara nyeti (fedha) na kwenye ofisi za mabalozi za nje. Wanaowekwa katika sehemu (ofisi) hizo ndiyo wateule, yaani aristokrasi

Tabaka la tatu ni la watu wenye tamaa ya madaraka kwa Kigiriki tabaka hili huitwa Timokrasi. Hili ni tabaka linaloundwa na wanafiki wanaounga mkono hoja za oligaki (matajiri) na aristokrasi (wateule wa matajiri) kwa ajili ya kupewa chochote ili waseme lolote.

Timokrasi ni watu wasio na msimamo wowote kwani wametawaliwa na tamaa na makuu, hivyo ni rahisi kuwasaliti wananchi.

Tabaka la nne ni la wananchi wanaoishi kwa matumaini ya kupata maisha bora ambayo ni vigumu sana kuyapata kutokana na kuimarika kwa tabaka hizi.

Swali: Kwa mujibu wa maelezo yako, uendeshaji wa siasa, uchumi na masuala mengine nyeti kwa Taifa umekwishaingiliwa?

Jibu: Kwa sasa ni dhahiri wapo wananchi wachache matajiri sana na wapo wananchi wengi masikini kwenye nchi hii yenye utajiri mkubwa wa rasimali. Na chanzo kikubwa cha hali hiyo ni ufisadi kama alivyosema Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba, mwaka 2000, kwamba pengo kati ya matajiri na masikini limeongezeka, na siasa imetekwa na matajiri. Ufisadi na rushwa vimekuwa muhimu kwenye chaguzi.

Naomba nimnukuu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere juu ya ufisadi na matokeo yake ambayo ni kuibuka kwa matabaka. Alisema; "Utajiri katika Tanzania unaweza kupatikana kutokana na rushwa kwa watumishi wa umma au kutokana na wafanyabiashara ambao wanawania nafasi za kisiasa ili wawe wadeni wa Rais aliyeko madarakani."

Tafsiri ya maneno haya ni kwamba anaweza akapatikana Rais kwa kugharimiwa na matajiri na akiwa madarakani itabidi alipe fadhila kwa matajiri waliomfadhili yeye na chama chake wakati wa uchaguzi. Zipo dalili kwamba haya yameanza kutokea.

Swali: Je, ni nini madhara zaidi ya kuibuka kwa matabaka haya nchini?

Jibu: Kutokana na mwenendo unaoendelea kwa sasa wa kuibuka na kuimarika kwa matabaka, unaotokana na uongozi kununuliwa kwa fedha, matokeo yake ni nchi kuwekwa rehani kwa matajiri kama alivyosema Rais Jakaya Kikwete.

Na nchi kuwekwa rehani kwa matajiri ni jambo hatari sana, maana yake serikali itaongozwa na matajiri na hivyo haitawajibika tena kwa wananchi na demokrasia itakoma na udikteta utaanza.

Serikali haitakuwa ya watu na kwa maana hiyo haitachaguliwa na watu na haitawajibika kwa wananchi. Matajiri wataamua nani awe rais, nani wawe wabunge kwenye majimbo.

Wananchi hawatachagua madiwani wanaowataka. Baadaye matajiri wataamua nani awe waziri, jaji na wakuu wa vyombo vya dola ili kuhakikisha maslahi yao yanalindwa sehemu zote kwa mwavuli wa maslahi ya Taifa.

Na zipo dalili za kuelekea huko. Serikali inapochelewa kuchukua hatua haraka juu ya ufisadi unaotendeka si dalili nzuri. Nakubaliana na mtaalamu wa Hisabati na Mwanafalsafa, Albert Einstein, aliyesema kwamba ulimwenguni pamekuwa mahali pa hatari sana kuishi, lakini haitokani na ufisadi unaofanyika, bali inatokana na wale wanaouangalia tu uovu ukifanyika na hawachukui hatua yoyote.

Swali: Kutokana na maelezo hayo ya Albert Einstein, Tanzania patakuwa mahali hatari pa kuishi?

Jibu: Kulingana na Einstein, Tanzania patakuwa mahali hatari kuishi, lakini haitokani na ufisadi unaofanyika bali inatokana na serikali kuchelewa kuchukua hatua madhubuti juu ya ufisadi unaofanyika. Ni muhimu serikali kuchukua hatua mapema dhidi ya ufisadi unaofanyika.

Swali: Katika moja ya vikao vya Bunge nakumbuka katika moja ya michango yako uligusia suala la kuwa na Katiba mpya. Je, Katiba ya sasa ina upungufu gani?

Jibu: Katiba ni sheria kuu ya nchi, ni sheria mama ya sheria zote nchini kwa kuwa inagusa nyanja na mifumo yote ya utawala wa nchi kisiasa, kiuchumi na kijamii. Maliberali wenyewe wanasema Katiba ni ramani ya madaraka ya nchi inayoonyesha jinsi mamlaka ya nchi yanavyopaswa kusimamiwa na kuratibiwa ndani ya vyombo vya utawala.

Kutokana na ufafanuzi huu, maoni yangu ni kwamba mfumo wa utawala tulionao unaotokana na Katiba hautoi fursa kwa watendaji kuwajibishana bali unatoa nafasi kubwa ya kulindana.

Ni mfumo wa viongozi kulindana badala ya kuwajibishana inapobidi.

Swali: Umesema ni mfumo wa viongozi kulindana badala ya kuwajibishana. Sababu gani zinazoambatana na maelezo yako hayo?

Jibu: Katiba yetu inatambua mihimili mitatu, Bunge, Serikali na Mahakama. Bunge kwa niaba ya wananchi linaisimamia serikali na kutunga sheria, Mahakama inatafsiri sheria na serikali inatekeleza mipango na sera zilizopitishwa na Bunge kwa kufuata sheria za nchi.

Kwa maoni yangu, ili Bunge liweze kuisimamia vizuri serikali ilipaswa taasisi kama TAKUKURU, Usalama wa Taifa, Tume ya Haki za Binadamu na Tume ya Maadili, watendaji wakuu wake wateuliwe na Rais, lakini waidhinishwe na Bunge na wawajibike bungeni kupitia Kamati za Kudumu za Bunge.

Kwa sasa watendaji wakuu wa taasisi hizi huteuliwa na Rais na wanawajibika kwake. Kutokana na mfumo huu ni vigumu sana watendaji wakuu hawa wakatoa taarifa ambayo itaikosoa serikali na ikubalike.

Utendaji kazi wa wakuu wa taasisi hizi hauwezi kuwa huru, bali utailinda serikali isionekane imeshindwa. Mfumo huu tuliourithi ni wa kulindana.

Kulingana na Katiba yetu, mawaziri wanatokana na wabunge. Katiba inaeleza kazi ya mawaziri ni kumshauri Rais, lakini wametokana na wabunge wanaoisimamia serikali na wao ni sehemu ya Bunge.

Swali: Katika mazingira haya, nafasi ya Bunge ikoje katika suala la kutimiza wajibu wake?

Jibu: Hapa ni kwamba usimamizi wa Bunge unapunguzwa nguvu, unaegemea zaidi kwenye ushauri usioilazimisha serikali kutekeleza iliyoagizwa. Mfumo huu unasababisha mvutako kati ya Bunge na Serikali na matokeo yake ni kupoteza muda na kuchelewesha maendeleo. Ni vema mawaziri wasitokane na wabunge.

Swali: Mgongano huo wa madaraka pia umo katika siasa. Rais ndiye mwenyekiti wa chama tawala, ambacho kina jukumu la kuisimamia serikali anayoiongoza. Hili unalizungumziaje?

Jibu: Katika vyama vya siasa, nashauri Rais asiwe pia mwenyekiti wa chama tawala. Chama kinaposhinda uchaguzi kazi yake kubwa ni kuhakikisha ilani ya uchaguzi ya chama inatekelezwa ipasavyo na serikali yake. Hivyo chama huisimamia serikali.

Mfumo tulionao, Rais ndiye mwenyekiti wa chama. Hivyo asipotekeleza vizuri ilani ya uchaguzi, hakuna kikao cha kumwajibisha.

Kama ni Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama yeye ni mwenyekiti, atawasilisha taarifa ya utekelezaji kwa chama kama Rais, baadaye wajumbe wa NEC wataijadili yeye akiwasikiliza kama mwenyekiti wao.

Ni mfumo wa kulindana si kuwajibishana. Na mawaziri wengi hugombea ujumbe wa NEC, hivyo waziri wa sekta atawasilisha taarifa ya sekta yake na yeye ataijadili kama mjumbe wa NEC na ikumbukwe waziri ni mshauri mkuu wa Rais katika sekta husika.

Hapa kuwajibishana si rahisi. Hali hii ipo mpaka ngazi ya kijiji. Vijijini, wajumbe wa serikali ya kijiji pia wengi huwa ni wajumbe wa halmashauri ya chama tawala. Kwa hiyo halmashauri ya chama tawala ya tawi haiwezi kuiwajibisha halmashauri ya serikali ya kijiji kutokana na kwamba unaweza ukakuta wajumbe wa halmashauri ya tawi ya chama tawala pia ni wajumbe wa halmashauri ya serikali ya kijiji. Watalindana, lakini matokeo yake hakuna maendeleo.

Taarifa za vikao hivyo huwa ni nzuri na hupigiwa makofi sana, lakini maendeleo hakuna. Ipo haja ya kubadili mfumo.

Swali: Kuna malumbano kuhusu ruksa ya Katiba katika kumshitaki Rais aliyestaafu ambaye amebainika kufanya makosa. Hili unazungumziaje?

Jibu: Ibara ya 46(2) ya Katiba inasema; "Rais mstaafu hawezi kufikishwa mahakamani kwa kosa la jinai alilolitenda wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais.

Kuna haja ya kuiangalia Katiba yetu ili tujihakikishie kwamba ina nguvu za kutosha kuilinda nchi yetu dhidi ya viongozi au Rais mchaguliwa ambaye anaweza kuamua kupora au kuruhusu uporaji wa uchumi wa nchi.

Uporaji wa uchumi wa Taifa letu unaofanywa na unaoweza kufanywa na watu wachache unatakiwa kudhibitiwa kikatiba kama tunataka nchi isalimike. Hali ya uovu inapoongezeka ndivyo tunapohitaji Katiba imara zaidi na sheria kali.

Mwanafalsafa Plato anasema hivi juu ya kuwapo sheria; "Watu wema hawahitaji kuwapo sheria kwani wao huishi na kutenda kiungwana, wakati watu waovu siku zote hutafuta namna ya kuzizunguka sheria."

Swali: Nini maoni yako kuhusu mjadala wa ununuzi wa mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans?

Jibu: Naunga mkono maoni yaliyotolewa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, William Shellukindo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, na Makamu wake, Dk. Harrison Mwakyembe. Nasisitiza mambo matatu.

Mosi, Kama Serikali ingekuwa imetekeleza maazimio ya bunge yanayohusu kuwawajibisha watendaji wa Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini waliojihusisha na kuishauri vibaya serikali kuhusu mchakato wa Richmond, haya yalitokea yasingetokea.

Walioishauri serikali wakati wa Richmond ni wale wale wanaoishauri serikali juu ya mitambo ya Dowans iliyokuwa ya Richmond. Hawajawajibishwa, wapo kwenye nafasi zile zile. Kilichofanyika ni kutaka kujisafisha na kashfa ya Richmond. Ni muhimu serikali iwawajibishe watendaji hao.

Pili, suala alilotahadharisha Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco kwamba nchi inaweza kuingia giza kwa kutonunuliwa mitambo ya Dowans, Watanzania walichukulie kwa uzito wake.

Inawezekana kweli nchi ikawa giza na kupata athari kubwa kijamii na kiuchumi kwa kukosa umeme, lakini si kwa kukosa kuinununua mitambo ya Dowans bali ni kwa hujuma au uzembe wa Tanesco.

Nilitarajia Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco alipoona hoja yake haikukubalika angejiuzulu. Hajajiuzulu, basi, serikali itafute mkurugenzi mwingine mwenye maono mapya anayeweza kupata mipango mbadala wa Dowans.

Swali: Kuna hatua zozote za ziada zinazoweza kuchukuliwa na Bunge na hata kwa upande wako?

Jibu: Upo uwezekano kupeleka bungeni hoja binafsi kutaka viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini wawajibishwe kwa kuiacha Tanesco iendelee na suala la Dowans. Na serikali ifahamu Bunge linaisimamia kwa niaba ya wananchi.
 
He is right. Hiyo ndiyo faida ya kutawaliwa na CCM karne hii. Nyerere atalaumiwa sana kwa hili kwa sababu ndiye aliuwa nguvu za upinzani mwaka 1995, na hivyo kuifanya CCM ijenge matabaka haya ambayo hayakuwapo au yalikuwa hayajakomaa wakati huo. Ingawa wagombea wengi wa upinzani wakati ule walikuwa dhaifu, hasa kwenye viti vya bunge, wagombea wa viti vya Rasi wa Muungano na Rais wa Zanzibar walikuwa imara ila Nyerere ndiye aliyewavuruga. Mabadiliko madogo ya namna hiyo wakati ule yalikuwa ya muhimu sana kwa maendeleo ya nchi hii.
 
He is right. Hiyo ndiyo faida ya kutawaliwa na CCM karne hii. Nyerere atalaumiwa sana kwa hili kwa sababu ndiye aliuwa nguvu za upinzani mwaka 1995, na hivyo kuifanya CCM ijenge matabaka haya ambayo hayakuwapo au yalikuwa hayajakomaa wakati huo. Ingawa wagombea wengi wa upinzani wakati ule walikuwa dhaifu, hasa kwenye viti vya bunge, wagombea wa viti vya Rasi wa Muungano na Rais wa Zanzibar walikuwa imara ila Nyerere ndiye aliyewavuruga. Mabadiliko madogo ya namna hiyo wakati ule yalikuwa ya muhimu sana kwa maendeleo ya nchi hii.

Kichuguu..
Lakini sisi watanzania si ndio tulipiga kura? Nashindwa kukuelewa unapomlaumu Nyerere kwa hii issue.. Tulikuwa na uwezo wa kukubaliana nae au kumkatalia na kuchagua hao magombea kutoka upinzani..
 
Kwa kweli sioni mantiki kwa mtu anayemlaumu Mwalimu (RIP) aliyefariki miaka mingi iliyopita!

Wapiga kura ndio wa kulaumiwa.
 
Sasa pale inapoambiwa achaneni na kuwapigia mafisadi makelele na badala yake nguvu zielekezwe kwenye Katiba ,huwa mnashikwa na kizunguzungu.
Kuendelea na kufukuzana na mafisadi ni kuwapa njia ya kujipanga upya na kutafuta sehemu zilizo kuwa dhaifu kujipitisha na kuweza kuzuka upya kwa njia nyingine ,wakati kuna makurupushano na mafisadi ni lazima wananchi kwa upande wao waelekeze nguvu zao kwenye mabadiliko makubwa ya katiba ya Nchi asikubali mtu yeyote yule anaedai kuwa kwa sasa Tanzania haihitaji mabadiliko ya Katiba ,mtu huyo tumtambue kuwa ni adui wa Taifa hili ,aidha atakuwa ni mwega unaotumiwa na mafisadi katika kujilinda na kuendeleza ufisadi.

Haya mabishano ya akina Mwakiyembe na Rustum ni ubabaishaji mkubwa unaofanywa na serikali ,watu wanabishana njenje na serikali inakodolea macho tu ,sababu ni wao kwa wao ,ni wenyewe kwa wenyewe maana hii nchi Sultani CCM ameifanya yake yeye na wafuasi wake ,hivyo inaonekana kama ni vita vya ndugu ,ili kuheshimiana inabidi waachwe wapigane ,ndio maana watu wanasikika wakisema Tanzania hatuna serikali inayowasaidia wananchi wake bali tuna genge linalotazama maslahi yao binfsi ,na genge hilo linapoamua kuwasaidia wananchi inakuwa ni kama sadaka.
 
I agree with Hon. Mpendazoe, lakini swai langu ni kwamba, kwa kufahamu kiini cha haya matatizo kuwa ni ufisadi unaoendelea kupaliliwa na kushabikiwa na CCM, then why is he still a member and a leader in this party? Haoni kwamba na yeye anakuwa ni part of the problem?
 
Kichuguu..
Lakini sisi watanzania si ndio tulipiga kura? Nashindwa kukuelewa unapomlaumu Nyerere kwa hii issue.. Tulikuwa na uwezo wa kukubaliana nae au kumkatalia na kuchagua hao magombea kutoka upinzani..

Labda hukumbuki kilichotokea mwaka 1995.
Tukubali kuwa Nyerere alikuwa na nguvu sana na mara nyingi alilosema lilikubaliwa; hivyo alipotembea karibu nchi nzima akimnadi Mkapa na kumponda Mrema, wananchi kwa kumuamini wakamuacha kipenzi chao Mrema na kufuata ushauri wa Nyerere. Huwezi kuwalaumu wananchi kwa hili maana ilikuwa ni muda mfupi Nyerere alikuwa ametoa kitabu cha uongozi na Hatima ya Tanzania ambamo aliwashambulia viongozi waliokuwa madarakani. Huyu ni baba wa Taifa, watu wakamuamini.
Pili likaja suala la matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar. DTV wakati huo ilionyesha fomu ya matokeo ambayo Sei Sharrif wa CUF alikuwa ameshinda na kuna watu walimuona komandoo Salmini DSM akiwa amekimbia Zanzibar baada ya kuona ameshindwa.
Inasemekana ni Nyerere aliyekwenda Zanzibar usiku na kuwalazimisha Tume ya Uchaguzi Zanzibar kubadilisha matokeo kwa kuharibu kura nyingi za CUF hadi ikaonekana CCM imeshinda. Kura ziliharibiwa nyingi kiasi kwamba ili mshindi apate zaidi ya 50% ilibidi tafsiri ya kura halali ibadilishwe iwe kwamba kura zinazoharibika si sehemu ya kura halali zilizopigwa.
Kukaja suala la matokeo ya ubunge DSM, ikaonekana DSM yote imechukuliwa na wapinzani, Nyerere akasema, inawezekanaje makao makuu ya nchi yatekwe na upinzani? usalama utakuwa wapi? Ikabidi uchaguzi wote wa DSM ufutwe saa tisa usiku wakati watu wote wameshapiga kura na matokeo vituoni yalishatolewa yakionyesha wapinzani kushinda!!
Hayo na mengine mengi yaliyomhusu Nyerere kuingilia kati masuala ya uchaguzi huo, ndiyo yanayowafanya watu wamlaumu. Hivyo wanaomlaumu wanayo sehemu fulani ya haki kufanya hivyo.
Ni kuanzia wakati huo ilipoonekana wazi kuwa watu wanaweza kupiga kura lakini matokeo yakatolewa tofauti. Kumbuka pia usemi aliomwambia Kaunda wa Zambia aliposhindwa "unayo serikali, una vyombo vyote vya dola, inawezekanaje ukashindwa?"
NAWASHANGAA KAMA HAYO HAMYAKUMBUKI
 
Sasa natambua sababu zinazowafanya mafisadi kule Shinyanga kumpiga vita mh. Mpendazoe!! He is patriotic and one of the few wabunge who are quiet but very analytical!! Unfortunately, ccm cannot support a legislator of his caliber because he puts his country first unlike the Ngombales!!
 
Back
Top Bottom