BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,005
Posted Date::6/2/2008
'Mafisadi hawapaswi kukaa meza moja na Kawawa, Mwinyi'
Na Salma Said, Zanzibar
Mwananchi
MFANYABIASHARA maarufu mjini hapa, Mohammed Raza amedai kushangazwa na Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kushindwa kuwachukulia hatua wajumbe wake wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kusisitiza hawapaswi kukaa meza moja na wazee wanaoheshimika, Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Rashid Mfaume Kawawa.
Kauli hiyo aliitoa jana nyumbani kwake Kibweni mjini hapa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tuhuma hizo ambazo zinawakabili baadhi ya wanachama wa chama hicho.
Raza, alisisitiza kuwa, CC ya CCM ni chombo nyeti na chenye dhamana kubwa kwa Taifa kwa vile kinawajumuisha viongozi wakuu wa kitaifa na marais wastaafu, hivyo haitakuwa busara kwa mafisadi kushiriki katika vikao hivyo.
Ingawa hakutaja jina wala cheo, Raza, alidai katika vikao hivyo vya kamati hiyo, wamo wajumbe wanaotuhumiwa kwa ufisadi, hivyo katika hali ya kawaida wanawasononesha wazee kama waziri mkuu mstaafu, Rashid Kawawa, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na wengine ambao wanaheshimika sana nchini.
Raza ambaye alikuwa mshauri wa michezo wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), alikishauri CCM kuhakikisha kila mwanachama wake aliyetuhumiwa kwa ufisadi, anahojiwa na kufikishwa katika vyombo vya kisheria.
" CCM kingewahoji hawa wanaotuhumiwa kwa ufisadi ambao wengine ni wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu, tukisema tunamficha maiti chumbani kwa kuogopa kilio, siku moja tutakimbia sisi wenye nyumba kwa harufu, alisema.
Alisema ni vyema urafiki ukawekwa kando na kutangulizwa maslahi ya umma mbele kwa kuwa nchi hii ni ya Watanzania wote na akasisitiza kuwa kamwe kundi haliwezi kuongoza nchi.
Inanipa mashaka Kamati Kuu inakutana katika vikao vyake wakiwa na wajumbe ambao ni mafisadi, chama chetu hakina bwana na wala kundi haliwezi kuongoza nchi, kwa hivyo ni muhimu kushughulikiwa suala la mafisadi ili chama chetu kiendelee kushinda, alisema.
Mfanyabiashara huyo alimuomba Rais Jakaya Kikwete kushughulikia ufisadi nchini kwa kuwa Watanzania wengi wako nyuma yake wakimuunga mkono.
Raza, alisema mabilioni ya fedha yaliyochotwa na mafisadi katika akaunti ya nje ya ulipaji madeni EPA ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), zingetosha kuhudumia jamii kama sekta za afya, elimu na muhimu kwa wananchi, lakini zimeishia kuwanufaisha wachache.
Alidai umefika wakati wananchi wakaguna kwa kususia kununua bidhaa zinazozalishwa na kampuni ambazo wamiliki wake wanahusishwa na ufisadi nchini kwani biashara zao, utajiri wao unatokana na wao kuzinunua.
Katika mkutano huo, alizungumzia tatizo la umeme visiwani Zanzibar, akijigamba kuwa yuko tayari kushirikiana na serikali kulipatia ufumbuzi mbadala kwa sababu yeye ana marafiki wengi katika nchi za Arabuni ameshafanya nao mazungumzo ya awali na kuonyesha dhamira ya kusaidia kulitatua.
Alisema kwamba ingawa jambo lenyewe linahitaji ufuatiliaji, lakini yeye kwa uzalendo wake atalifanya hila pasipo ujira wowote, kwani anaogopa yaliyotokea katika sakata la umeme wa dharura kwa Tanzania Bara maarufu kama Richmond.
Raza, alisema katika kutatua tatizo la umeme Zanzibar, Serikali ya Jamhuri ya Muungano inawajibika kusaidia kwa hali na mali kwa kuwa Zanzibar ni sehemu yake na hivyo isisubiri mpaka kuombwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Ndugu zangu waandishi suala la kununua jenereta kwa ajili ya Zanzibar lenye uwezo wa kuzalisha umeme megawati 40 kwa serikali ya Muungano ni sawa na vijisenti tu, hivyo tunaomba watusaidie wenzetu kwani hata wao walipokuwa wana matatizo tuliwasaidia, " alisema.