Mafisadi EPA miaka 18 kila mmoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi EPA miaka 18 kila mmoja

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jul 26, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD][​IMG][/TD]
  [TD]MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam,

  imewahukumu washitakiwa waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya

  kujipatia fedha isivyo halali kutoka

  kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya nje [EPA] kwenda jela miaka 18 kila mmoja[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Hukumu hiyo ilitolewa jana Mahakamani ambapo waliyohukumiwa ni pamoja Rajabu Maranda na Farijala Hussein ambao ni ndugu ambapo imedaiwa ni mtu na binamu yake

  Hukumu ambayo ilisomwa na Hakimu Kahyoza na aliitoa kwa kusema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi saba wa upande wa mashtaka mahakama bila kuacha shaka imeona washtakiwa hao wana hatia kwenye makosa sita kati ya saba waliuyoshitakiwa

  Mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya washitakiwa hao kupatikana na hatia ya makosa sita kati ya saba waliyokuwa wanakabiliwa nayo ikiwemo la kujipatia fedha Sh. bilioni 2.2 za Akaunti ya malipo ya Madeni ya Nje (Epa) kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Kufuatia kifungo hicho wametimiza jumla ya miaka 18 jela ambapo awali walishahukumiwa kifungo cha miaka mitano ambapo hukumu hiyo itakwenda sambamba na kile cha awali

  Hukumu hiyo ya imeainisha kuwa kwa kila kosa watatumikia miaka mitatu jela ambapo wamepatikana na makosa sita limo la kula njama, kughushi nyaraka, kuwasilisha hati bandia na kujipatia Sh. 2,266,049,041.25 kutoka katika Benki hiyo

  Kwa mujibu wa Hakimu, washtakiwa hao wataanza kutumikia kiifungo hicho kuanzia jana sambamba na kifungo cha awali.

  Awali katika kesi ya msingi, washtakiwa hao walidaiwa kuwa Machi 20 -25 Desemba, mwaka 2005 washitakiwa hao walijipatia hizo wakidai kwamba Kampuni ya B.Graciel ya Ujerumani imehamishiwa deni na Kampuni ya Money Planers & Consultant ya Tanzania.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Mafisadi EPA miaka 18 kila mmoja
   
Loading...