Mafisadi 38 Kutajwa

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
3
  • Rais asema watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
  • Asema wananchi wakiwaona, wataamini vita inapiganwa
  • Viongozi sasa kueleza jinsi walivyopata ukwasi walionao
na waandishi wetu, Dar, Dodoma

RAIS Jakaya Kikwete ametoa kauli inayoashiria kwamba siku si nyingi, Watanzania watashuhudia vigogo 38 watuhumiwa wa ufisadi, wakifikishwa mahakamani.

Rais Kikwete ametoa dalili za kuwapo mpango huo, katika hotuba yake ya ufunguzi kwenye Mkutano Mkuu wa Nane wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), unaofanyika katika Ukumbi wa Kizota, nje kidogo ya mjini Dodoma, juzi.

Katika hotuba hiyo, Rais Kikwete alisema vigogo hao 38 wamebainika kuwa na mali yenye thamani kubwa kuliko kipato chao.

Alisema Tume ya Maadili imebainika kuwa viongozi hao wanamiliki mali ambayo maelezo yake ya namna ilivyopatikana, hayalingani na kipato chao.

Alisema baada ya kubainika, taarifa hizo ziliwasilishwa kwa uongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambao aliwaita “wanaume wa shoka.”

Rais alisema TAKUKURU wanafanyia kazi taarifa hizo kabla ya kuwafikisha mahakamani na kujigamba kwamba, mara vigogo hao watakapofikishwa mahakamani, Watanzania ndiyo wataamini kuwa Serikali haina mchezo katika vita dhidi ya rushwa.

“Kwa upande wa rushwa, tayari kesi moja iko mahakamani na wakati wowote watapeleka kesi nyingine.

“Naamini kesi hizo na nyinginezo zitakapofikishwa mahakamani, ndipo watakapojua kuwa mapambano dhidi ya rushwa ni jambo tulilodhamiria na kwamba hatulisemi idomoni tu,” alisema Rais.

Aliwahakikishia wananchi na wadau wote kwamba hakuna jambo linalotajwa kuhusu rushwa, halifuatiliwi.

“Hakuna kiongozi anayetajwa ambaye suala lake halifuatiliwi . Kila taarfa hufuatiliwa, iwe imetoka gazetini au katika mkutano wa dhahara au kwa ujumbe wa simu ya mkononi au kwa minong’ono na uvumi tu,” alisema.

Alisema Takukuru imekuwa ikifanya uchunguzi wa kina ili inapokwenda mahakamani, iwe na uhakika wa ushindi.

“Kufanya hivyo kunawapan uhakika wa ushindi mahakamani, lakini pia kunazuia watu wasionewe au kuvunjiwa heshima kwa makosa wasiyokuwa nayo. Hata mtuhumiwa ndugu zangu, anastahili kutendewa haki mbele ya vyombo vya sheria.

“Mtu hana hatia mpaka pale Mahakama au chombo husika cha sheria kitakapotamka hivyo. Ni kanuni ya msingi sana katika utoaji haki ambayo lazima tuizingatie ipasavyo,” alisema.

Alisema anajua vizuri jinsi wananchi wanavyochukia rushwa na wala rushwa, hata hivyo, alitahadharisha kuwa hasira zisiwafikishe mahali wakasahau kutenda haki.

“Ni hatari kupuuza msingi huo muhimu kwani tutatoa fursa kwa walio hodari kusema na wenye majukwaa ya kusemea kuwaonea wale wasiokuwa nayo. Tutatoa fursa kwa watu wazushi na wafitini kuwamaliza wenzao wasiokuwa na hatia.

“…Nawaomba sana wenzangu, tuchukie sana rushwa, lakini tusisahau wala kupuuza kuwatendea watu haki, huo ndiyo msingi wa utawala wa sheria,” alisema.

Kuhusu maisha bora kwa kila Mtanzania, Rais Kikwete alisema wapo waliopotosha kwa kudhani kuwa kufumba na kufumbua, Tanzania itakuwa nchi ya maziwa na asali.

“Najua maajabu yanawezekana, lakini kwenye maendeleo hayaji ghafla. Yanachukua muda kwa sababu maendeleo ni mchakato unaochukua muda kukamilika.

Alisema maisha bora yanayozungumzwa yana sura mbili, upatikanaji wa huduma za kiuchumi na kijamii zilizo bora na zinazotosheleza na upatikanaji wa mapato ambayo yakiongezeka, watu watakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kujipatia mahitaji ya maisha.

Rais Kikwete alisema miezi 23 tangu Serikali ya Awamu ya Nne iingie madarakani, tathimini ya utekelezaji dhana ya maisha bora kwa kila Mtanzania inapata mafanikio makubwa, licha ya changamoto kadhaa. Pia alisema ajira zaidi ya 300,000 zimepatikana katika kipindi hicho, dalili ambazo zinaonyesha kuwa lengo la kutengeneza ajira mpya milioni moja ifikapo mwaka 2010, litatimia.

Kuhusu Tume ya Maadili, alisema imeanzisha utaratibu wa kuhakiki taarifa za mali zinazotolewa na viongozi kwa mujibu wa sheria.

“Kwa ajili hiyo, hufanya ukaguzi wa mali za viongozi kama walivyojaza kwenye fomu ili kuthibitisha ukweli wa taarifa hizo. Fomu ya tamko imebadilika na kumtaka kiongozi kueleza jinsi alivyoipata mali , tofauti na siku zilizopita ambako alieleza tu mali na madeni aliyo nayo,” alisema.

Habari hii imeandaliwa na Waandishi Wetu, Manyerere Jackton kutoka Dodoma na Godfrey Dilunga, aliyeko Dar es Salaam.

Source: Gazeti la Mtanzania
 
let see, i bet itakuwa makatibu kata na manaibu katibu wa office. Let see this
 
Mtanzania=salva=Rostam=mtandao=Usanii..sasa Muungwana wenyewe ni mmoja wa mafisadi,unategemea nini?watajwe mara ngapi??aliyepewa tume ya Maadil;i ndio yule Mtanzania mwenzetu aliyesaini mkataba wa Richmond,
Unategemea kutakuwa na maadili,kawekwa pale kuwasafisha tena hawa wasanii..
Sijui tunaelekea wapi?Kwanini nilichagua sisiemu...najuta
 
Ni vizuri kama rais mwenyewe ametamka hivyo. Lakini issue inakuja kuwa na yeye mwenyewe anatajwa kuwa enzi hizo akiwa waziri alihusishwa, na la pili linalotia hofu unaweza kusikia kuwa mfanya biashara wa mbao kutoka Makete, au Mrina asali wa Tabora au Muuza samaki wa Mwanza ndio mafisadi wakubwa, lakini yale MASAMAKI makubwa yenyewe yanaweza kuachwa tu. Sijui kama Mheshimiwa aligusia hilo
 
Fisadi mkubwa Chenge kashika nafasi ya tatu Nec ( kundi la kifo) what do we expect?
 
“Naamini kesi hizo na nyinginezo zitakapofikishwa mahakamani, ndipo watakapojua kuwa mapambano dhidi ya rushwa ni jambo tulilodhamiria na kwamba hatulisemi idomoni tu,” alisema Rais.

Aleluia! Nazisubiri siku hizo kwa shauku kuu. Naamini haitakuwa 2010.
 
Mtanzania=salva=Rostam=mtandao=Usanii..sasa Muungwana wenyewe ni mmoja wa mafisadi,unategemea nini?watajwe mara ngapi??aliyepewa tume ya Maadil;i ndio yule Mtanzania mwenzetu aliyesaini mkataba wa Richmond,
Unategemea kutakuwa na maadili,kawekwa pale kuwasafisha tena hawa wasanii..
Sijui tunaelekea wapi?Kwanini nilichagua sisiemu...najuta

Mimi naamini hapa tunamwandama tu JK, ngoja awafikishe hao mafisadi 38 na tuwaone ndiposa tutaanza kusema kama hao mafisadi na dagaa au la. Tumpe muda, tuvute subira. Naamini uchaguzi mkuu ujao hautafika.
 
Huyu Rais ameshaweka MAZINGIRA YA SIASA kwenye hizo kesi zitakazikuja (kama kweli zitakuja)...kwa maana nyingine HAKI YA WATUHUMIWA ameshaitia kapuni kwake...hao watashtakiwa kwa sababu Rais kasema...
 
  • Rais asema watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
    [*] Asema wananchi wakiwaona, wataamini vita inapiganwa
    [*] Viongozi sasa kueleza jinsi walivyopata ukwasi walionao

Hizi ni porojo tu.... Hamna lolote hapa. Msije mkashangaa kusikia waliomo katika iyo listi ni wakutubi, medical assistants ama watu wa kawaida tu. Ila the biggest fish wenye matumbo makubwa wanapeta tu.
 
.....RAIS Jakaya Kikwete ametoa kauli inayoashiria kwamba siku si nyingi, Watanzania watashuhudia vigogo 38 watuhumiwa wa ufisadi, wakifikishwa mahakamani.
........Alisema Tume ya Maadili imebainika kuwa viongozi hao wanamiliki mali ambayo maelezo yake ya namna ilivyopatikana, hayalingani na kipato chao..........Source Gazrti la Mtanzania

Blah!Blah!Blah, Mimi binafsi zimenichosha, na infact, zinanipandisha hasira!

Pia, je kama ni kuwaangalia vipato vyao na mali walizonazo nani atabakia? Je wataanzia kwa wastaafu?, mbona hiyo idadi ni ndogo sana?
 
ni kweli kabisa...vitakamatwa vidagaa tu...hatutawaona JK eleven hata mmoja...Mzee wa porojo, anaendeleza porojo zake..
 
let see, i bet itakuwa makatibu kata na manaibu katibu wa office. Let see this


Kama uko na JK vile. Hapa tutapata list ya maaskari kadhaa, manesi kadhaa, maafisa watendaji wa kata na vijiji, maafisa maliasili kidogo na watu wanaofanana na hao, halafu tunaambiwa "Si mmeona wala rushwa, tunafanya kazi yetu".
Kumbuka kuwa kesi ya Mahalu ndio imepigwa tiktak, siku si nyingi ataachiwa huru.
Yetu macho.
 
Tumeona mafisadi wote wameshinda kwa kishindo ujumbe wa NEC kule Kizota. Leo unatuambia kuwa utawafikisha (mafisadi) mahakamani wakati unajua fika kuwa ukiwafikisha mahakamani unaihukumu CCM na huo ndiyo utakuwa mwisho wa CCM.

Kama si utani huu nini Mr. President? Hivi lini utaacha hizi kejeli na matusi ya rejareja kwa watanzania?
 
Katika hotuba hiyo, Rais Kikwete alisema vigogo hao 38 wamebainika kuwa na mali yenye thamani kubwa kuliko kipato chao.

..hii imeniacha najiuliza!is this serious?

..hawa watakuwa vigogo au vijiti?

..don't call me skeptic,but this sounds like mockery or some!

..na kama itakuwa vigogo na si vijiti,hakutakalika!
 
Mtanganyika...You are very right. It's always the underdog that gets to face the music in TZ
 
katika hayo majina 38 kuna viongozi wangapi toka upinzani ? au mafisadi hao ni kutoka chama tawala, kama hakuna mchanganyiko(not just because mchanganyiko maana najua mafisadi wapo kote kote) hiyo list batili !

Slaa, Mbowe nao wawepo ! hela za vilema, huyu nae kabwia pesa za kampeni !
 
haya sio madai yangu, bali ni kitu ambacho kipo, ulikuwa wapi wakati tunadiscuss hayo mambo hapa JF ?

tena na sio hao tu, (slaa, mbowe) wapo wengine wengine kibaooo (wanafahamiana) ! stay tuned !
 
haya sio madai yangu, bali ni kitu ambacho kipo, ulikuwa wapi wakati tunadiscuss hayo mambo hapa JF ?

tena na sio hao tu, (slaa, mbowe) wapo wengine wengine kibaooo (wanafahamiana) ! stay tuned !

Kipo kipo wapi? Na kama ndio ni hivyo kwa nini bado wanapeta uraiani kama vile hawana makosa? Kwa nini hawako gerezani? Na kama sio madai yako ni ya nani sasa? Nani anayewatuhumu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom