cheusimangala
JF-Expert Member
- Feb 27, 2010
- 2,585
- 497
Mafataki wameweka pamba masikioni lakini ilishaandikwa za mwizi ni 40, aya zinazofuata zina kile kilichompata mfanyabiashara anayedaiwa kupenda ngono na ‘videnti'.
Ijumaa iliyopita (Novemba 26, 2010), mfanyabiashara huyo ambaye aligoma kutaja jina lake, alinaswa akiwa na denti wa miaka 10, wakiingia Gesti ya Green, Sinza, Dar es Salaam.
Habari zinasema kuwa mhudumu wa gesti hiyo (jina tunaliminya) alikuwa wa kwanza kumtilia shaka mfanyabiashara huyo kabla ya wananchi wenye hasira kuingilia kati na kumpa kipigo chenye uzani mkubwa.
LIFTI NI CHANZO CHA YOTE
Siku hiyo, majira ya saa nane alasiri, denti huyo (jina lake na la shule kapuni), akiwa na sare za Shule eneo la Legho, Sinza, alisimamishwa na mfanyabiashara huyo aliyekuwa ndani ya taksi.
Habari zaidi zinasema kuwa mfanyabiashara huyo akiwa amevaa sura ya mtu mwema, alimtaka denti huyo apande kwenye gari ambaye naye kwa wakati huo alisahau tangazo la Sidanganyiki.
LIFTI MPAKA GESTI
Taarifa za mashuhuda kwa kuunganisha na maelezo ya mtoto, zinatoa picha kuwa wakiwa ndani ya taksi, mfanyabiashara huyo alimuomba mtoto huyo wakapumzike gesti na angempa shilingi 10,000.
Mtoto kusikia 10,000 kwa kuongezea chips kuku na soda akaona mtu mwema ndiyo huyo, bila kujua kwamba alichokuwa anakwenda kufanyiwa ni kitendo kichafu kupita kiasi.
Vyanzo vyetu vilisema kuwa baada ya kumpa lifti eneo la Legho, walifika mpaka kwenye Gesti ya Green iliyopo Sinza ya Madukani.
Baada ya kufika kwenye gesti hiyo, mfanyabiashara huyo aliingia kwenye nyumba hiyo ya wageni na kukodi chumba, alipopata alirudi kwenye gari kumchukua denti huyo kisha kwa mwendo wa kujiamini akaingia naye ndani.
WANANCHI WAKASEMA HAIWEZEKANI
Mhudumu baada ya kuona mteja wake anataka kuingia chumbani na mtoto huyo, akahamaki lakini kabla ya kufanya chochote, kundi la watu kutoka nje walimvaa mfanyabiashara huyo na kuanza kumpa kipigo.
Wananchi hao walianza kumpa kipigo mfanyabiashara huyo ambaye baadaye kwa kuhofia maumivu zaidi, alitimua mbio hadi kwenye taksi aliyokwenda nayo.
Watu hao wenye hasira walijaribu kumchomoa lakini mwenye gari aliomba wasivunje vioo, badala yake waasubiri Polisi wafike.
SINZA YAZIZIMA
Wananchi walijaa barabarani kushuhudia tukio hilo, hivyo magari yakawa hayapitiki na kusababisha foleni kubwa katika Barabara ya Shekilango.
Kelele za wananchi waliotaka mfanyabiashara huyo ‘asulubiwe' ziliisha pale Polisi walipofika eneo la tukio na kumchukua mtuhumiwa huyo na kwenda naye katika Kituo cha Polisi Urafiki, Dar.
KAULI YA MTOTO
Huku akilia, mtoto huyo alisema: "Mimi sikujua ananipeleka wapi, alinipa lifti, akasema atanipa shilingi 10,000 nikiingia naye gesti."
MAMA WA MTOTO
"Huyu baba lazima nimfikishe pabaya, siwezi kumuacha kwa hiki kitendo alichomfanyia mwanangu," alisema mama wa mtoto huku akigoma kutaja jina lake.
MIMI CHEUSIE NIKIWA KAMA MAMA MTARAJIWA ROHO YANGU IMEUGUA SANA KWA KITENDO HIKI.
NAKILAANI SANA HICHI KITENDO NA NINAWAWEKA WANAUME WOTE WENYE TABIA KAMA HIZI KATIKA KUNDI MOJA NA NGURUWE.
MAFATAKI MSHINDWE NA MLEGEE ,VIUMBE MSIO NA HAYA WALA KUJUA VIBAYA!
m#sc#zenu!