Mafao ya kujitoa mifuko ya jamii iwe kigezo cha kuwatema wabunge wasiounga mkono mabadiliko.

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Katika kikaocha Bunge kinachokuja, suala la mafao ya pensheni lipewe kipau mbele na iwekigezo cha kuwatema wabunge wote ambao hawataunga mkono wala kuteteawafanyakazi wapewe mafao yao wakati wowote wanapoacha kazi au kufukuzwa kazi kama wao Wabunge wasivyosubiriwala kuzungushwa punde tu wanapomaliza awamu zao za Ubunge. Hatuna haja yakusubiri tufikishe miaka 60.
Wananchi, Wabunge ambao hawatatetea hoja hii,wapo Bungeni kwa maslahi ya nani? Tujiulize hili kisha chukueni hatua, na hatuani kuhakikisha wanapoteza viti vyao katika awamu ya Bunge lijalo. Vigezo namasharti kuzingatiwa. Kama vipi mafao yetu yapewe na 'interest' kwani hizo fedha zinafanyia biashara. Nawasilisha.
 
Hakuna kitu kinauma kama kushikilia pesa ya mtu kwa nguvu, kuifanyia biashara bila idhini yake na mbaya zaidi bila kumgawia faida hata kidogo. Ingekuwa chaguo langu nisingejiunga na mfuko wowote wa mafao. Hii mifuko haielekei kuwa kwa manufaa ya wachangiaji.
 
Nanukuu!!!
JF Senior Expert Member Array

[h=2]
icon1.png
Re: Wafanyakazi wa Migodi Kanda ya Ziwa watangaza Vita na Serikali[/h]
Serikali inacheza na maisha ya watu wake, maana pesa zetu hizo ndizo zinafadhili masafari ya jk, na ndiyo hayo yanayojenga daraja la kigamboni, pesa zetu zinawekezwa kwenye miradi mikubwa yenye kutengeneza faida lakini sisi wachangiaji wa hiyo mifuko wala hatunufaiki na hiyo faida. Katika mapungufu mengi ya hii serikali ni kutokuwa makini na wafanyakazi, anzia walimu, ni mgogoro, madaktari shida, sasa hivi ni matatatizo katika sekta zoote yani ni bora liende. Mtu utakuwaje mazalendo wakati serikali haikujali..... Jk anamaliza vibaya sana wakati wake​
 
Tatizo vyama vya wafanyakazi navyo havina umoja katika kuwaunganisha wafanyakazi katika hii ishu.
 
Kwa utaratibu wa bunge letu kupitisha miswaada kwa kusema ndiyooo.... itakuwa vigumu kuwabaininani kaunga mkono au laa !

Apo cha msingi tusirisubiri bunge, tukomae na serikali adi kieleweke!
 
Mimi na wategemezi wangu, tutampa kura yule mgombea ambaye pamoja na masuala mengine ataahidi kupigania kuondolewa kwa kipengele kinachozuia fao la kujitoa. Kama serikali inasoma alama za nyakati, basi ifanye jambo la maana Bunge la Oktoba, 2012.
 
Naunga Hoja! Hata wanaotaka ubunge waonyeshe kukerwa na ujambazi huu wa mchan
 
Suala hili ni nyeti sana kwa mustakabari wa Taifa letu na waajiriwa wote walio serikalini na wale ambao wapo katika sekta binafsi. Pesa zinazokatwa kama michango toka kwa wafanyakazi na kupelekwa katika mifuko hii ni mali au ni pesa za wafanyakazi wenyewe na si za serikali.

Makato (Pay as you earn-PAYE) huwa yanachukuliwa na serlikali kama kodi. Pesa inayochukuliwa na mifuko hii ya jamii (PPF, NSSF nk.), ni kwa nini haina mrejesho wowote kama riba kwa anayechangia? Kuna umuhimu sasa kwa mifuko hii kuangalia namna ya kuwawezesha wanachama wake kwa kuwapa au kutoa riba kadri mwanachama alivyochanga.

Kama pesa ambazo zimechangwa na wanachama na pesa hizo zikawekezwa kwenye mradi fulani iwe ni kwa kukopesha watu binafsi au taasisi mbalimbali, kwa nini faida yake isigawanywe kwa wanachama? Huo ndio uwizi ambao wafanyakazi kama wanachama wa mifuko hii tumekuwa tukidanganywa na kuibiwa kwa muda mrefu sana.

Mungu katufunulia uozo na uovu wa viongozi wasio na utii, upendo na huruma kwa walala hoi wanaofanya kazi katika mazingira magumu kwa kukubali kupitisha na kusaini mabadiliko ya sheria ya mafao kwa wafanyakazi hasa waajiriwa katika sekta mbalimbali kwa kuongeza muda wa kuchukua mafao yao mpaka pale watakapostaafu wakiwa na umri wa miaka 55!

Hawa viongozi ni lini wamefanya makubaliano na Mungu kuhusu hitimisho la mwanadamu (mwajiriwa) hapa duniani? Pesa ya mtu aliyoitafuta kwa jasho lake ni halali yake. Ndiyo maana maandiko Matakatifu yanasema "Asiyefanya kazi na asile." Viongozi wamefanya makosa kujiamulia na kujichukulia maamuzi juu ya mali isiyokuwa yao. Ni aibu sana eti kusubiri mpaka mwezi ujao wa Oktoba, 2012 wakati wa vikao vya Bunge ndiyo wajadili.
 
umenena Mkuu!
 
Nadhani kwa hili hatuna budi kuweka madarakani serikali itakayokuwa kwa ajili ya kupigania hili.

Hii serikali ya ccm inatuburuza sana
 
Wadau wote waathirika na Sheria hii kandamizi, tuungane tulianzishe mpaka waachie fao letu! Wafanyakazi wenye machungu wani-PM.
 
Ndio maana namchukia mtu anaeishabikia serikali dhalimu ya CCM. Wanatukenulia meno tu ila wauaji wakubwa. Yaani niache kazi halafu sina hela wakati mihela yangu imekaliwa na mtu fulani. WEEEEEEE patachimbika acheni mchezo nyinyi.
 
Vita hii imeepukwa, Serikali kwa kuogopa aibu ya kushurutishwa imebadilisha sheria hii mapema kabla hapajachimbika, Serikali ifanye hivyo basi kwa kila jambo lenye manufaa kwa taifa, ubinafsi na kulindana sasa bhaaasiiii!!
 
.......

kwa hiyo ukiacha kazi ni ruksa kuchukua majasho yako..
 
Vita hii imeepukwa, Serikali kwa kuogopa aibu ya kushurutishwa imebadilisha sheria hii mapema kabla hapajachimbika, Serikali ifanye hivyo basi kwa kila jambo lenye manufaa kwa taifa, ubinafsi na kulindana sasa bhaaasiiii!!
Sheria haijabadilishwa. Wameondoa tu ile amri ya kusitisha mafao. Sheria iko vilevile na ikianza kutumika....back to 55
 
Back
Top Bottom