Mafanikio yako yanategemeana sana na maamuzi yako

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
4,102
4,228
Natamani tulione kwa pamoja hili na kama halipo sawa basi turekebishane ili tuweze kupiga hatua zaidi kutoka hapa tulipo.

Kumekuwa na tabia ya wengi wetu kulalamika san juu ya mafanikio yetu na kufikiri huenda Sisi siyo sababu ya hali zetu jambo ambalo limeendelea kutufanya kubaki katika hali ileile ya kulaumu na kutafuta wa kulaumu na tunajikuta tukisahau sehemu yetu ya msingi sana katika maisha yetu ambayo ni Maamuzi yetu juu ya vyanzo vya mafanikio vinavyopita mikononi mwetu au akilini mwetu.

Tunapaswa kufahamu kuwa maamuzi juu ya matumizi ya fedha au chanzo chochote cha mafanikio yetu ni muhimu kuliko kiasi hicho tunachokipata. Haijalishi unapokea mshahara mkubwa au mdogo kiasi gani katika kufanikiwa,mafanikio yetu kwa sehemu kubwa ni zao la maamuzi yetu yaani tunaamua nini kabla y akutumia kile tunachokipata au kinachopita mikononi mwetu mara kwa mara?

Ikumbukwe kuwa hakuna Binadamu ambaye hana maamuzi juu ya kile alichonacho au anachokipata mara kwa mara na sifa hii ya kimaamuzi ni sifa ambayo Mungu alitupendelea Wanadamu kiasi ambacho tunao uwezo wa kuamua aina ya maisha yetu na hali zetu.Jambo la msingi hapo ni aina ya maamuzi tunayoyachukua mathalani kupokea mshahara mzima na kuutumia wote bila kuacha akiba na kusubiria mshahara mwingine nayo ni maamuzi.

Kwa akina Mama kuamua kukaa nyumbani na kuitwa Mama wa Nyumbani huku fursa kibao unaziona na zina kupita ukaamua kuridhika kwa sababu una Mume na anafanya kazi nayo ni maamuzi. Mume kumkataza mkewe kufanya shughuli yoyote halali y kuingiza kipato na kuamua kujishughulisha mwenyewe wakati uwezo wa kusaidiana upo nayo ni maamuzi.
Kununua liabilities wakati unafahamu assets nayo ni maamuzi. Ni uhuru wetu kuamu lakini ni muhimu san kuangalia aina ya maamuzi tunayoyaamua mara kwa mara kwa kuwa ndiyo yanayotusababisha tuwe tulivyo.

Mimi naamini maisha yangu pamoja na sababu nyingine mabalimbali yapo yalivyo kwa sababu ya maamuzi yangu na kwa maana hiyo muda mwingi nautumia kujilaumu pale ninapoona niliamua vibaya n suala la msingi zaidi ni kukubali pia nina sehemu kubwa katika hali yangu ilivyo na sehemu hiyo inatokana na maamuzi yangu.

Kwa mfano ukiwakopesha watu wawili fedha mmoja akaamua kuizungusha ili kuzalisha zaidi na mwingine akaitumja tu kisha akaanza kufanya kazi tena ili kuipata na kulipa deni kwa wakati na ukifika wakati wa kulipa wote wakakulipa hapo napo lipo la kujifunza.
Kama tunatamani kwa dhati kabisa kupiga hatua hatuna budi kuangalia kwa kina juu ya maamuzi yetu juu ya vipato vyetu vya mara kwa mara kwani pamoja na sababu nyingine nyingi umasikini au utajiri ni zao la Maamuzi ya Mtu binafsi.

Tukiangalia kipato mara kwa mara tutasema hakitoshi na ndiyo maana hata Serikali yetu imekuwa ikiongeza mishahara ya watumishi kwa imani inapunguza ugumu wa maisha lakini ilipaswa pia itoe elimu juu ya maamuzi ya matumizi ya kids ke inachokitoa kwa maendeleo ya kila mmoja na hatimaye Taifa zima. Umasikini hautaisha kama hatujaamua kuukataa kwa dhati na Mishahra kila siku itaonekana haitoshi kutokana na Maamuzi yetu tulio wengi kuwa katika mwelekeo wa kuangalia tukio badala ya sababu.
 
Ushauri mzuri sana mkuu.
Ila kwa Watanzania hasa wanaoshi jiji la Dar,wakiona uzi mrefu utaona wanauruka.
Na ndio jinsi wanavyoruka njia za kutafuta maisha kwa muda mrefu wao ni utapelii,wizi,ujanja ujanja mwingiii,kupiga dili sanaaaa.Wanataka Maisha ya short cut
Ubarikiwe kwa kutuelewesha nakutukumbusha
 
Kumbe kuna uhusiano wa kimawazo wa nilichoandika na mawazo ya wengine!!!!
 
Uliyeomba summary usijali nitafanya hivyo ingaw hata hiyo ni summary pia
 
Kwa kifupi sana mafanikio au ufukara wa Mtu ni zao la aina ya maamuzi yake@ Amenn
 
Safi sana mkuu mleta mada nimenufaika na elimu uloitoa na nimechunguza maisha yangu na ya jirani yangu nikaona ukweli ndani yake.
 
Back
Top Bottom