Mafanikio ya Utawala wa Jakaya Kikwete ndani ya Miaka 10

Valuhwanoswela

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
1,223
2,000
Fly-overs sio miradi mikubwa na hayo mabwawa ya umeme na SGR hazijakamilika bado.
Tanzania mbona tuna wajinga hivi, je ni matokeo ya bure elimu ya Magufuli? Hizo mnazoita na kuimba kuwa ni Flyovers ukweli hayo ni madaraja tu juu ya barabara zingine kama itakavyokuwa SGR hapo Dar itapita juu ya barabara za Jiji ili magari yapite bila kungoja treni ipite.

SGR ni Mradi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kama ile ya Kenya ambayo inapita juu daraja la 57km juu ya Mbuga ya Wanyama ya Tsavo ili kuruhusu Wanyama wapite chini ya treni bila kuhatarisha maisha yao.

SGR yetu, Mradi uliosisiwa Awamu ya Nne na kuanza Awamu ya Tano, ilikuwa ikamalike mpaka Morogoro mwezi Novemba, 2019, leo Waziri ametangaza rasmi kuwa sasa itafika Moro mwezi Februari, 2021. Umeme wa Stiegler's Gorge ulianza kuimbwa wakati mmoja na SGR lakini hadi leo bado ni maandalizi tu ya eneo kutakapojengwa bwawa lakini ujenzi wenyewe wa bwawa bado hata kuanza.

Awamu ya Tano ilipoingia tu madarakani ilinunua madege yakawa yanakuja moja baada ya jingine Dar nzima ikijaa Uwanjani kuyapokea sasa yakiwa yamefikia manane ya masafa marefu yakiwa wamepark tu, matatu mengine yakingojewa na wimbo wa kusifia ukiwa umepungua. Hiyo ndiyo Miradi mitatu mikubwa inayosifiwa sana na wapambe ya Awamu ya Tano ambayo imeshindikana kukamilika katika miaka 5.
 
Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
3,793
2,000
Hili jamaa mwamba sana, lkn namuombea kwa Mungu tu asonge mbele ki afya! yaaani jakaya yaaaaani Baba wewe ni Mutu ya watu hakika Mungu akujalie afya njema na alikuchagua haswa hkn njia nyingine tuna kukumbuka sana naomba Mola sana sana wanao wabebe hulka yako mwenendo na Tabia yako

Mungu akulinde akutunze vyema Baba!!! na kila mutu asema Amiiiinaaa!!!
 
ighaghe

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
2,257
2,000
Poa! Ila JPM ana msimamo , hayumbishwi , katika kipindi chote ulishaona nidhamu kazini kama awamu hii?
Huwezi sifia awamu hii kwa kuponda awamu iliyopita. Nidhamu unaipima vipi? JPM na JK hawafanani ila wote wameitoa nchi sehemu moja kwenda nyingine bila kujali nani kafanya zaidi.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,291
2,000
Asante sana. Hata ukimpa jiwe miaka mingine 10 hatoweza kufanya hayo, sijui ni mradi gani wa jiwe ulio mkubwa umekamilika hadi sasa lakini hizo kelele zake utafikiri anafanya jambo ambalo viongozi waliopita hawakulifanya.
Miradi ya Jiwe ni SGR, Stiglers Gorge na ATCL.

Na kabakiza miaka 3 tu, halafu yote imeFLOP.

Halafu ana roho ya Uharibifu, akigusa kitu lazima kiharibike: Korosho, Ajira, Mbaazi, Elimu, Bunge, mahakama et al
 
dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
664
1,000
Orodha ni ndefu mimi nayakumbuka haya:

1. Daraja la Kigamboni
2. Daraja La Kilombero
3. Daraja la Umoja
4. Daraja la Maragarasi
5. Chuo Kikuu cha Dodoma na vinginevyo vingi
6. Hospitali ya Mloganzila
7. JNIA terminal III
8. DART(Mwendo kasi)
9. Sekondari za Kata nchi nzima kila kata ina shule.
10. Mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria
11. Songwe Airport
12. Kigoma Airport
13. Tabora Airport
14. Umeme wa REA
15. Benjamin Mkapa hospital Dodoma
16. Chuo kikuu cha Nelson Mandela Arusha
17. Dangote industry
18. Bomba la gesi Mtwara Dar
19. Kinyerezi I&II
20. Hospitali ya Moyo
21. MOI
22. Nchi nzima kuunganishwa kwa barabara za lami(zaidi km 14000 zilijengwa nchi nzima)
23. Umeme kwa makao makuu ya wilaya
24. Kuvusha Umeme Zanzibar
25. Ujenzi wa Mkongo wa taifa wa mawasiliano(leo tunajimwambafai na internet matunda ya JK)
26. JNICC Conference Center(Ukumbi wa kisasa)
27. Hata CCM wenyewe aliwajengea ukumbi wa kisasa Dodoma.
28. Nyongeza ya mishahara kwa watumishi kila mwezi Julai
29. Ajira kila mwaka hasa walimu bila Kijali umesomea sanaa au sayansi
30. Annual Increment ilikuwa haki ya Mtumishi.
32. Diplomasia ya kimataifa ilikuwa juu katika ukanda wa maziwa makuu.
33. Demokrasia iliyopevuka hasa chama ya sasa kufanya mikutano.
34. Aliwagomea CCM wenzangu na kuwaambia hoja za kisiasa hujibiwa kisiasa, sio kwa kipigo cha polisi.
35. Uhuru wa vyombo ya habari.
36. Maisha bora kwa wanajeshi wetu kupitia Maduka Yao maalum.
37. Mikopo bodi ya mikopo uwe unasoma sanaa au sayansi,na Makato yaliyozingatia sheria
38. Watumishi Wengi wa umma walijiendeleza kielimu,na wengi sana walijenga Nyumba bora.

Hayo ni machache ya Mwamba Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete lakini hakujimwambafai.

Hawa wanaomtukana na kusema kuwa tulichelewa mno Vp?

Naomba nawe utukumbushe Mambo makubwa
Sijaona kanda ya ziwa ilipata nini tukumbushane.
 
Nakapanya

JF-Expert Member
May 22, 2012
2,098
2,000
Na miradi mingi aliyoifanya ndiyo imepelekea mifuko ya hifadhi ya jamii kufilisika,hivi vikokotoo tunaletewa ni makosa yaliyofanywa na JK.
 
mlimilwa

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,421

Siokweli.
Kosa alilofanya jpm kaanza na matumiz makumwa kuliko anacho pata.

Sawa kulipwa mshahala wa laki 1,matu miz ya laki na 80.
Lazima ufeli.
Na ndio maana hata hiyo miladi anayo anzisha sio bora na haitaisha.

Wakati anaingia alijigamba nchi imehalibiwa na sasa anakoendea ndio ataiacha ameivuluga kuliko wakati ote uliopita.
 
uliza hela za kujenga UDOM zimetoka wapi.
Uliza hela za kujenga daraja la kigamboni zimetoka wapi and maby more.

Mizigo mingibe imesababishwa na JK tusimsingizie JPM
 
mlimilwa

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,421
2,000
uliza hela za kujenga UDOM zimetoka wapi.
Uliza hela za kujenga daraja la kigamboni zimetoka wapi and maby more.

Mizigo mingibe imesababishwa na JK tusimsingizie JPM
Ukisikia mtu kaacha mzigo,angekua kaacha deni kubwa na ndan hakuna hela.

Jk kaacha deni kawaida,jpm.alipoingia akajigamba hela ipo.
Jk aliacha bajet ya mwaka anakusanya tilion 19 na alikua anakadilia matumizi ya tilion 21-22.

Huyo unaemtetea amepokea nchi ikiwa inakusanya.tilion 19 kwa mwaka akasema hela tunayo,akaanza kuvuluga matajili na vitisho kwa wenye pesa/ na wafanya biashara wakubwa.

Wakati anafanya hayo amesahau.kwamba kiwango cha kukusanya pesa kitashuka matokeo yake anakadilia bajet ya tilion 29.5.

Na tayali ameanzisha miladi.mikubwa kabisa kwa mpigo.
Matokeo yake anaongeza deni wakati huohuo anajisifu.yeye ni tajili.
YAAN,,.SAWASAWA LEO JAMAA YAKO.ANAKUJA KUKUKOPA HELA KUA ANASHIDA HALAFU UNAKUTANANAE TAANI NA BIA MKONONI HUKU ANAJIGAMBA KUA NI TAJILI NA HATA WEWE ULIEMKOPESHA.ANAKUTISHA.

kwa haraka hapa ndipo.serkali ya magu ndipoilipo teleza.
Na nakwambia asipokua makini atakabidhi nchi ikiwa hoi kabisa.

Deni limepanda mala 2 ya jk,kodi imekua kubwa mtaani.
Lakini bado maisha ndio yanazidi kua magumu.kabisa.
 
Kwa ufupi magu.hana wachumi wazuri ingawa wengi walisema hashauliki.
Hivyo ndivyo ilivyo.

Pesa kidogo matumiz makubwa.
 
pilipili--mbuzi

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
1,735
2,000
Orodha ni ndefu mimi nayakumbuka haya:

1. Daraja la Kigamboni
2. Daraja La Kilombero
3. Daraja la Umoja
4. Daraja la Maragarasi
5. Chuo Kikuu cha Dodoma na vinginevyo vingi
6. Hospitali ya Mloganzila
7. JNIA terminal III
8. DART(Mwendo kasi)
9. Sekondari za Kata nchi nzima kila kata ina shule.
10. Mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria
11. Songwe Airport
12. Kigoma Airport
13. Tabora Airport
14. Umeme wa REA
15. Benjamin Mkapa hospital Dodoma
16. Chuo kikuu cha Nelson Mandela Arusha
17. Dangote industry
18. Bomba la gesi Mtwara Dar
19. Kinyerezi I&II
20. Hospitali ya Moyo
21. MOI
22. Nchi nzima kuunganishwa kwa barabara za lami(zaidi km 14000 zilijengwa nchi nzima)
23. Umeme kwa makao makuu ya wilaya
24. Kuvusha Umeme Zanzibar
25. Ujenzi wa Mkongo wa taifa wa mawasiliano(leo tunajimwambafai na internet matunda ya JK)
26. JNICC Conference Center(Ukumbi wa kisasa)
27. Hata CCM wenyewe aliwajengea ukumbi wa kisasa Dodoma.
28. Nyongeza ya mishahara kwa watumishi kila mwezi Julai
29. Ajira kila mwaka hasa walimu bila Kijali umesomea sanaa au sayansi
30. Annual Increment ilikuwa haki ya Mtumishi.
32. Diplomasia ya kimataifa ilikuwa juu katika ukanda wa maziwa makuu.
33. Demokrasia iliyopevuka hasa chama ya sasa kufanya mikutano.
34. Aliwagomea CCM wenzangu na kuwaambia hoja za kisiasa hujibiwa kisiasa, sio kwa kipigo cha polisi.
35. Uhuru wa vyombo ya habari.
36. Maisha bora kwa wanajeshi wetu kupitia Maduka Yao maalum.
37. Mikopo bodi ya mikopo uwe unasoma sanaa au sayansi,na Makato yaliyozingatia sheria
38. Watumishi Wengi wa umma walijiendeleza kielimu,na wengi sana walijenga Nyumba bora.

Hayo ni machache ya Mwamba Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete lakini hakujimwambafai.

Hawa wanaomtukana na kusema kuwa tulichelewa mno Vp?

Naomba nawe utukumbushe Mambo makubwa
Hizi namba ndizo zitawaondoa CCM madarakani mwaka 2025;
29,30 na 37.
 
Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
8,042
2,000
Ukisikia mtu kaacha mzigo,angekua kaacha deni kubwa na ndan hakuna hela.

Jk kaacha deni kawaida,jpm.alipoingia akajigamba hela ipo.
Jk aliacha bajet ya mwaka anakusanya tilion 19 na alikua anakadilia matumizi ya tilion 21-22.

Huyo unaemtetea amepokea nchi ikiwa inakusanya.tilion 19 kwa mwaka akasema hela tunayo,akaanza kuvuluga matajili na vitisho kwa wenye pesa/ na wafanya biashara wakubwa.

Wakati anafanya hayo amesahau.kwamba kiwango cha kukusanya pesa kitashuka matokeo yake anakadilia bajet ya tilion 29.5.

Na tayali ameanzisha miladi.mikubwa kabisa kwa mpigo.
Matokeo yake anaongeza deni wakati huohuo anajisifu.yeye ni tajili.
YAAN,,.SAWASAWA LEO JAMAA YAKO.ANAKUJA KUKUKOPA HELA KUA ANASHIDA HALAFU UNAKUTANANAE TAANI NA BIA MKONONI HUKU ANAJIGAMBA KUA NI TAJILI NA HATA WEWE ULIEMKOPESHA.ANAKUTISHA.

kwa haraka hapa ndipo.serkali ya magu ndipoilipo teleza.
Na nakwambia asipokua makini atakabidhi nchi ikiwa hoi kabisa.

Deni limepanda mala 2 ya jk,kodi imekua kubwa mtaani.
Lakini bado maisha ndio yanazidi kua magumu.kabisa.
Ilikuwaje tukampeleka ICC?? Soma comments zenu kipindi hicho alafu linganisha na Sasa mnavyosema. Kisha jipigeni kifuani na kusema "sisi ni wajinga"
 
Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
8,042
2,000
Tanzania mbona tuna wajinga hivi, je ni matokeo ya bure elimu ya Magufuli? Hizo mnazoita na kuimba kuwa ni Flyovers ukweli hayo ni madaraja tu juu ya barabara zingine kama itakavyokuwa SGR hapo Dar itapita juu ya barabara za Jiji ili magari yapite bila kungoja treni ipite.

SGR ni Mradi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kama ile ya Kenya ambayo inapita juu daraja la 57km juu ya Mbuga ya Wanyama ya Tsavo ili kuruhusu Wanyama wapite chini ya treni bila kuhatarisha maisha yao.

SGR yetu, Mradi uliosisiwa Awamu ya Nne na kuanza Awamu ya Tano, ilikuwa ikamalike mpaka Morogoro mwezi Novemba, 2019, leo Waziri ametangaza rasmi kuwa sasa itafika Moro mwezi Februari, 2021. Umeme wa Stiegler's Gorge ulianza kuimbwa wakati mmoja na SGR lakini hadi leo bado ni maandalizi tu ya eneo kutakapojengwa bwawa lakini ujenzi wenyewe wa bwawa bado hata kuanza.

Awamu ya Tano ilipoingia tu madarakani ilinunua madege yakawa yanakuja moja baada ya jingine Dar nzima ikijaa Uwanjani kuyapokea sasa yakiwa yamefikia manane ya masafa marefu yakiwa wamepark tu, matatu mengine yakingojewa na wimbo wa kusifia ukiwa umepungua. Hiyo ndiyo Miradi mitatu mikubwa inayosifiwa sana na wapambe ya Awamu ya Tano ambayo imeshindikana kukamilika katika miaka 5.
Unafki utawaangamiza.
Huyu jk mliompeleka ICC leo ndio unamsifia hivyo? Soma comments zenu kipindi hicho kwenye huu uzi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom