Mafanikio ya Utawala wa Jakaya Kikwete ndani ya Miaka 10

Kasegela

Senior Member
Mar 24, 2019
123
500
Kumekuwepo na vijembe na lugha za kejeli zinazotolewa na baadhi ya viongozi kutuhumu awamu zilizopita hasa awamu ya tano kana kwamba wao waliiba na hakuna maendeleo waliyoyafanya.

Orodha ni ndefu mimi nayakumbuka haya.

1. Daraja la Kigamboni
2. Daraja La Kilombero
3. Daraja la Umoja
4. Daraja la Maragarasi
5. Chuo Kikuu cha Dodoma
6. Hospitali ya Mloganzila
7. JNIA terminal III
8. DART(Mwendo kasi)
9. Sekondari za Kata nchi nzima kila kata ina shule.
10. Mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria
11. Songwe Airport
12. Kigoma Airport
13. Tabora Airport
14. Umeme wa REA
15. Benjamin Mkapa hospital Dodoma
16. Chuo kikuu cha Nelson Mandela Arusha
17. Dangote industry
18. Bomba la gesi Mtwara Dar
19. Kinyerezi I&II
20. Hospitali ya Moyo
21. MOI
22. Nchi nzima kuunganishwa kwa barabara za lami(zaidi km 14000 zilijengwa nchi nzima)
23. Umeme kwa makao makuu ya wilaya
24. Kuvusha Umeme Zanzibar
25. Ujenzi wa Mkongo wa taifa wa mawasiliano(leo tunajimwambafai na internet matunda ya JK)
26. JNICC Conference center(Ukumbi wa kisasa)
27. Hata CCM wenyewe aliwajengea ukumbi wa kisasa Dodoma.
28. Nyongeza ya mishahara kwa watumishi kila mwezi julai
29. Ajira kila mwaka
30. Annual Increment ilikuwa haki ya Mtumishi.
32. Diplomasia ya kimataifa ilikuwa juu katika ukanda wa maziwa makuu.
33. Demokrasia iliyopevuka
34. Aliwagomea CCM na kuwaambia hoja za kisiasa hujibiwa kisiasa, sio kwa kipigo cha polisi.
Hayo ni machache ya Mwamba Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete lakini hakujimwambafai.

Hawa wanaomtukana na kusema kuwa hakufanya chochote zaidi ya wizi na ufisadi walikuwa wanaishi nchi gani?

Hivi huyo wanaemtukuza amefanya jambo gani kubwa linalofikia hata robo ya mkubwa aliyoyafanya Kikwete?

Kwakuhitimisha Kikwete alifanya makubwa na Mikopo aliyokopa kila mmoja ananufaika nayo na vitu vinaonekana.

Naomba nawe utukumbushe Mambo makubwa yaliyofanywa enzi za Jakaya.

Tiririka .....
 
britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,708
2,000
Kwa Kifupi Kikwete kafanya Mambo mengi sema kosa alilofanya ni kuruhusu watu wamchezee sharubu

Kikwete Kaongeza Hospital kadhaa
While za Kata
Nyumba za watumishi wa Umma kama Polisi na Walimu
Vivuko nchi nzima
Barabara za kutosha
Kajenga Mwendo kasi
Kajenga uwanja wa Ndege terminal 3 japo JPM kaja kuizindua tu
Kajenga viwanja vya ndege Songwe, Bukoba, Mbeya, na Mwanza
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
8,067
2,000
1. Bomba la gas, Mtwara to Dar Zaidi ya
600km.
2. Mtambo wa kuchakata gas Madimba
plant pale msimbati mtwara.
3. Ndie Rais aliyeiongezea Tanesco uwezo
wa kuzarisha umeme kwa kuiwezesha
kumiliki plants kadhaa kuwa mali ya Tz,
Tegeta plant 75MW, Ubungo plant
100MW, Mwanza nyakato plant 60MW,
Kinyerezi 1& 2 100MW+.
4. TRA waliongeza makusanyo mara tisa
zaidi kutoka alipopokea kijiti mpaka
anaondoka aliacha TRA wanakusanya
900bilions wakati alipokea 100bilion
kutoka kwa BWM, hii ilikuwa matokeo ya
kupromote sekta binafsi..

MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI, JK ALIFANYA SEHEMU YAKE.
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,349
2,000
Kikwete Kilichomponza Ni Mtandao Uliojipenyeza Kwenye Serikali Yake Na Kutengeneza Corrupted Ruling System. Kwa Kuwapa Fadhira Waliomuweka Madarakani, Ndio Maana Alipambana Kumzuia Lowassa Kwenda Ikulu Ili Yasijirudie Yakwake.

All In All Aliyoyafanya Mazuri Ni Mengi Kuliko Mabaya Yake Mnyonge Mnyongeni Lakini Haki Yake Mpeni"
 
Sir Khan

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
5,120
2,000
Wale waliotuhakikishia kipindi cha awamu ya nne kuwa Kikwete hajafanya lolote ndio leo wamegeuka na kuanza kuorodhesha yote aliyofanya.
Wale waliosema ccm tangu uhuru haijawahi kufanya chochote leo wamekuwa waimba pambio wa kusifia mambo yaliyofanywa na awamu nne zilizopita.

Kikwete na Mkapa ni viongozi ovyo kuwahi kutokea nchi hii, hata yule baba yenu wa taifa naye ovyo japo yeye alijitahidi compared to those couple above.
Nikiona watu leo wanamsifia Kikwete nachoka kabisa na kujiuliza how stupid these black people are.

Nikisema Waafrika wengi ni viumbe wapumbavu mnaanza kulia mara ooh Sir Khan mbaguzi.
Magufuli wanyooshe hawa watu mpaka akili ziwarudie.
 
JAY MTAALAM

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
1,585
2,000
Kumekuwepo na vijembe na lugha za kejeli zinazotolewa na baadhi ya viongozi kutuhumu awamu zilizopita hasa awamu ya tano kana kwamba wao waliiba na hakuna maendeleo waliyoyafanya.

Orodha ni ndefu mimi nayakumbuka haya.

1.Daraja la Kigamboni
2.Daraja La Kilombero
3.Daraja la Umoja
4.Daraja la Maragarasi
5.Chuo kikuu cha Dodoma
6.Hospitali ya Mloganzila
7.JKNIA terminal III
8.DART(Mwendo kasi)
9.Sekondari za Kata nchi nzima kila kata ina shule.
10.Mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria
11.Songwe Airport
12.Kigoma Airport
13.Tabora Airport
14.Umeme wa REA
15.Benjamin Mkapa hospital Dodoma
16.Chuo kikuu cha Nelson Mandela Arusha
17.Dangote industry
18.Bomba la gesi Mtwara Dar
19.Kinyerezi I&II
20.Hospital ya Moyo
21.MOI
22.Nchi nzima kuunganishwa kwa barabara za lami(zaidi km 14000 zilijengwa nchi nzima)
23.Umeme kwa makao makuu ya wilaya
24.Kuvusha Umeme Zanzibar
25.Ujenzi wa Mkongo wa taifa wa mawasiliano(leo tunajimwambafai na internet matunda ya JK)
26.JKN Comference center(Ukumbi wa kisasa)
27.Hata CCM wenyewe aliwajengea ukumbi wa kisasa Dodoma.
28.Nyongeza ya mishahara kwa watumishi kila mwezi julai
29.Ajira kila mwaka
30.Annual Increment ilikuwa haki ya Mtumishi.
32.Diplomasia ya kimataifa ilikuwa juu katika ukanda wa maziwa makuu.
33.Demokrasia iliyopevuka
34.Aliwagomea CCM na.kuwaambia hoja za kisiasa hujibiwa kisiasa,sio kwa kipigo cha polisi.
Hayo ni machache ya Mwamba Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete lakini.hakujimwambafai.

Hawa wanaomtukana na kusema kuwa hakufanya chochote zaidi ya wizi na ufisadi walikuwa wanaishi nchi gani?

Hivi huyo wanaemtukuza amefanya jambo gani kubwa linalofikia hata robo ya mkubwa aliyoyafanya Kikwete?

Kwakuhitimisha Kikwete alifanya makubwa na Mikopo aliyokopa kila mmoja ananufaika nayo na vitu vinaonekana.

Naomba nawe utukumbushe Mambo makubwa yaliyofanywa enzi za Jakaya.

Tiririka .....
Usisahau na nyumba za pale Monduli..Ova
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
8,067
2,000
Kikwete Kilichomponza Ni Mtandao Uliojipenyeza Kwenye Serikali Yake Na Kutengeneza Corrupted Ruling System. Kwa Kuwapa Fadhira Waliomuweka Madarakani, Ndio Maana Alipambana Kumzuia Lowassa Kwenda Ikulu Ili Yasijirudie Yakwake.

All In All Aliyoyafanya Mazuri Ni Mengi Kuliko Mabaya Yake Mnyonge Mnyongeni Lakini Haki Yake Mpeni"

Hili uliloliona wengi wanajifanya hawalioni, JK anapashwa kupongezwa kwa kulisaidia Taifa na kutoruhusu lile kundi lake kuingia Ikulu, JK angeamua Lowassa awe Rais na ampiganie leo hii EL angekuwa Ikulu..

JK ndiye angepaswa atembee na ulinzi wa kutosha kwa kitendo kile cha kuwageuka wenzake mapema kabisa but he did not zaidi ya kutumia akili za kimedani nafikiri wazee akina Butiku nk wanafahamu risk aliyokuwanayo JK wakati ule.
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
8,067
2,000
Wale waliotuhakikishia kipindi cha awamu ya nne kuwa Kikwete hajafanya lolote ndio leo wamegeuka na kuanza kuorodhesha yote aliyofanya.
Wale waliosema ccm tangu uhuru haijawahi kufanya chochote leo wamekuwa waimba pambio wa kusifia mambo yaliyofanywa na awamu nne zilizopita.

Kikwete na Mkapa ni viongozi ovyo kuwahi kutokea nchi hii, hata yule baba yenu wa taifa naye ovyo japo yeye alijitahidi compared to those couple above.
Nikiona watu leo wanamsifia Kikwete nachoka kabisa na kujiuliza how stupid these black people are.

Nikisema Waafrika wengi ni viumbe wapumbavu mnaanza kulia mara ooh Sir Khan mbaguzi.
Magufuli wanyooshe hawa watu mpaka akili ziwarudie.

Unauhakika gani kama mtoa maada ndio wale, binafsi JK toka akiwa Rais niliyaona haya, nilimponda pale alipokosea..Maana anapokosea hatupaswi kukaa kimya.. Lakini pia hata mliompigia makofi kipindi kile ndio mnaomponda sasa...
 
Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,688
2,000
Kikwete Kilichomponza Ni Mtandao Uliojipenyeza Kwenye Serikali Yake Na Kutengeneza Corrupted Ruling System. Kwa Kuwapa Fadhira Waliomuweka Madarakani, Ndio Maana Alipambana Kumzuia Lowassa Kwenda Ikulu Ili Yasijirudie Yakwake.

All In All Aliyoyafanya Mazuri Ni Mengi Kuliko Mabaya Yake Mnyonge Mnyongeni Lakini Haki Yake Mpeni"
Ni Mtandao Uliojipenyeza Kwenye Serikali Yake Na Kutengeneza Corrupted Ruling System. Kwa Kuwapa Fadhira Waliomuweka Madarakani,
bora hako kakundi hakakuathiri mishahara wala biashara za watu
Hebu niambia kwa sasa Kabila zima kila kona kila wilaya, hata wakwere umewasikia kwenye ukurugenzi wowote?
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
9,371
2,000
Kwani wewe unadhani hawajui kuwa JK kafanya kazi nzuri sana
Ila tu inabidi wamshushe kwa sababau wasipofanya hivyo viatu vya JK ni vikubwa sana kwa wao kuvivaa!

Ngoja niongeze vitu vingine katika achievement za JK

35. Zana nzito za kutisha za jeshi letu
36. Mfumo wa IT wa kukusanya mapato wa Halmashauri na e-Government
37. Ajira kwa vijana (Bodaboda, Bajaji, M-Pesa, Tigo-Pesa, HalotelMoney)
38. Kununua Vivuko kibao nchini kwa mfano kununua MV Magogoni, MV Utete, ununuzi wa MV Pangani, MV Kinesi etc
39. Kufanyia repair vivuko kibao kama vile MV Alina, MV Kigamboni, MV Sebgerema etc
40. Miradi kibao ya Kilimo kwa mfano kufungua chuo kuu cha kilimo cha Mwalimu Nyerere huko Butiama
41. Miradi ya maji ya bomba na visima kibao, mfano Maji ya bomba ni mradi kama wa Ruvu chini unaosupply Bagamoyo, Bunju na Makongo
42. Kuongezeka kwa wanafunzi wanaopata mkopo chuo kikuu, Ikumbukwe JK ndo aligeuza vyuo vinavyotoa advanced diploma kuwa vya digree na alitoa mikopo kwa wanafunzi wengi mno katika utawala wake
43. Kwenye afya alipambana vilivyo na ugonjwa wa Malaria,
44. Kwenye Kilimo wakulima wa Kahawa, Korosho, Mbaazi, Alizeti, walipata neema sana
45. Aliibadirisha sheria ya madini ile ya mzee Ben angalau tukaanza kunufaika na madini (Achilia mbali sarakasi za kina profesa mruma za kudai kuwa tumeibiwa na ACACIA madini na kodi vyenye thamani ya trilion 425 )
46. Aliukarabati uwanja wa mpira wa Uhuru (Shamba la Bibi) siku hizi una majukwaa na pitch nzuri sana
47. Aliwekeza pia ktk michezo kwa mfano, kutuletea makocha wa nje kama vile Maximo na kusaidia kuleta Hamasa ya mpira na watu kuipenda timu yao ya Taifa
48. Aligawa chakula kwenye majanga kama vile njaa, penye ukame aligawa chakula, alisema hakuna ambaye angekufa kwa njaa
49. Kijeshi alitupa heshima, Aliwatwanga M23, Alimnyoosha Kanali Bacar wa Anjuani Comoro
50. Aliipa heshima TZ kidiplomasia, alisuluhisha migogoro mingi ya majirani wetu kama vile Kenya etc
51. Aliongeza ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilion 160 kwa mwezi mwaka 2005 hadi shilingi bilion 850 kwa mwezi mwaka 2015
52. Ujenzi wa nyumba za maaskari sehemu mbalimbali nchini kwa mfano huko Kimbiji, Tabata n.k
53. Mafanikio ya NHC na NSSF kwenye kujenga nyumba nzurinzuri nchi nzima za bei nafuu
53. Angalau alitutoa ushamba kwa kuvutia investment kama vile Mlimani City na Mashopping malls mbalimbali katika miji mikuu
53. Angalia daraja kama la Furahisha mwanza
54. Miradi ya stendi mbali mbali kama vile ile ya Mbezi Mwisho, Stendi ya Tegeta kwa gari zinazoenda Bagamoyo
55. Kwa mara ya kwanza tangu nchi hii ipate uhuru aliruhusu taarifa za CAG ziwe zinasomwa na kujadiliwa bungeni
56. Alituruhusu tuone Bunge Live, siku hizi wananchi hawaelewi sana kinachoendelea huko bungeni
57. Skyline ya Dar es salaam ilipendeza wakati wa JK, Dar ya mwaka 2015 ni tofauti na ile ya mwaka 2005, kulikuwa na ujenzi mkubwa wa skyscrapers Dar wakati wa kipindi chake (chukulia mfano mmoja tu pale Victoria kuelekea Morocco, na yale majengo marefu kuliko yote kule Posta city center)
58. Alianzisha mpango wa umeme vijijini wa REA (kila ulipokuwa unanua LUKU unakatwa senti kadhaa kuchangia REA)
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom