Mafanikio ya Serikali yanapimwaje??

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
19
WanaJambo wenzangu salaam... Leo nimesoma kwenye gazeti la Mwananchi, 06/12/2007. Kwa kweli sio mbaya kujitetea kwamba Serikali bado changa (miaka miwili) hili hatulikatai in "general terms" lakini hili la kwetu naomba niweke yafuatayo kwa Mhe Katibu Mwenezi kuyaangalia:

1. Tanzania ilipata Uhuru miaka 46 iliyopita chini ya TANU. Kisha tulijiunga na ASP na vyama vingine (kama vilikuwepo) kuzaa CCM (1977). Hii ni miaka takriban 30. Kwa hili basi CCM isiseme kuwa serikali yake ni changa, to me Serikali ya CCM imekuwa madarakani kuanzia 1977 (forget the 16 years since Uhuru mpaka kuzaliwa kwa CCM, for argument sake)!! Kama chama kinakiri kwamba serikali yake ni mpya (2 years) then Chama kinakiri kwanza hakuna uhusiano kati ya Serikali ya awamu ya 1, ya 2, ya 3 na hivi sasa ya 4. Sasa kwa mantiki hiyo inaonyesha kwamba CCM had never had any plan of action!! Kila awamu yaja na mpya ambacho ni "wrong".....

2. Asilimia zaidi ya 60 (kama nimekosea naomba nisahihishwe) ya Baraza la Mawaziri (leave alone few new faces at Deputy Ministerial level) wamekuwa kwenye Serikali za awamu zilizopita (some of them as long as the first Cabinet, so I hear!!). Sasa Waziri ambaye ameshakuwa waziri awamu iliyopita lazima atakuwa anakumbuka kile kilichokuwa kimepangwa na kutekelezwa wakati wa awamu ileeeeee (aliyokuwapo kabla) na inambidi kama "Professional Minister" awaelekeze na kuwaongoza wale wageni "Rookies". NAshikilia kuwa hili ni muhimu "Unless the argument in 1 above is correct".

3. Wakati wa kampeni kuna mengi yalisemwa na wagombea ambayo yalipelekea wapiga kura kuwekeza katika ndoto hizo na kepelekea ushindi wa KISHINDO (si mchezi asilimia 81!!). Miaka miwili kamili baadae, REDET wanasema wapiga kura walewale wameteremsha imani ya mpaka asilimia 44 (nusu msimu wa kishindo). Sasa kama Serikali ya CCM inatendelea kulifumbia macho hili, kuna uwezekano kuwa ikifika 2010 watakuwa na asilimia kama 12 (mean averaging). Hapo itakuwa ngumu kidogo kujitetea na sababu kama hizi za leo. Nadhani ile timu ya uchaguzi itabidi ikae na ketengeneza "Election Slogan" nzuri ili kuweza kutufumba macho sisi wapiga kura watiifu wa nci hii.

4. Sasa Mhe, nakumbuka nilipoanza kazi nilipewa miezi 6 ya "Probation". Wengi wanasema ujifunze kazi lakini sio kujifunza bali ni kutafta namna ya kutumia "Theoretical knowledge from school" kutatua "Real life problems" kwa njia muafaka. Madaktari, wanasheria nakadhalika wana "Probation period" zao. Sasa tunaomba kwa vile Chama kimekiri kwamba wao ni wageni/wapya watafiti mipango "strategic plans" zao kisha watuambie sisi wavuja jasho kwamba targets zetu ni A, B, C and timelines kufikia "milestones" zetu ni X, Y Z. Bila ya kuwa na "self identified performance indicies" watakuwa wanajaza maji kwenye gunia. Tafadhali usifikiri kusema "performance index" ni vitu kama maisha bora kwa kila MTanzania, bali ni vile vitu vitakavyopelekea MTanzania kuishi maisha bora (mfano ni: rushwa, elimu - ambayo so far so good, miundombinu, ulinzi & usalama, huduma za jamii. The list goes on..... So kila Wizara lazima iainishe targets zake na kuweza implementation plan with reasonable milestones and timelines ili siku tukitaka kujua ufanisi tuangalie zile target kama zimekuwa achieved eti!!!

5. Mwisho Mhe Katibu, ni swli ninalojiuliza nalo ni kwamba tumekuwa na chama kimoja tangu uhuru na bado kila awamu inasema bado Serikali changa ngojeni baada ya miaka (5/10) mtana vituz. Tatizo ni kwamba 46 years later bado serikali ya Awamu ya 4 tunaiita mpya hivy tuendelee kungojea. Sasa wajamani, kama tungekuwa na "Total Shifts" kama kule kwa WaMarekani (Democrats/Republicans) tungeweza pata maendeleo kweli?? Vyama vyetu ni vidogo (kwa wakati huu) lakini muda utakuja ambapo kujitetea kwa vigezo kama "tupeni muda", "ni kutokana na ukame", "wale ni wasiokipenda chama chetu", "mngechagua CCM msingekuwa hapo"; and the list goes on - itakuwa kama "kumtishia mtu mzima nyau"

Jamani mimi sio mwanasiasa bali ni Mhandisi na nimejaribu kutumia "Logic" and "Common Sense" katika kuangalia mambo yanavyoenda.

Naomba kuwakilisha na naomba masamaha kwa insha ndefu sana, nipo kwenye "lunch break" nikasema nijaribu kuweka mawazo yangu ili yajadiliwe na pale ninapokosea niwe "corrected and educated accordingly". Kweli ni refu sana, kunradhi!!!


CCM yapinga utafiti wa Redet
*Yasema si wakati muafaka kufanyika

Na Kizitto Noya
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepinga utafiti uliofanywa na Mpango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia (Redet) ulionyesha kuporomoka kwa utendaji wa serikali kwa kusema maendeleo ya nchi hayaji kama miujiza bali kwa mchakato wa muda mrefu wa utekelezaji wa ilani ya chama kinachotawala.

Akizungumza na Mwananchi jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Sera wa CCM, Kapteni John Chiligati alisema si vyema kuihukumu serikali kwa utendaji kazi katika kipindi cha miaka miwili ambacho alidai kuwa ni kifupi kupimwa kwa vigezo vyovyote vile.

Chilligati alitoa msimamo huo wa chama kuhusu ripoti ya Redet iliyoeleza kushuka kwa utendaji wa serikali ya Awamu ya Nne katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete.

Alisema ni mapema mno kutoa tathmini hiyo kwani hakuna serikali yoyote duniani inayoweza kufanya miujiza katika kipindi cha miaka miwili ya utawala.

"Maoni ya wananchi tumeyasikia na changamoto tunazifanyia kazi, lakini hatuwezi kutegemea maendeleo kuja kama miujiza, kipindi cha miaka miwili ni kidogo mno kutoa tathmini nzito kama hii ," alisema Chiligati.

Alisema tathimini hiyo inapingana na maazimio ya CCM katika mkutano wake mkuu uliofanyika mjini Dodoma mwezi uliopita ambapo wajumbe walionyesha kuridhishwa na utendaji wa serikali na kutoa maelekezo ya namna ya kusonga mbele.

Alisema wajumbe hao waliafiki kuwa ingawa serikali ina kipindi kifupi tangu iingie madarakani imejitahidi kufanya mambo mengi ya kuwaletea wananchi wake maendeleo endelevu.

Alifanunua kuwa dhana ya maisha bora kwa kila Mtanzania inayolalamikiwa na baadhi ya wananchi kwamba CCM haijaifikia, ni majumuisho ya mambo mengi ambayo tayari serikali imeyawekea mkakati wa kuyafanya kuifikia.

Alitaja mikakati hiyo kuwa ni ujenzi wa madarasa kwa ajili ya kuboresha elimu, mkakati wa ujenzi wa zahanati katika kila kata na jitihada za kuboresha miundombinu.

"Mambo hayo yote yana lengo la kumwandalia fursa mwananchi wa kawaida kuwa na maisha bora , sio suala la miujiza" alisema

Alisema CCM imepokea changamoto zilizotolewa katika ripoti ya Redet na kuzifanyia kazi, lakini ukweli unabaki kwamba ripoti hiyo haikutolewa wakati muafaka.

Aliwataka Watanzania kuwa wastahimilivu na kumpa muda zaidi Rais Kikwete kutekeleza ilani ya CCM badala ya kumvunja moyo kwa tafiti zisizojali muda katika utekelezaji wa mambo hayo.
 
Huyo Chiligati anayesema serikali ni changa,ni kwamba amekuwa waziri muda mrefu tuu hadi sasa.Sielewi uchanga katika utendaji anauingizaje hapo.Naona amejisahau kwamba ni waziri anayeongoza wizara muhimu na bado anathubutu kuutangazia umma utumbo kama huo.Kikwete ondoka na hawa watu wako!ebo, mmetuchosha mbaya sasa.
 
Umenikosha sana kuuliza jinsi ya kupima mafanikio ya serikali. Siku nyingi hili jambo limekuwa likinikera sana. Ili uweze kupima mafanikio lazima tuwe na vigezo (KPI - key performance indicators) ambavyo vimetokana na malengo (goals) yetu. Pia lazima ujuwe pia kwamba umeanzia wapi (baseline). Tatizo kubwa la malengo mengi ya serikali hayawekewi yardstick and time frame kuyatimiza.
 
Vipimo vya mafanikio ya sirikali vipo vingi sama. Kuna vya kimataifa na vya kitaifa. Vya kimataifa ni GDP na GNP, lakini mara nyingi hivi huwa havitoi picha ya halisi ya serikali husika. Hapa lazima utasikia takwimu nyingi sana, ambazo kwa hali halisi huwa sio wakilishi wa mazingira ya nchi husika.
Kwa vipimo vyangu mimi, nadhani ni vyema tukaangalia picha zifuatazo halafu tuseme kwamba je hivi ni vipimo sahihi ama sio sahihi!
 
Hawa CCM ni wababaishaji sana wanasemaje miaka miwili tu wakati chama ni kile kile wanabadilisha madereva tu lakini makondakta ni wale wale!

Mafanikio yanapimwa kwa ongezeko la ajira kwa wananchi, ongezeko la kipato na purchasing power, ongezeko la huduma muhimu kama vile upatikanaji maji safi, matibabu na madawa, idadi ya wagonjwa wanaolala chini au kushare vitanda kupunguana na dadi ya wanafunzi waokaa chini kupungua au kwisha kabisa. Haya ni baadhi tu ya mambo yanayoweza kutumika kupima mafanikio ya siri kali na haya yanapotokea basi idani kubwa ya wananchi huwa wanakubaliana nayo maana wanaona positive impact katika maisha yao ya kila siku kupitia vipato vilivyoongezeka au huduma muhimu zilizoongezeka ubora.
 
Back
Top Bottom