mafanikio ya serikali madhubuti ya ccm katika nyanja ya Uvuvi na mifugo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mafanikio ya serikali madhubuti ya ccm katika nyanja ya Uvuvi na mifugo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mujumba, May 22, 2012.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  HAYA NI BAADHI YAMAFANIKIO YA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI, YOTE HAYA YAMEFANYIKA CHINI YA SERIKALI MADHUBUTI YA CCM, LAKINI BADO KUNA WATU SIJUI NI KUKOSA UELEWA WA MAMBO WANASEMA HAKUNA KILICHOFANYIKA? NAFIKIRI WANAHITAJI KUPIMWA AKILI ZAO..

  Katika kipindi cha miaka minne kuanzia Desemba, 2005 hadi Desemba, 2009,
  Wizara imetekeleza majukumu yake na mafanikio ya utekelezaji yameainishwa
  katika maeneo yafuatayo:
  3.1 Sekta ya Mifugo
  3.1.1 Kuongezeka kwa Uzalishaji wa Mazao ya Mifugo: Maziwa,
  Nyama na Mayai
  Ili kuongeza uzalishaji wa maziwa pamoja na ulaji wake, Wizara imeendelea
  kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya kusindika maziwa, uundwaji wa

  vikundi vya kukusanya na kusindika. Usindikaji wa maziwa umeongezeka kutoka
  lita 56,580 kwa siku mwaka 2004/2005 hadi lita 88,940 mwaka 2008/2009
  sawa na ongezeko la asilimia 57.2. Aidha, uzalishaji wa maziwa umeongezeka
  kutoka lita bilioni 1.4 mwaka 2004/2006 hadi lita bilioni 1.6 mwaka 2008/2009
  sawa na ongezeko la lita milioni 200 (asilimia 13.8).
  Katika kipindi hicho, uzalishaji wa nyama uliongezeka kutoka tani 378,509 hadi
  tani 422,230. Kati ya hizo tani 225,178 nyama ya ng’ombe, tani 82,884 za
  mbuzi na kondoo, tani 36,000 za nguruwe na tani 78,168 ni za nyama ya kuku.
  Aidha, uzalishaji wa mayai uliongezeka kutoka mayai bilioni 1.8 hadi mayai
  bilioni 2.8 mwaka 2008/2009 sawa na ongezeko la mayai bilioni 1.0 (asilimia
  55.6). Ongezeko hili limetokana na mwitikio wa wafugaji kutumia chanjo
  stahimilifu ya joto ya kuzuia ugonjwa wa mdondo wa kuku. Chanjo hii
  imepunguza vifo vya kuku wa asili.
  3.1.2 Kuimarisha Mashamba ya Uzalishaji Mitamba
  Wizara imenunua jumla ya ng’ombe wazazi 570 na madume 10 kwa ajili ya
  mashamba ya kuzalisha mitamba ya Mabuki, Nangaramo, Sao Hill na Ngerengere
  ili kuimarisha uzalishaji. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na mashirika yasiyokuwa
  ya Kiserikali imesambaza jumla ya mitamba 24,549 na mbuzi wa maziwa 5,379
  kupitia mpango Kopa Ng’ombe/Mbuzi, Lipa Ng’ombe/Mbuzi katika mikoa yote
  nchini katika kipindi cha mwaka 2004/2005 hadi 2008/09.

  1.3 Kuimarisha Uhimilishaji
  Wizara imeendelea kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya uhimilishaji kama njia
  ya haraka ya kuboresha mifugo yetu. Hadi sasa Wizara imeanzisha vituo vya
  uhimilishaji katika Kanda za Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Kanda ya Ziwa
  (Mwanza), Mashariki (Kibaha) na Kati (Dodoma). Aidha, imenunua mitambo
  minne ya kutengeneza hewa baridi ya Naitrojeni (Liquid Nitrogen) kwa ajili ya
  Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) Arusha na vituo vya Kanda
  vilivyoanzishwa. Vilevile, madume 10 bora ya mbegu ya aina Ayrshire (4),
  Friesian (5) na Simmental (1) kutoka Afrika ya Kusini yamenunuliwa kwa ajili ya
  kuimarisha huduma hiyo katika kituo cha NAIC Arusha. Katika kipindi hicho, NAIC
  imezalisha jumla ya dozi 252,985 za mbegu za ng’ombe (semen) na ng’ombe
  221,183 wamehimilishwa. Uwezo wa kuzalisha mbegu bora umeongezeka
  kutoka dozi 50,000 hadi dozi 340,000 kwa mwaka na uzalishaji halisi wa
  mbegu umeongezeka kutoka dozi 37,832 hadi 74,000 na uhimilishaji kutoka
  ng’ombe 28,950 hadi ng'ombe 68,900. Mafanikio haya yanatokana na
  kuimarishwa kwa Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji – NAIC .
  3.1.4 Kuongezeka kwa Mauzo ya Mifugo na Mazao yake
  Jumla ya ng’ombe 2,496,829, mbuzi 2,014,353 na kondoo 362,154 wenye
  thamani ya shilingi bilioni 703.9 waliuzwa minadani. Aidha, jumla ya ng’ombe
  13,042 na mbuzi 13,714 wenye thamani ya shilingi bilioni 7.9 waliuzwa nje ya
  nchi, zikiwemo Comoro, Kenya, Burundi na Falme za Kiarabu. Vilevile, kiasi cha
  tani 674.0 za nyama ya ng’ombe, mbuzi na kondoo zenye thamani ya shilingi
  bilioni 2.1 zimeuzwa nje ya nchi zikiwemo nchi za Oman, Saudi Arabia, Misri,
  Kuwait, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Comoro pia Jumla ya vipande vya ngozi milioni 7.12 za ng’ombe, milioni 7.5 za mbuzi na milioni 4.42 za kondoo vilizalishwa na kuuzwa nje ya nchi na kuliingizia Taifa shilingi bilioni 58.03.1.6 Kuimarisha Mfumo wa Kutambua, Kusajili na Kufuatilia Mifugo
  na Mazao yake
  3.1.5Mfumo wa Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Mifugo
  unajumuisha kutambua mifugo kwa vitambulisho vya kudumu, kusajili mifugo iliyotambuliwa katika rejesta na kuwepo na taratibu za kusimamia na kuongoza matukio ya kuhamisha mifugo, ulishaji vyakula na matibabu. Mfumo huu unaendelea kuimarishwa ambapo hadi sasa mashamba ya mifugo 26 yenye jumla ya ngo’mbe 42,902, mbuzi 3,793, kondoo 1,134 na nguruwe 574 yametambuliwa kwa kusajiliwa kitaifa. Aidha, wafugaji wa asili 1,399 wenye jumla ya ng’ombe 133,321, mbuzi 10,739, kondoo 7,439, kuku 12,392, punda 67 wamesajiliwa kitaifa katika rejesta za vijijini. Pia, ng’ombe 124,552 wametambuliwa kwa chapa ya namba ya kitaifa
  inayoonyesha nchi (TZ),
  Ujenzi wa Mabwawa na Malambo
  Ili kukabiliana na uhaba wa maji kwa ajili ya mifugo, Wizara imekarabati na
  kujenga malambo 20 na mabwawa 2. Aidha, kupitia Mipango ya Maendeleo ya
  Kilimo ya Wilaya (DADPs) jumla ya malambo 217 yamejengwa katika maeneo
  mbalimbali. Pia, kupitia Mradi Shirikishi wa Maendeleo ya Kilimo na Uwezeshaji
  (PADEP) jumla ya malambo 193 yamekarabatiwa na kujengwa ambapo visima
  virefu 39 vimechimbwa. Vilevile, jumla ya malambo 107 yamejengwa na
  kukarabatiwa kupitia mradi wa DASIP (60) na TASAF (47) Uchunguzi wa Mwenendo wa Magonjwa ya Mifugo
  Mfumo wa utoaji tahadhari mapema kuhusu matukio ya magonjwa uliimarishwa.
  Vijitabu 2,000 vya taratibu za ufuatiliaji (Standard Operation Procedures) na
  utoaji taarifa za magonjwa ya mlipuko (TADs) na vijitabu 2,000 vyenye
  maelekezo mafupi kuhusu magonjwa (extension messages na disease fact
  sheets) vilisambazwa katika Halmashauri zote nchini. Aidha, mafunzo yalitolewa
  kwa wataalamu wa VICs na Makao Makuu ili kuwawezesha kutoa takwimu na
  taarifa za magonjwa ya mifugo kwa kutumia mfumo wa TADinfo ulioanzishwa na
  Shirika la Chakula Duniani (FAO).
  Pia Wizara imeendelea kuhimiza ukuzaji wa viumbe hai kwenye maji kwa lengo la
  kuongeza upatikanaji wa samaki na mazao mengine ya majini. Hadi sasa
  yafuatayo yamefanyika:
  · Kukamilisha Mkakati wa Kitaifa wa Uendelezaji wa Ukuzaji wa Viumbe
  Kwenye Maji (National Aquaculture Development Strategy).
  · Kuboresha vituo 8 vya kuendeleza ukuzaji wa viumbe kwenye maji
  ambavyo ni Ruhira (Songea), Kilimanjaro, Sikonge (Tabora), Mtama
  (Lindi), Kagera, Musoma, Mwanza na Kingolwira (Morogoro).
  · Kituo cha Kingolwira (Morogoro) kimeboresha teknolojia ya ufugaji wa
  samaki aina ya kambale kwa kuongeza muda wa kuishi (survival rate) wa
  vifaranga wa kambale kutoka asilimia 5 hadi kufikia 40.
  · Vituo vya Kingolwira na Mbarali vimezalisha na kusambaza vifaranga
  1,799,380 aina ya perege na 9,832 aina ya kambale kwenye mabwawa
  ya kuchimba katika Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Pwani, Dar es Salaam,
  Tanga, Tabora, Iringa, Manyara, Kilimanjaro, Mbeya na kupandikiza
  vifaranga 624,571 kwenye malambo ya asili katika mikoa ya Dodoma,
  Tanga Pwani, Rukwa, Iringa, Tabora. Shinyanga, Mara, Pwani, Kilimanjaro
  na Morogoro.
  · Vituo vya ukuzaji wa viumbe kwenye maji vya Mikoa ya Kagera,
  Mwanza, na Mtama (Lindi) vimechimba mabwawa ya mfano yanayotumika
  kama mashamba darasa kwa ajili ya wafugaji wa samaki katika maeneo
  hayo
  · Kuboresha Ufugaji wa Kambamiti kibashara unaofanywa na Kampuni ya
  Alphakrust Wilayani Mafia. Mradi huo una mabwawa 30 yenye ukubwa wa
  wastani wa hekta moja na nusu kila bwawa na uwezo wa kuzalisha
  kambamiti ni wastani wa tani 912 kwa mwaka zenye thamani ya Dola za
  Kimarekani milioni 8.5 kama mabwawa yote 76 yanayotegemewa
  kuchimbwa yatatumika. Hadi sasa mradi umezalisha tani 374.5 zenye
  thamani ya takribani Dola za Kimarekani 2,351,880
  NITAENDELEA KUWAJUZA MAFANIKIO MBALIMBALI MAANA NAONA WATU WENGI WAMEKUWA WAKIPOTOSHA WATANZANIA KUWA HAKUNA KILCHOFANYIKA..HAYA YOTE HAWAYAONI JAMANI...MAHABA NA VYAMA VYETU VYA SIASA YASITUFANYE TUWE WAPOFU
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ok tunashukuru kwa wewe nawe kuanzisha uzi, hongera sana.
   
 3. paty

  paty JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,256
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  asante mkuu kwa taarifa ya asali na maziwa, ila nashauri uongezee na FAILS, CHALLENGES na WAY FOWARD, mara zote tunashindwa kwa kuangalia upande mmoja tu
   
 4. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  asante mkuu, yote utayapata humu
   
 5. F

  FUNGO jr JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  selikali mathubut tukifananisha na ip katika dunia hii ama kweli kaz ipo
   
Loading...