jailos mrisho
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 647
- 1,360
Shida yako ni moja tu! Hujui ulichokiandika! Zezetaa za magogoniLeo gazeti za Citizen limeripoti mawakala wa Utalii kutoka Nchini Marekani wameingia Tanzania kujionea vivutio vya Utalii vilivyopo hapa nchini Kwa ajiri ya kuwaleta Wamarekani. Hii ni wiki chache tu tangu Rais Samia Suluhu Hassan afanye kipindi maarufu duniani kinachohusiana na utalii na fursa za uwekezaji cha The Royal Tour.
Ikumbukwe kuwa pamoja na kuwa na vivutio vingi vya utalii na fursa nyingi za uwekezaji, Tanzania imekuwa nyuma sana katika kupokea watalii wengi hapa Africa Kwa kupokea watalii chini ya Milioni 2 kwa mwaka. Hili limekuwa linatokea huku sekta ya utalii ikiwa ndo sekta inayochangia kwa Kiwango kikubwa zaidi pato la Taifa kabla ya kutokea Kwa janga la corona!
Kwa mafanikio haya makubwa yanayoanza kuonekana katika sekta ya utalii Tanzania inaweza kufikisha watalii Mil 5 ifikapo mwaka 2025 na pato la Taifa kukua kwa kiwango cha kutisha.
Hongera sana Rais Samia kwa Ubunifu wa kufanya program ya Royal Tour na hakika The future is now promising for Tanzania.
Go Samia! Go Tanzania