Kiukweli na pasina shaka Rais Magufuli amefanya mambo mengi sana katika taifa hili la Tanzania hasa Ujenzi wa barabara, Kuzirejesha meli zilizokuwa hazifanyi kazi kwa muda mrefu, Kukarabati shule kongwe zilizokuwa zimechakaa mfano Pamba Secondary ya Mwanza ilikuwa imejaa popo ukiiangalia sasa hivi imekuwa kama mpya na nyingine nyingi, Kuanzisha ujenzi wa treni ya mwendo kasi SGR, Kuboresha jiji la Dar es Salaam, Kuhamishia makao makuu Dodoma. Kuanza safari za treni kutoka Dar mpaka Arusha , Kuboresha huduma za Afya, Usambazaji wa umeme vijijini mfano siku nilipotembelea kijiji cha wazazi wangu na kukuta umeme unawaka sikuamini kabisa lakini ndivyo hivyo. Nawaasa vijana tusipendelee sana ushabiki wa kisiasa katika mitandao tuwe wazalendo wakufanya mambo yanayohihusu jamii kubwa na sio kujiangalia wewe kama wewe hujafanyiwa nini Rais unayemtuhumu kila siku ni kutoa matusi yasiyoleta tija kwa jamii.
Ndiyo amefanya hayo lakini kwanini asiwaongeze mishahara watumishi kama pesa ya kufanya hayo anayo hivi hayo aliyofanya yatamsaidia nini mtanzania kama mwalimu na daktari hawaongezewi mshahara ili waweze kufanya kazi yao kwa weledi hivyo ni vitu kwanini hajali watu, wastaafu wanahangaika hawalipwi pension yao kwanini.
Pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii zimechukuliwa zote kwanini. Kutowaongeza mishahara wafanyakazi kumrfanya maisha yamekuwa magumu sana kwa watanzania walio wengi ambao sasa hawaoni faida yoyote kama maisha yao hayana nafuu. Chuki inatokana na maisha ya wananchi walio wengi kuzidi kuwa magumu kila siku huku wakihubiriwa kuwa wamefika uchumi wa kati.
Wananchi wanaona maisha yao yamezidi kuwa duni kinyume na matarajio yao halafu mtu anasema unataka Rais akupe pesa, hivi kutomuongeza mfanyakazi mshahara wake kwa miaka mitano huku hali ya maisha inazidi kupanda si ni kumfanya awe fukara zaidi nini kisichojulikana.
Hata biashara zinategemea wafanyakazi wanunue hata wakulima wanategemea wafanyakazi wanunue hata viwanda vinategemea wafanyakazi wanunue sasa usipomuongezea mshahara mfanyakazi unamnyima mkulima kupata soko la mazao yake sababu mfanyakazi hana uwezo wa kununua, unamnyima mwenye kiwanda uwezo wa kuuza bidhaa zake sababu mfanyakazi hana uwezo wa kununua unamnyima mfanya biashra kupata mauzo sababu mfanyakazi hana uwezo wa kununu ndiyo tumefikishana hapa tulipo kila mtu analalamika maisha magumu. Chanzo ni serikali kushindwa kupandisha mishahara ya wafanyakazi ili iendane na gharama ya maisha.