Katika Sekta ya Kilimo, ufugaji na Uvuvi kwa Miaka mitano iliyopita Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufuta Tozo 114 kwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi. Katika kipindi kijacho Serikali imejipanga kutengeneza machinjio ya kisasa, kuendeleza na kujenga Maghala ya kuhifadhi na Vituo vya kuchakata mazao. (Ilani ya Uchaguzi Uk 33-56)
Adjustments.jpg
 
Pale mtetezi wa wanyonge anapowaletea umasikini wanyonge uleta shaka juu ya uzalendo wake. Mtetezi wa wanyonge katu hawezi Kuwasomesha namba wanyonge ili wawe masikini ili wamuabuduhttps://youtu.be/N7QJEFijpb4
Hii ni kauli ambayo ni mbaya Sana, Kwa Nini kuongoza wanyonge tuu badala ya kuongoza watu wenye uwezo wa kujinasua kimaendeleo ili tuwe Katika viwango vya kutotumika na wanasiasa Kwa maslahi yao binafsi, so disgusting kuita wanyonge!
 
Hii ni kauli ambayo ni mbaya Sana, Kwa Nini kuongoza wanyonge tuu badala ya kuongoza watu wenye uwezo wa kujinasua kimaendeleo ili tuwe Katika viwango vya kutotumika na wanasiasa Kwa maslahi yao binafsi, so disgusting kuita wanyonge!
NAfikiria kwanza,lakini bado mawazo yako yananipa mashaka kidogo.Japo nchi hiii inampa kila mtu uhuru.
 
Katika Sekta ya Kilimo, ufugaji na Uvuvi kwa Miaka mitano iliyopita Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufuta Tozo 114 kwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi. Katika kipindi kijacho Serikali imejipanga kutengeneza machinjio ya kisasa, kuendeleza na kujenga Maghala ya kuhifadhi na Vituo vya kuchakata mazao. (Ilani ya Uchaguzi Uk 33-56) View attachment 1564651
WASITUGAWE
Serikali ya Ccm Imedhamiria kuendelea kuwa nchi isiyofungamana na upande wowote ili kuweza kutetea na kulinda masilahi ya nchi yetu kwa kuzingatia misingi tunayoiamini;Kuimarisha utumishi wa umma unaozingatia weledi, nidhamu, uadilifu, bidii na maarifa katika kazi
 
Rais Dkt John Pombe Magufuli toka aingie madarakani 2015 amefanya mambo mengi sana kwa maana ukiyaanza kuyaelezea siku nzima itaisha humalizi, hii ni kutokana na Uzalendo alokuwa nao kwa kuipenda nchi yake, Uongozi ni dhamani lakini kwa Miaka yake mitano tumeona ametuheshimisha wa TANZANIA.
Mnyonge mnyongeni haki yake tumpatie.

Rais Magufuli anamaono mapana sana
Kwanza Amejenga miundombinu yote hiyo ili tuwe na uwezo wa kujitegemea,sio kila kitu tusubiri misaada kwa mabeberu. mfano mzuri kwenye huu ugonjwa wa corona kama tusingekuwa na ndege zetu ndugu zetu wa Tanzania mpaka leo hii wangekuwa Bado wako nchi za watu na wangenyanyasika mnoo.

Lakini pia adhima yake ya kufanya hivyo ni kuhakikisha mpka 2025 ajira za kutosha ziwe zimetengenezwa,na uzuri tushaanza kuona kwenye Ujenzi wa bomba la mafuta ajira Zaid ya 12,000 si hiyo tu bali nyengne zinakuja,
Huyu ndio Dkt John Pombe Magufuli

Tumpe mitano mingine akamilishe Yale ambayo ameyaanzisha
 
Ha ha imebidi nicheke. na kelele zote hizi haya ndio kayafanya. Kukomesha rushwa how , nidhamu makazini unaweza kuniambia how, airport mwanza na Dar pamoja na flyovers ni on going projects alizikuta. Alichofanya yeye ni kununua bombardier used 2 ,kujenga hostels ya wanafunzi na kupanua hicho kipande cha barabara ya moroko.
Nyingine tunasikia kila siku ni mikwara , vitisho na ubabe ,kabaki kusema fanyeni kazi. Tutaona hiyo 2020. Hajaanza hata km 50 ya lami toka aingie ikulu
Hahahaaaah!! Bombadier used 2
 
Tuacheni mihemko tumsifu pale alipopatia maana nchi ilikuwa imeoza.
Fikiri mkuu hajaenda hata dubai kuosha macho kwa Uzalendo wake.
Huu ni wendawazimu tu, watu tumekuwa wanafiki sana, kumsifia mpaka ujinga, ni heri anayekosoa maana huyo ndiye rafiki mzuri na anayependa uendeleee!!

Sifa hazikupi changamoto positive, challenges zinakupa positive thinking to conquer your ways!!

Tuache kusifiasifia hovyo hovyo kwasababu ya tamaa ya tumbo!!
 
Ajira gani unazungumzia?
Ukitoa walimu na madaktari ambao bado nao ni wanaonekana kuwa wengi.
Ajira za kada zingine kwa mashirika ya serikali zinatangazwa kila siku pitia wovuti ya utumishi Mkuu.
Hizo ajira sasa zinatosha???

Tume inatangaza nafasi 1 wanaomba watu 1000, unasema ajira anatoa???

Hiyo nafasi yenyewe watu wa tume wanapeana ndani kwa ndani, kutangaza inawekwa tu kama ushahidi!!
 
WanaJF, Takwimu hazidanganyi kwa wale waliosoma takwimu za kimataifa ni dhahiri tupo uchumi wa kati.

Kampeni za CCM zimepelekea maelfu ya wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara kujaza viwanja na kufurika.

Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania sasa wanapatiwa elimu bora kuliko wakati wowote ule tangu uhuru wa Taifa hili, wanafunzi hawa wanaajirika na kukubalika kimataifa.

Leo hii wafanyakazi wa serikali na wale wa sekta binafsi wamepunguziwa kodi kwa asilimia kubwa sana kuanzia mwezi July 2020. Punguzo la kodi limeongeza uwezo wa jamii kuuza na kununua.

Upande wa wafanyabiashara kodi zimekuwa rafiki zaidi ukilinganisha na miaka mitano kabla ya JPM, Wafanyabiashara wanaruhusiwa kulipa kodi kwa majadiliano na Mamlaka ya mapato TRA.

Aidha, Maelfu ya wanafunzi wameajiliwa serikalini kuanzia mwaka 2014. Sekta ya afya zaidi ya madaktari mia sita wameajiriwa,Karibuni zaidi ya ajira elfu kumi na tatu za walimu zimetangazwa.

Kwa upande wa wakulima mambo ni mazuri zaidi, Wakulima wa nafaka na mikunde serikali imeimarisha uhimilivu wa bei hivyo bei kutoyumbishwa na madalali wachache,Hali hii imepelekea wakulima kulima na kuuza kwa wakati,Zao la korosho limeimarika kwa kipindi cha miaka mitano baada ya serikali kuingilia kati watu waliotaka kushusha bei kwa manufaa binafsi,Serikali iliamua kununua korosho zote na kulipa kwa wakati.

Ni furaha,na Upendo kila kona ya nchi hii,Mzunguko wa pesa ni mzuri kwa wajasiriamali walio wengi na hii imepelekea kila mtu kula ,kununua na kufanya atakalo bila kuvunja katiba ya nchi.

Tutashinda kwa mbinu za kisasa zaidi kwa maendeleo ya watanzania wote.

Hoja hujibiwa kwa hoja bali si kwa matusi,Mwenye kupinga alete takwimu zake hapa JF.

Je, hatupo uchumi wa kati?
Je, wanafunzi graduate wa udaktari na ualimu hawajaajiriwa?
 
66 Reactions
Reply
Back
Top Bottom