Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Anasambaza Upendo Kwa Watu Wote
Waliomchagua Ni Wote!

Tuvumiliane Tutafika Salama.
Mabeberu Hayana Nafasi
 
Sisis wakristo makafiri... Nyangau ww mbona tunachangiaga ujenz wa misikiti mitaani... Acha ujinga na roho mbaya...
Na ukienda hospitalini ukimkuta daktar mkristo asikutibu basi maana ni kafri..
Hizi dini tumeletewa tuu zisitufanye tushindwe kuheahimiana kama watanzia..
 
For the past five years, we have seen the performance of His excellence president John Pombe Magufuli. He performed well in some areas but in many and more important areas we have seen a fiasco. Areas where he performed badly were;

  • Human rights
  • Democracy
  • Private sector
  • Creation of employment
  • And many other
However, there is one area where he performed well. This is none other than the construction of infrastructure.

We thank him for his contribution towards the development of this nation, but we humbly request him to transfer power peacefully later this year to Tundu Lissu.
 
Sisis wakristo makafiri... Nyangau ww mbona tunachangiaga ujenz wa misikiti mitaani... Acha ujinga na roho mbaya...
Na ukienda hospitalini ukimkuta daktar mkristo asikutibu basi maana ni kafri..
Hizi dini tumeletewa tuu zisitufanye tushindwe kuheahimiana kama watanzia..
Ndugu yangu hata siku moja MJINGA HAKUI hata ukimuelewesha vipi
 
Hotuba ya leo Mh.JPM ni nzuri sana imebeba maono sijasikia ukiwataja watu wale wa ajabu ajabu kwani ungefanya hivyo ni sawa na kuwapromote Hongera sana sana nimeipenda sana.
 
Habari za majumu wadau wa jukwaa hili.
.
.
.
.

Tarehe 25 October mwaka 2015 kama taifa tulifanya uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais. Miezi mitatu kabla tunakumbuka timuatimua vumbi lililokuwepo likichagizwa na chama kikuu cha upinzani CHADEMA pamoja na chama dola CCM. Kampeni zilikuwa za moto, wagombea walihaha kuwashawishi wapiga kura, hakuna upande ulikuwa na uhakika wa kushinda, mikutano ya kampeni ilizajaza nyomi isiyosimulika si tu kwa CCM bali pia kwa upinzani (UKAWA).

Tulishuhudia jinsi ambavyo wanasiasa nguli na vigogo walivyojinasua CCM na kujiunga na upinzani wakiongozwa na waziri mkuu msaafu Edward Lowasa baada ya kukatwa na kamati kuu wakati wa mchakato wa kumpata mpeperusha bendela ya urais CCM. Tukio hilo liliongeza nguvu kubwa mno kwa upinzani na kufanya kampeni kuwa na amshaamsha ya juu.

Ikumbukwe kuwa kabla ya hapo CCM ilikuwa imepoteza mvuto kwa wanachi, hii ilitokana na maisha magumu yaliyosababishwa na serikali ya CCM kwa wananchi wa kawaida, huduma mbovu za jamii ikiwemo shida ya maji mijini na vijijini, mgao wa umeme, uduni wa huduma za afya, elimu, miundombinu ya barabara na ukosefu wa ajira kwa vijana. Hii ilitokana na serikali kunuka ufisadi na rushwa iliyowaneemesha vigogo na wanasiasa wachache serikalini huku nchi ikitopea kwenye umasikini wa kunuka. Rasilimali za nchi walifaidi wazungu kwa mikataba mibovu iliyosainiwa hotel za nyota tano ikiwa na mashariti kandamizi na kuwafaidisha waporaji kwa jina la uwekezaji. Tuliibiwa sana!

Kwahiyo mpaka tunaenda kwenye uchaguzi mkuu wa October 2015, siyo vingozi wastaafu, siyo wanachama wa CCM, kila mtu alielewa ilikuwa tia maji tia maji, hata katibu mkuu CCM kipindi hicho Mzee Kinana maji yalikuwa shingoni.

Labda nikumbushe tu kuwa katika kipindi cha miaka kumi ya Rais Kikwete, serikali yake ilikumbana na kashifa za ufisadi na utakatishaji wa mabilioni ya shilingi. Vigogo waliokuwa ndani ya CCM na serikalini wengi walituhumiwa kwa skendali za ufisadi, mpaka tunaenda ngwe ya mwisho ya rais Kikwete hakuna aliyejua mrithi wake. Chama kilikuwa kimejaa mafisadi na wala rushwa, hakuna ambaye alikuwa na uafadhari wa kukubalika kwa wananchi. Swali lilibaki ni nani ataipeperusha bendera ya chama cha mapinduzi ambaye alikuwa na unafuu?

CCM ni kama walilamba dume katika uteuzi wao kwenye kamati kuu. Hapo walionyesha umahiri wao wa kuchanga kibunda cha karata na hatimae kumuibua Pombe #Magufuli. Huyu mwamba anayetokea kanda ya ziwa alikuwa naibu waziri na waziri katika wizara tofauti. Ni kwenye wizara nyingi aliweza kuacha alama, ila zaidi kwenye wizara ya ujenzi aliweza kuonyesha umahiri wake. Wazee wenzangu muliokuwepo kipindi hicho mnaweza kukumbuka alipokesha kwenye site za madaraja, alivyoigiza ni dereva wa malori na kuwanyoosha mizani na mengine mengi.

Katika historia ya nchi yetu tangu tupate uhuru hakuna kipindi tumewahi kuwa na joto la siasa la juu kiasi kile. UKAWA walijaza nyomi kubwa kwenye mikutano yao ya kampeni na CCM nao wakajaza nyomi, hii iliwapa ugumu hata wataalamu na wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini kutabiri ni nani angeibuka mshindi wa urais. Pengine lipo kundu kubwa la wananchi walioamini CCM ilikuwa inaenda kuangukia pua, labda goli la mkono litumike kuinusuru kusalia madarakani.

Yakutokea yalitokea uchaguzi ulifanyika tarehe 25 October 2015, nakumbuka siku hiyo nilikuwa msimamizi wa uchaguzi kituo fulani mkoa wa Kilimanjaro. Pombe #Magufuli alikuwa mshindi wa kiti cha urais, mwamba akaapishwa.

Pamoja na mambo mengine, mimi nikiwa mwanaharakati na mufuasi wa mageuzi, Pombe #Magufuli ndiye rais #tuliyemngoja zaidi ya miongo minne tangu tumepata Uhuru. Hapa siongelei ushabiki wa kivyama ila naongelea masilahi mapana ya nchi yangu.

Miaka mitano ya Pombe #Magufuli Tanzania kwa mara ya kwanza tumekuwa na fly over, kwa mara ya kwanza tumejenga treni ya umeme (SGR), kwa mara ya kwanza tumekuwa na ndege zaidi ya 12, kwa mara ya kwanza tunajenga bwawa kubwa la kufua umeme (stiglus gorge) litakalozalisha zaidi ya megawatts 2115 na wakati matumizi yetu kwa sasa yakiwa ni megawatts 1200 na kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru elimu ya sekondari imetolewa bure.

Mambo mengi makubwa tumeyashuhudia, kwa mara ya kwanza zaidi ya vijiji 10,000 vya Tanzania vimekuwa na umeme kutoka 2,000, huduma za maji zimeboreshwa mjini na vijijini ukiwepo mradi mkubwa wa kutoa maji ziwa Victoria kuyapeleka kwenye miji na vitongoji vya Tabora.

Pamoja na mambo makubwa na yanayopendeza aliyoyafanya katika kipindi cha miaka mitano, pia kumekuwepo na changamoto za hapa na pale. Ajira zimepotea ndani ya miaka mitano, hakuna nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi wa umma. Hivyo yapo makundi ya wahitimu wa elimu za juu katika kada mbalimbali na wafanyakazi wa umma na watu wengine ambao kwa namna moja ama nyingine hawakuguswa na utendaji kazi wa huyu Mwamba, acheni ubinafsi.

Hata kama rais atatoka mbinguni hawezi kumgusa kila mtu kwa hitaji lake, hata yesu wapo aliowakela. Tuache #ubinafi wa kumhukumu huyu mwamba toka kanda ya ziwa kwa kushindwa kutoa ajira au kutoa nyongeza ya mishahahara. Tanzania ina watu zaidi ya milioni sitini, wafanyakazi ni chini ya asilimia kumi ya watu wote. Vipi akisema awaangalie nyie tu, kundi linalobaki inakuwaje.

Hata kwa wasomi tunaohitimu vyuo tuache ubinafsi alihali tukijua sehemu kubwa ya familia zetu ni watu hawajasoma ama wameishia darasa la saba na wanahitaji maji safi, umeme, huduma za afya na barabara za lami. Rais yupo kubana matumizi kuwa na wafanyakazi wachache watakaotimiza majukumu yao kwa kuwajibika lakini pia akitekeleza miradi ya maendeleo itakayogusa maisha ya kila mtu.

Mwisho, ila si kwa ulazima, ningependa kumuona Pombe #Magufuli akiendelea kuwa rais hata baada ya ungwe yake ya pili kuisha. Watanzani! ni rahisi kumpata rais ila siyo rahisi kumpata rais mzalendo asiyepepesa macho wala kumuonea mtu aibu kwenye mambo ya maendeleo ya taifa letu. Taifa kubwa kama China wameendelea na uchumi wao kuwa tishio duniani kwa kuwa na viongozi wachapa kazi na wazalendo kwa nchi zao. Hakika miaka kumi ijayo tukiwa na magufuli naiona Tanzania taifa litakalojitegemea kiuchumi.
 
1.5 Trilioni

Ukijumlisha kashfa zote za upigaji za Kagoda, Meremeta,Buzwagi Radar, Richmond kwa pamoja hazifikii 1.5 T.

Uzalendo gani huo unaosema wewe
 
Pamoja na madhaifu yake.. lakini Magufuli amedhubutu na anahitaji kupewa miaka mingine 5.. naamini Tanzania itakua mbali sana.

Japo ndani ya hii miaka 5 anahitaji kufanya haya mambo mawili ili kuacha legacy kama Rais Bora.

1. Kuweka mezani mchakato wa katiba
2. Kuwezesha Tanzania kupata katiba mpya isiyo na mizizi ndani ya ccm.

Watu wa Dar msipo mchagua .. mtakua hamna maana kabisa.. dar inamelemeta kwa barabara za mitaani, taa, vituo vya afya, etc.

Huyu hapa ndio Rais wa kumchagua.

View attachment 1541828
Duuuuh!!!
 
  • Biashara zimekufa na zilizopo hazina matumaini ya kustawi.
  • Hali za maisha ya watu imekuwa hoi.
  • Raia wana hofu ya kutekwa na kuuawa kila mahali.
  • Hali za wakulima ziko hoi kwasabb bei za mazao zimeporomoka.
  • Wafanyakazi hali zao mbaya kwasabb mishahara yao haijawahi kuongezeka tangu Kikwete aondoke madarakani.
  • Vijana wanaomaliza vyuo wamekosa matumaini kwasabb serikali haitoi ajira.
  • Sekta binafsi imekuwa adui wa serikali (inazidi kuminywa).
OKTOBA 28 MCHAGUE JPM KUYAENDELEZA HAYA AMA MKATAE KUYAONDOA.
 
66 Reactions
Reply
Back
Top Bottom